GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Mechi zote ambazo Klabu yangu 'pendwa' ya Simba SC imekuwea ikicheza hasa hizi zinazoitwa 'Mechi Mazoezi' tukishinda tu utaona katika Kurasa mbalimbali za Mitandao ya wana Simba SC na hata Klabu ya Simba huwa tunapewa 'Matokeo' haraka sana. Kwa mujibu wa Mtangazaji wa Clouds FM Shaffih Dauda jana mwishoni mwa Kipindi chao cha Michezo cha 'Sports Extra' alisema ( alihabarisha ) kuwa Simba SC ilicheza 'Mechi Mazoezi' na Timu ya Jeshi pale Mwenge Vinyago ya Green Warriors ambayo kiukweli huwa si tu inatusumbua lakini pia inatutesa kila tukikutana nayo na kama yetu Simba SC tulichezea 'Kichapo' kizuri tu kutoka Kwao.
Wana Simba SC Wenzangu hii 'dhana' kwamba Simba SC yetu haipaswi 'Kufungwa' tuiache na nimesikitika kuona taarifa hii haijaletwa Kwetu jana.
Wana Simba SC Wenzangu hii 'dhana' kwamba Simba SC yetu haipaswi 'Kufungwa' tuiache na nimesikitika kuona taarifa hii haijaletwa Kwetu jana.