Nilishaona maelezo yamekaa kiualimu alimu hata kabla hujataja walimu huko chini.
Ebwana hii kitu ipo sana ila walimu huwa tunachanana makavu tu na ndiyo sababu ya maana na faida ya kuwa na vikao vya kila wiki shuleni.
Pia kuna baadhi wanasolve kivingine na wengine wanakaushia kabisa kama hakuna kinachoendelea vile.
Kwa mfano wengine wanafanya the best kwenye kazi zao mpaka yule boss anajishtukia, basi mwenyewe anaanza kujirudi. Kwa mfano hiyo ishu uliyosema hapo kusukumiwa kwenye kazi za moyo (kujitolea zaidi) basi unakuta jamaa anajitutumua balaa.
Wengine anajali yale ya lazima tu (yaliyomuweka hapo) na mengine yote anapuuzia hata ofa na mavitu zingine anakataa zinapomjia chances. Mbinu hii wanatumia wenye kujiwezaweza kuonesha kwamba hategemei promotions zao.
Wengine nao wanaact kinyume chake yaani mfano boss anamsnichi yeye ndo kwanza anamtetea inapotokea boss amebananishwa. Mfano ishu ya wageni (ugeni wa kikazi shuleni) huwa walimu wa aina hii (watengwa) ndo wanaookoaga sana jahazi.