Unafanyaje kuishi maisha ya kigeto geto bila kupika?

Sasa upike na ulie humo humo unakuwa kama homosepeansi;πŸ˜…
 
Unamshauri mtu gadgets za jikoni za 150,000 wakati chakula cha 2,500/- anajifikiria?
 
Haya maisha niliyaishi mwaka 2013-2016 nilisave sana hela πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ
 
Wee bwana lunch ya serena moja husikii njaa siku tatu...wee ni kunywa maji tuu.
Hii mbona wengi wangetajirika πŸ˜‚πŸ˜‚ kama unakula mlo mmoja unakazia na maji siku 3 πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™Œ
 
Mnaposema ukipika mwenyewe gharama haipungui muweke wazi mnakula migahawa ya chakula cha 1500-2500. Nikupe mfano mgahawa ninanokula wali au ugali nyama maharage na mbogamboga ni 5,000 jumatatu hadi jumatano, alhamisi kuna pilau 7,000 na ijumaa kuna biriani 8,000 hapo hujaongeza na maji au pepsi baridi.
 
Wewe ndio unakula sasa acha mimi nalalamika kisa 2,000 🀝🀝
 
Nilikuwaga na Chimbo langu Sumbawanga, Tulizoea kupaita Mboga Saba, yule sister alikuwa anapikia Nyumbani kwao. Kwa Tsh 3000/= tu unapata Ugali au Wali na Mboga na Kutosha. Kama ni ugali Nyama, basi utapewa na Maharage, Kisamvu, Na Dagaa. Nilipenda kulq pale milo yote Miwili. Maana ki geto geto kupika mboga zote hzo nisingeweza kutokana na ufinyu wa Muda
 
2013 kabla sijaanza kujipikia nilikuwa natumia kwa mwezi 30,000 nampa mama lishe hiyo hela nakula asubuhi mchana na jioni sasa hivi hii hela hata chai tu haitoshi kwa mwezi maisha yamebadilika sana kiasi kwamba pesa kwa sasa haina thamani tena.
 
Hayo maisha ya levo hiyo wanaishi majambazi maana hata masela hawaishi hivo
 
Na mwambie asidhani kupika mwenyewe ndio gharama zitapungua... Tena gharama inaweza kuwa juu zaidi..

Uzuri wa kupika mwenyewe ni ile kupata chakula chenye ladha nzuri na salama bila uchakachuzi... Ila gharama iko pale palee
Sio kweli bana ulikua hosteli nn? Uaan kupika na kununua vikae sawa we bado ulikua na hela
 
Sio kweli bana ulikua hosteli nn? Uaan kupika na kununua vikae sawa we bado ulikua na hela

Nipe gharama za kupika wali, kuanzia mchele na mazaga zagaa Yote... Halafu jiko ni umeme rice cooker au gesi. Plate moja na mboga yake utatumia gharama kiasi gani!?
 
Nimegundua hata watoa comment wanahela haha et geto kula 8000 kwa kupika siukajenge tu
 
Nipe gharama za kupika wali, kuanzia mchele na mazaga zagaa Yote... Halafu jiko ni umeme rice cooker au gesi. Plate moja na mboga yake utatumia gharama kiasi gani!?
Babu kwan mchele kg 5 ni bei gani? Na utatumia siku ngap haya kg 5 tuseme ni 10k kwa 2k 2k haya upo single kg 5 za 10k utakula mda gn? Nunua mafuta hata nusu lita, okay wenye friji sijui sisi machoko tunanunua vitunguu kwa jumla tunajaza unabaki unasaka hio 200 za nyanya per day maharage umenunua makavu yapo ndani kg zako za dagaa unga kg 5 1200 kg wakati huko kwa mama ntilie ugali 2000 una presha cooker yako yakuchemshia maji maharage gesi isiishe na vitu ka hizo na jiko la gesi, babu cost zitakua mwanzo tu ila huwezi compare na misosi ya kununua we unacheza labda kama unakula kg kwa siku hapo sawa
 
Nimegundua hata watoa comment wanahela haha et geto kula 8000 kwa kupika siukajenge tu
Ukifanya tu chai asubui 1000 mchana 2000 jioni 2000 kununua kwa mama ntilie kama unapika geto, hizo vitu umenunua unakula siku 3 hadi 4
 
Acha ushamba siku hizi kuna vifaa vingi vinarahisisha kupika mf pressure cooker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…