Unafikiri ni kwanini hutakiwi kuanika maisha yako binafsi mtandaoni?

Unafikiri ni kwanini hutakiwi kuanika maisha yako binafsi mtandaoni?

Black Opal

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2023
Posts
233
Reaction score
298
Habari Wakuu,

oversharingg.jpg

Wengi tumekuwa tunapokea ama kutoa ushauri kwa watu kuacha kuanika maisha yao binafsi mtandaoni. Baadhi wanaelewa huku wengine ikionekana maneno yanaingia sikio moja na kutokea jingine.

Baadhi wamepata madhara kwa kuanika maisha yao mtandaoni huku wengine wakifaidika na hilo kwa kutembea na kiki.

Wewe unafikiri ni kwanini hutakiwi kuanika maisha yako binafsi mtandaoni? Kuna faida yoyote ya kufanya hivyo?
 
Maisha yanatakiwa yawe Siri kwà 90% na wazi kwà 10% . Kila mtu kaumbiwa vinasaba vyake humu duniani.

Si vyema kutoa siri ya vinasaba vyako. Ni vyema uishi kwà kutoeleweka na kwà kuwapa watu maswali mengi.

Maisha ni fumbo la imani na pia ni mfano wa Upendo.

What people don't understand, they call names,...And what they understand they destroy.

Watu wengi sana wameharibiwa , kuibiwa na hata kuuliwa kwasababu ya kuweka maisha yao wazi kwà 90% na huku wakificha siri zao kwà 10% .

Note: Ukianika siri zako , then unabecome a prey,......utaanza kuwindwa pasipo wewe kujua both physically & spiritually. Na ndio maana kama unapenda kufanya hivyo....jitahidi sana kuwa na Elimu ya kutosha pamoja na Maarifa ya kutosha.

Hofu ya Mungu itakupa Elimu ( Bodyguard)
Kumcha Mungu kutakupa Maarifa (Security Guard)

Kumbuka watu wengi huangamia kwà Kukosa Security Guard ( Maarifa )
 
Kwenye Maisha hakuna faida wala hasara. Itategemeana na mhusika.
Kama ulivyosema Jambo moja linaweza kuwa hasara Kwa MTU mmoja lakini likawa faida Kwa MTU mwingine.

Jambo kubwa kuliko NI kuishi Kwa Furaha. Kama Jambo halitaathiri furaha yako ya Leo na ya baadaye(Future) basi hilo unaruhusiwa kulifanya.

Ingawaje kwenye Ulimwengu wa Wasaliti, Watu wenye Chuki, na kutokuaminiana ni vizuri usitume mambo yako binafsi hasa ya Siri mitandaoni.
Kwa mfano Kutuma picha ukiwa na Mkeo au Mumeo Wakati huohuo Mumeo au Mkeo sio mwaminifu hiyo inaweza kukuletea fedheha na kudhalilika.

Au mambo ya uchumi, inaweza kuchukiwa au kuundiwe zengwe kama sio kulogwa au kuvamiwa na majambazi.

Lakini kama unajiamini na kama ni furaha yako kufanya hivyo. Unaweza kufanya
 
Habari Wakuu,

View attachment 2614072

Wengi tumekuwa tunapokea ama kutoa ushauri kwa watu kuacha kuanika maisha yao binafsi mtandaoni. Baadhi wanaelewa huku wengine ikionekana maneno yanaingia sikio moja na kutokea jingine.

Baadhi wamepata madhara kwa kuanika maisha yao mtandao huku wengine wakifaidika na hilo kwa kutembea na kiki.

Wewe unafikiri ni kwanini hutakiwi kuanika maisha yako binafsi mtandaoni? Kuna faida yoyote ya kufanya hivyo?
Mtoto wa kike ana sura na shape yake nzuri,

Anajipigapiga picha anaanika mtandaoni.

Muhuni wanachukua picha anaenda kupost huko kwamba anauza papa. Tena anatoa kubwa na ndogo.

