Unafanya nini mbwa wako kuwa mkali

[emoji23] [emoji23] [emoji23] Aise mi nanao 8 ila akija mgeni asiache viatu nje maana kama hukuwatambulisha basi viatu hivyo kesho mkanunue vingine tu maana mtakutana na vijimasalia....na watu huwa wanapiga simu kuuliza kama tupo ndo ili wakpokelewe getini maana huwa ni dhoruba wakisikia mgeni
 
Daah hapo ulinzi tosha mkuu.
 
MIE NDIO NIMENUNUA MBWA WADOGO..... swali langu je _wakiwa bandani muda wote ni sahihi au niwe nawatoa kama kawaida
Mkuu ninavyojua mbwa lazima afanyiwe socialization angali mdogo, nao wanahitaji game time, wakimbie kimbie, wagale-gale kwenye vumbi kidogo,hii husaidia mbwa kuwa na mazoezi na asiwe mkali kupitiliza anaweza kujeruhi mtu. Kama bado wadogo walau saa moja wakishinda nje haina madhara.
 
Uko vizuri sana mkuu nawapenda wanyama sana na wakikosa chakula huwa niko tayari kuwapikia cha kwetu ili mradi wale tu
 
Ndo raha ya kufuga mbwa, mi nachukizwa na wageni wanaokuja bila kutoa taarifa. Yani inakua ni usumbufu, mtu anakuja saa saba msosi ushapikwa, inabidi mtu aingie tena jikoni[emoji35]
 
Usipompa jina utawasiliana naye vipi

Hapo kwenye jina nabisha, mpe jina kalikali kama simba, Chui , mamba, (hata dab ili hawe mtekaji) ili awe mkali
 
Hapo kwenye jina nabisha, mpe jina kalikali kama simba, Chui , mamba, (hata dab ili hawe mtekaji) ili awe mkali
Au Van Dame, Chuck Norris, Bolo Young, Dhamendra Khan, Bruce Lee n.k. Majina ya kibabe babe..πŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜‡
 
Nakumbuka zamani tukiwa kijijini tulikuwa tunawavutisha sigara
 
Ulitaka ajisaidie wap wakat umemfungia zaid ya masaa 12
Watu tunasafiri kwa bus zaidi ya masaa 12-18 lakini hatujisaidii kwenye bus,tunafuata utaratibu, anyway tuweke utani pembeni-mimi nina mbwa mdogo wa miezi minne alikua fala sana kipindi namchukua kelele kulalamika hovyo mpaka kero kwa majirani, pia akawa anajisaidia hovyo bila utaratibu bandani, nilianza mafunzo ya kumtrain ulaji kuwa serious na kujisaidia sehemu maalumu niliyomtengenezea bandani, kufahamu watu wote wa familia hadi watoto wadogo-saizi yuko poa hapigi kelele bila utaratibu anajisaidia sehemu yake, ugomvi wake ni kwa wageni hadi raha... Chakushangaza nguo ikidondoka kwenye kamba au viatu vinazagaa anabeba kwa mdomo wake anakuja kudondosha mlangoni kuingia ndani na bado ni mbwa mdogo kwa umri... ila upande wa chakula bado shida anataka nyama tu though ninamfundisha vyakula vingine vya mbwa mdogo mdogo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…