Unafanya nini ili usifilisike na usipotee kwenye ramani? Nafsi yangu inangia huzuni na hofu nikikutana na waliofilisika

Shida ukidumu kwenye biashara moja, vipi kesho hio biashara ikaingiliwa na wababe zaidi yako?

Ndio mana watu wanajaribu kuwa na biashara japo 3 + mashamba ya matunda na miti na korosho + nyumba za kupangisha na UTT juu
Uko sahihi mkuu.

Jambo la msingi ni kuwekeza pesa sehemu pamoja na wajuzi ama ukiwa mjuzi mwenyewe.

Ni sahihi kabisa kuwa na multiple source of income
 
Katopic kazuri, ukianguka tuliza akili utaamka.

Miaka fulani nilikuwa silali hotel ambayo ni chini ya elf 50 kwenda juu.

Baadae nikauguliwa na mama mzazi nikatumia hela zote na hakupona akafariki, Kuna siku nakumbuka maeneo ya Tandika nimeingia Guest chumba elf 15 mm nina elf 10, nilimuomba mhudumu akasema nakupa ila jitahid hata kukopa kesho umalozie elf 5. Niliingia room nililia kiume kitandani nikajisemea kwamba sasa nimejua kabla hujafa hujayaona ya Dunia.

Nikaendelea kujivuta vuta nikawa saww tena baada ya miaka kama miwili.

Ila pia utawala wa huyu Hangaya haubariki biashara zangu kwa sasa, profit margin inashake balaa
Dah na mimi nipo kama wewe , Huwa sikubali kulala guest Huwa mazingira yaake yananichanganya, guest Haina Haina laundry machine, wanalipa 20 wanafanya ngono humo, wanatoa mashuka wanatandik mengine ,.kwa kwa kweli sipendi.guest na akili imejipanga hiivo, mimi Huwa kulala ni hotelini tu ,nimejifunz kitu why hotelini , kwani wengine wanapoteza nin wakila guest
 
Katopic kazuri, ukianguka tuliza akili utaamka.

Miaka fulani nilikuwa silali hotel ambayo ni chini ya elf 50 kwenda juu.

Baadae nikauguliwa na mama mzazi nikatumia hela zote na hakupona akafariki, Kuna siku nakumbuka maeneo ya Tandika nimeingia Guest chumba elf 15 mm nina elf 10, nilimuomba mhudumu akasema nakupa ila jitahid hata kukopa kesho umalozie elf 5. Niliingia room nililia kiume kitandani nikajisemea kwamba sasa nimejua kabla hujafa hujayaona ya Dunia.

Nikaendelea kujivuta vuta nikawa saww tena baada ya miaka kama miwili.

Ila pia utawala wa huyu Hangaya haubariki biashara zangu kwa sasa, profit margin inashake balaa
Umenikumbusha.

Hapo awali nilikua naona kupika ni umama daily kula kwa mama ntilie, saiv uchumu umeyumba ghafla, napika kama nimekua chef 😀
 
Moja ya jambo linalotisha kwenye maisha ni kufilisika, ulikuwa na mali zako kidogo zinakusogeza na zinakupatia chochote, una watu wamekuzunguka unawapa kazi na unawapatia chochote japo kidogo, then inatokea hiyo hali inakata, humiliki Cha maana, mission za mjini zimekata, huonekani aisee unapauka, mahitaji ya msingi unayaona ni anasa, tabia za majungu zinakurudia, kutoka kutafuta muda saizi unawaza upotezaje muda, hali hii Huwa inatisha na kuchanganya sana.

Ninapokuwa mjini na ninapokutana na kaka zangu na watu tofauti wa hapa kwetu hasa wale walionekana miaka Ile wamebotoa au wapo njiani kutoboa halafu unakuta wamechoka, uzee huu hapa, ngozi zao hazishawishi, wamechagua kufanya kazi ndogo ndogo, mara bodaboda nk, wanakuomba pesa.

Niseme ukweli mimi binafsi nafsi yangu inangia na huzuni na hofu, huwa najiuliza wao walikosea wapi na mimi nina nini cha maana ambacho kinaweza kuwa ni ngao na uhakika.

Nikiwa kanisani nimejikuta sala yangu ni kuomba, "Mwenyezi MUNGU mwingi wa upendo, azibariki siku zangu, aniondolee siku za mateso, aniepushe na mikosi, laana na mabalaa," kwani Sioni what so special nilichonacho, je wewe unafanyaje ili usikae nje ya mstari wa maisha?
Ukifika Mbeya uliza aliko Shaban Chawe aliyekuwa anamiliki mabasi ya Fresh Ya Shamba, helicopter za ukokozi enzi za elnino ya miaka ya 2000.

Alikuwa akiishi jumba la fahari eneo la Uzunguni Mbeya akiendesha Mercedes Benz latest model.

