Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 530
- 1,446
Kwa miaka 4 sasa na mwezi mmoja nimeishi bila kujipikia nikila kwa migahawa nfanya hivi kwa maisha haya ya kutojipikia kwa sababu mimi siyo mtu wa kukaa sehemu moja nikatulia hii ni sababu ya mazingira yangu ya utafutaji nakaa sehemu kwa muda mfupi baadae naenda eneo jingine nikiridishe kwenye mada leo bhana nimeona naumia kwa siku natumia chai 1,000 hadi 1500 inategemea nimepita wapi siku hiyo maana sina kasumba ya kula sehemu moja nikazoeleka.
Mfano: Chakula cha mchana natumia 2,000 hadi 2500 nikijilipua sana labda 3000 siku zingine.
Sasa leo nikaenda nilikozoea wanasema chakula nilichokuwa nakula 2,000 leo wamepandisha ni elf 2500 hivyo hivyo hadi chai mpaka vyakula vingine!
Imebidi niulize hivi nyie kwanini imekuwa ghafla sana na hizi bei za vyakula wanasema vitu vimepanda bei na wanasema hata bajeti imekuja na mabadiliko ya vitu kupanda hivyo tuzoee!
Nimeishiwa nguvu ya kuendelea kusema chochote imebidi nilipie tu nijipange kununua vitu na mimi nianze kujipikilisha, na kupika ndio mvivu wa kwanza katika sekta hii ya kijipikia hasa kuosha vyombo ni mtihani kwangu siyo kwamba najiona hapana, sijui wengine wasema wanaona "aibu" hapana kitu nachokuwa nazembea nipale nimekula nimeshiba nikimaliza vyombo vinaniangalia tena yaani kikifikia hatua hii ndio naona kupika kazi bwana.
Kwa wenzangu ambao mnaishi maisha ya kigeto geto bila kupika, mna ushauri gani juu ya hili? Je, kuna njia rahisi za kupika ambazo hazihitaji jitihada kubwa au muda mwingi? Na je, ni vipi mnavyopambana na gharama hizi za juu za chakula nazungumzia wewe kwa wale ambao hampiki huku mkiendelea kuishi bila kujipikia? Naomba uzoefu na mawazo yenu.
Karibuni kwa mjadala!