Kidogo kidogo hizo post zinafika kwa mzazi wake au mume wake mtarajiwa.

Unadhani atajitetea ataeleweka?

Ni basi tu watu wanakaza mafuvu.
 
Mkianzisha uzi kutaka maoni ya wengine, wekeni yenu kwanza
Ni aina glani ya uoga na unafiki unaotusumbua watanzania na Africa kwa ujumla wake .
Mtu anataka apewe ushauri kwa kutumia matatizo ya watu wengine .
 
Ni aina glani ya uoga na unagiki unaotusumbua watanzania na Africa kwa ujumla wake .
Mtu anataka apewe ushauri kwa kutumia matatizo ya watu wengine .
Wengine huanza na mapito na mapitio yao ili wengine wajifunze, kisha wanauliza wengine maoni
 
Mtoto wa kike ana sura na shape yake nzuri,

Anajipigapiga picha anaanika mtandaoni.

Muhuni wanachukua picha anaenda kupost huko kwamba anauza papa. Tena anatoa kubwa na ndogo.

Kidogo kidogo hizo post zinafika kwa mzazi wake au mume wake mtarajiwa.

Unadhani atajitetea ataeleweka?

Ni basi tu watu wanakaza mafuvu.

Kuna Watu wapo sosho hivyo kupost kwao sio shida. Wapo ambao hawapost na wengi wao ndio picha zao zinavuja au kuvujishwa na watu wasio waaminifu.
 
Habari Wakuu,

View attachment 2614072

Wengi tumekuwa tunapokea ama kutoa ushauri kwa watu kuacha kuanika maisha yao binafsi mtandaoni. Baadhi wanaelewa huku wengine ikionekana maneno yanaingia sikio moja na kutokea jingine.

Baadhi wamepata madhara kwa kuanika maisha yao mtandao huku wengine wakifaidika na hilo kwa kutembea na kiki.

Wewe unafikiri ni kwanini hutakiwi kuanika maisha yako binafsi mtandaoni? Kuna faida yoyote ya kufanya hivyo?
Sioni faida au hasara ilio dhahiri, ila mimi binafsi utashi wangu nikuishi simple humble life, nisipate kujulikana sanaa na watu, ndio furaha yangu.
 
Aisee huo utoto wa kupost mambo mtandaoni tuwaachie mademu
Kwasababu hii ni dunia yao. Mbinguni ni kwà wanaume.

Note: Wanawake wanapenda sana wanaume wachaMungu, wakati wanaume wao Hupenda sana wanawake wenye hofu ya Mungu.

Reason is, Wanaume hutegemea sana kupata Elimu kutoka kwà Wanawake, wakati wanawake hutegemea kupata maarifa kutoka kwà wanaume.

Na ndio maana, palipo na Mafanikio ya Mwanaume ,..nyuma yake yupo Mwanamke mwenye hofu ya Mungu ( Bodyguard)

90% ya wanawake hawana hofu ya Mungu na wala hawapendi kwenda Mbinguni. Kwahiyo Mwanaume akijichanganya akakutana na Mwanamke wa hovyo....meaning hataweza kurudi Mbinguni ( huko juu ) bali atabaki mateka hapa duniani ( kwà Wanawake )
 
Ungeleta reference ya maoni yako au backup yoyote ingependeza sana kwasbb umeongelea vitu vyenye spiritual connection.
 
Inadepend mtu na ntu.
Kama wewe kweli ni Mwanaume,...fanya uwezavyo, ...urudi kwà Baba Yako wa kweli aliyeko mbinguni.

Huyo unayemuita Baba wa hapa duniani , sio Baba Yako wa kweli...ni Baba Yako wa Mchongo ambao umeaminishwa na hawa wanawake wa Ulimwengu huu kuwa ndiye Baba Yako....
40_Mat_23_09.jpg
 
Back
Top Bottom