Saa hizi anaishi Mbalizi na anasafiri kwa Bodaboda kwenda kwenye shughuli zake. Ukimuona usisite kumpa Tsh 10,000 kama unayo
 
Mkuu,ili usifilisike inabidi uwe fukara,uwe maskini.

Sasa unawezaje kuwa maskini na wakati wewe ni TAJIRI?Hapo Ndipo neno la kitaalamu linaloitwa LEVERAGE linkuja.Leverage,your money,leverage,your assets,leverage you time,leverage your skills,leverage all that you think you have.As long as una leverage Basi Daima utakuwa unahitajika na As long as unahitajika Hautafilisika.

In short ukisikia watu wanakwambia FUKARA Hafilisiki basi ujue kuna maana mbili na mojawapo ni Hii ya POWER of Leverage.
 
Ukiwa kweny kilele cha mafanikio uwe na akili za uwekezaji , mtu mwenye akili ya pesa sio rahisi kufilisika labda awe mtu wa kuchukua mikopo kwa kuweka rehani mali zake .

Usipende kuwa mtu wa sifa sifa sana , uoga ni akili kama kweli ni muoga wa kufilisika lazima utawekeza mapema ...Unaweza kuwa tajiri ila ukaishi fresh tu kawaida sio umejnga nyumba ila bado matumizi makubwa . ukienda kweny maofisi makubwa utakuja hawa madogo walioajiriwa kama wageni ndio wana mbwembe sana za kununua magari mapya , anasa.

Uzuri wa maisha ili upate usingizi bora ni kusave pesa na kuwekeza ukilijua hilo basi ndio kila kitu .

Kiufupi mtu mweny elimu ya pesa sio rahisi kufilisikia , ukiwa na pesa nyingi usijaze liability nyingi wekeza kweny assets ...Hay magari unayotumia mafuta ya lak 3 ni liability .
 
Moja ya jambo linalotisha kwenye maisha ni kufilisika, ulikuwa na mali zako kidogo zinakusogeza na zinakupatia chochote, una watu wamekuzunguka unawapa kazi na unawapatia chochote japo kidogo, then inatokea hiyo hali inakata, humiliki Cha maana, mission za mjini zimekata, huonekani aisee unapauka, mahitaji ya msingi unayaona ni anasa, tabia za majungu zinakurudia, kutoka kutafuta muda saizi unawaza upotezaje muda, hali hii Huwa inatisha na kuchanganya sana.

Ninapokuwa mjini na ninapokutana na kaka zangu na watu tofauti wa hapa kwetu hasa wale walionekana miaka Ile wamebotoa au wapo njiani kutoboa halafu unakuta wamechoka, uzee huu hapa, ngozi zao hazishawishi, wamechagua kufanya kazi ndogo ndogo, mara bodaboda nk, wanakuomba pesa.

Niseme ukweli mimi binafsi nafsi yangu inangia na huzuni na hofu, huwa najiuliza wao walikosea wapi na mimi nina nini cha maana ambacho kinaweza kuwa ni ngao na uhakika.

Nikiwa kanisani nimejikuta sala yangu ni kuomba, "Mwenyezi MUNGU mwingi wa upendo, azibariki siku zangu, aniondolee siku za mateso, aniepushe na mikosi, laana na mabalaa," kwani Sioni what so special nilichonacho, je wewe unafanyaje ili usikae nje ya mstari wa maisha?
Familia bora
 
Kufilisika ni kubaya sana
 
Wakati nimeanza kazi nilikutana na Mzee mmoja ambaye alikuwa amebakiza miaka 2 kustaafu Kwa Lazima Utumishi wake.

Tukiwa kwenye kazi za Site pamoja, alikuwa haachi kuniusia usiwe kama Mimi, Kuna Siku nilipata wasaa kumuuliza kuhusu hiyo kutokuwa kama Mimi, ana maana gani.

Nilichojifunza kutoka kwake, kama Mwanaume;-
  • Kujifunza kuwekeza kadri unavyopata fursa na nafasi
  • Kubana Matumizi, huwezi kupata laki 1 sasa na ukaitumia yote Kwa mara moja kwenye Starehe n.k
  • Kupunguza Nyumba ndogo/Side chicks na kuhonga kiujanja
  • Kuwa na vyanzo vingi vya kuongeza kipato binafsi
  • Kupunguza ama kuacha Matumizi ya Pombe/Ulevi
  • Kuwa na kiasi kwenye kutoa misaada iwe Kanisani na watu wenye uhitaji
  • Kuwekeza kwenye vitu visivyoshuka Thamani i.e Ardhi/Real estate business
Katika yote, kujitahidi kulinda Afya zetu, Afya ni muhimu sana kwenye mustakabali wa maisha yetu ya kesho.

Play safe
 
Back
Top Bottom