Unafanyaje ukijua bosi wako kazini ni mnafiki dhidi yako?

Unafanyaje ukijua bosi wako kazini ni mnafiki dhidi yako?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Mathalani fikiria hii situation umeajiriwa mahali ila boss wako machoni anacheka na wewe fresh kabisa na hakuonyeshi ubaya wowote ule ila under carpet anakusnichi. Fikiria mazingira yafuatayo.

1. Hakupendekezi kwenye Jambo lolote lenye maslahi na akikupendekeza anakupa vitu vidogovidogo sana visivyoendana na elimu uzoefu na seniority yako.

2. Ikitokea umepata barua flani yenye jambo lenye maslahi anaiblock juu kwa juu ili isikufikie tena anakoment vibaya juu yako ili waliokupenekeza wa terminate uamuzi wao.

3. Taarifa za wewe kusnichiwa unazipata kutoka kwenye verified source mathalani unapigiwa simu MBONA HUJAJA KWENYE SEMINA NA TUMEONA JINA LAKO? unabaki kutoa macho seminaaaa😯😯🤔🤔🤔

4. Ila anakuchekea vizuri Sana na kukiwa na Jambo lisilo na maslahi wewe ndio chaguo lake mfano kusuluhisha migogoro mahali pa kazi.

Hebu tupeane uzoefu kama ni wewe unafanyaje? Unaishi vipi na boss kama huyu?

Uzoefu hapa nawategemea walimu zaidi maana hawa ndio nawasikia mara nyingi wakilalamika kutokupewa kazi kama za marking na usimamizi wa mitihani isipokuwa wakuu huwa wanawatu wao spesho.
 
Ukistukia hzo we pia mchekee kinafiki hvo hvo na usjefanya Jambo lolote la kujitolea au ziada kumsaidia,tafuta mishe binafsi za kukuongezea kipato Ila ifanye kwa siri kubwa Sana ata workmates yeyote asiijue maana lazma bosi uyo atakua anakufatilia kisiri,afu pia ishi simple life, usionekane kushine sana until ahamishwepia usionekane unacare about hzo allowances za kiupendeleo maana ao mabosi (wengi historical wametoka kwny dhiki) hudhani ndo rungu la kukupigia lakin wakiona hubabaiki wanakuja directly bila na tabasamu feki tena, na ukipata mda wa ziada au unatengeneza visa vingi vya matatizo ya kifamilia ili ukawe karibu na mishe zako na ujiondoe na stress za bosi choko km uyo,

NB mabosi kama hao hupekua mafaili na kuangalia nakala za vyeti hususani birth certificates Kisha kuchukua majina yako kamili na ya mama yako mzazi Kisha hupeleka kwa masangoma wa kitabu kukujengea chemistry ya kukulipua so inatakiwa kuwa na imani thabiti na kuwa msiri na usietabirika kwenye mambo yako yote.
 
Wewe endelea kupiga kazi kwa bidii hasa, panga vzr na tumia muda wako unapokuwa off kufanya mambo yako kama biashara au ujasiliamali, wakati mwingne omba hata ED au ruhusa ya dharura kwaajili ya kufanya mambo yako. Mpumbavu hujibiwa kwa vitendo.
 
Nilishaona maelezo yamekaa kiualimu alimu hata kabla hujataja walimu huko chini.

Ebwana hii kitu ipo sana ila walimu huwa tunachanana makavu tu na ndiyo sababu ya maana na faida ya kuwa na vikao vya kila wiki shuleni.

Pia kuna baadhi wanasolve kivingine na wengine wanakaushia kabisa kama hakuna kinachoendelea vile.

Kwa mfano wengine wanafanya the best kwenye kazi zao mpaka yule boss anajishtukia, basi mwenyewe anaanza kujirudi. Kwa mfano hiyo ishu uliyosema hapo kusukumiwa kwenye kazi za moyo (kujitolea zaidi) basi unakuta jamaa anajitutumua balaa.

Wengine anajali yale ya lazima tu (yaliyomuweka hapo) na mengine yote anapuuzia hata ofa na mavitu zingine anakataa zinapomjia chances. Mbinu hii wanatumia wenye kujiwezaweza kuonesha kwamba hategemei promotions zao.

Wengine nao wanaact kinyume chake yaani mfano boss anamsnichi yeye ndo kwanza anamtetea inapotokea boss amebananishwa. Mfano ishu ya wageni (ugeni wa kikazi shuleni) huwa walimu wa aina hii (watengwa) ndo wanaookoaga sana jahazi.
 
Maboss kama hao huwa wanakua na vinyongo vya muda mrefu belive m kuna kitu ulifanya kiwe kizur au kibaya lakin yeye hakukifuraia so anakukomoa. Sisi wengine tunaishi na wafanyakaz wenzetu wanatusnitch kwa boss tunajua halaf wakija kwetu wanajichekesha chekesha halafu tunafanya kama hatujui wanazid kuumia maana wanagombana na mtu asiyegombana nao,wanahis kudharaulika.

Kwa ishu yako ningekushauri kufanya yafuatayo
-Usifanye kazi za ziada zisizo na malipo yaan kujitolea
-Kuwa serious muda wote ulio kazin
-Epuka story na wafanyakaz wenzako zinazozid dk 10 mfululizo
-Kuwa serious muda wote unapokua kazin
-Onesha standard zako wazwaz(fanya kaz kwa bidii bila kupitiliza mipaka)
-Boss usimnunie na wala usijipendekeze kwake
-Usifanye jambo lolote kuwavutia wafanyakaz wenzako au boss
-Jaza ratiba yako kwa mambo binafsi ili kuounguza muda wa kufikiria hizo ishu za semina semina,mf kuwa na muda na familia yako,marafiki wako tofauti na wa kazin,kujiunga na vikund vya mazoez,kufanya business zingine za kukuza kipato.

-Mwisho kabisa usilipe ubaya kwa ubaya,hiyo itakua tofauti yako na yeye
Usijisemee sana wapo watakaokusemea kutokana na kazi bora utakayoifanya zingatia sana kutokufanya kazi zaid ya nafac uliyonayo maana huko ni kujipendekeza,epuka. Sana makosa maana boss wako atakushtaki kwa hayo
 
Back
Top Bottom