Unafuatilia kipindi cha ‘Snakes in the City’?

LAPSE RATE

Senior Member
Joined
Oct 18, 2015
Posts
119
Reaction score
147
Kwa yeyote mwenye mapenzi na documentaries kuhusu maisha ya wanyama au watalam wa mambo ya wildlife mnisaidie kwenye hili. Kuna channel maarufu inyoitwa NatGeoWildAfrica HD iliyoko king'amuzi cha Azam channel namba 184 inarusha masuala mengi kuhusu wanyama.

Point yangu kubwa ni kuhusu huyu bwana aitwaye Simon Keys akiwa na Siouxsie Gillett anayekamata nyoka aina mbalimbali wenye sumu kali kama black mamba, king cobra, forest cobra, puff adder na wengine wengi wasiyo na sumu. Mara nyingi huonekana akiwa na wasaidizi wa kike mmoja mweusi na mwingine mzungu. Huenda mataifa mbalimbali kuwakamata nyoka kutoka kwenye makazi ya watu, majumbani, mashambani, kwenye visima vya maji na kwingineko.

Swali langu ni je huwa na ujuzi gani unaomfanya asidhurike na hao nyoka? Na hiyo huduma ya kuwatafta nyoka huwa analipwa au ni msaada. Na kwanini anawapata nyoka kirahisi hata kama wako ufichoni na nyoka humtii kirahisi? Anafaidikaje na kazi hii?

images (45).jpeg
images (1).webp
snakes-in-the-city-s8-team-1.jpg
MV5BMzAyZjg2MzYtYjgwNC00ZTRkLWI2YTctMDY3MzU2NWQzOTQ0XkEyXkFqcGc@._V1_.jpg
images.webp
 
Labda anawauza kwenye mazoo na research facilities, kunae watu wanafuga nyoka kama pets, content pia, ana utaalamu wa kuwasiliana na viumbe hao pia ndiomaana hawamleteagi kashkash. Wengine wanafanya kwakuwa anapenda tuu kufanya hivyo.
 
Haha imebidi kwanza nicheke, kabla ya kuanza kumsaka nyoka huwa wanahitaji maelezo kwa wakaazi wa alipoonekana nyoka ili kujua kwanza ni nyoka wa aina gani na wachukue hatua zipi za kukabiliana nae. Kama hawajapata maelezo ya kueleweka huwa wanachukua tahadhari zote kama za kuvaa miwani na groves mikononi na kuanza kumtafuta. Wakishamtambua ni aina gani ya nyoka huwa wanamuelezea kuanzia aina za sumu alizonazo na incase akakuwahi kukung'ata unapaswa kuchukua hatua gani.
Kiufupi hiyo huduma huwa hawaotoi bure bali hulipwa baada ya kufanikisha ukamataji. Hawajizungukii tu mitaani bali hupigiwa simu na hutoa price yao.
 
Kwa yeyote mwenye mapenzi na documentaries kuhusu maisha ya wanyama au watalam wa mambo ya wildlife mnisaidie kwenye hili. Kuna channel maarufu inyoitwa NatGeoWildAfrica HD iliyoko king'amuzi cha Azam channel namba 184 inarusha masuala mengi kuhusu wanyama.

Point yangu kubwa ni kuhusu huyu bwana aitwaye Simon Keys akiwa na Siouxsie Gillett anayekamata nyoka aina mbalimbali wenye sumu kali kama black mamba, king cobra, forest cobra, puff adder na wengine wengi wasiyo na sumu. Mara nyingi huonekana akiwa na wasaidizi wa kike mmoja mweusi na mwingine mzungu. Huenda mataifa mbalimbali kuwakamata nyoka kutoka kwenye makazi ya watu, majumbani, mashambani, kwenye visima vya maji na kwingineko.

Swali langu ni je huwa na ujuzi gani unaomfanya asidhurike na hao nyoka? Na hiyo huduma ya kuwatafta nyoka huwa analipwa au ni msaada. Na kwanini anawapata nyoka kirahisi hata kama wako ufichoni na nyoka humtii kirahisi? Anafaidikaje na kazi hii?
Hao jamaa wanafanya episode,1-8 walikua wanakamata Nyoka live South Africa hasa Durban,episode ya 9 walienda India wakishirikana na mkamata Nyoka maarufu wa kule,..........kumbuka south Africa na Mozambique's ndio nchi zinazoongoza kwa kua na Nyoka wengi Africa,...
Wale jamaa hulipwa Na hio channel ya Natgeowild lakini pia hulipwa pound kama 15 ambayo ni call out fee yao,hela ya mafuta,ila kwa watu masikini huenda bure tu
Wanachoma vaccine na dawa zingine za kujikinga na sumu ya Nyoka wanazo ili wasizulike
Nyoka wote wanaowakamata huwaachia waende maporini kwenye mazingira yao ya asili
 
Huyo jamaa ni wa muda sana, katafute historia yake alianza na mke wake wa kwanza wakaachana mpka akawa na uyo mzungu hapo..

Ko ni mzoefu anajua basics zote za kukamata nyoka, naamini alisomea hayo mambo.

Wanalipwa kwa episode inayorushwa kwenye kipindi.. na njia nyengine, kwa kifupi jamaa mzigo anao usimchukulie poa kabisa.
 
Hatari kubwa ya nyoka wa black mamba ni kama hutakuwa na antivenon yake karibu.
Hiyo jamaa anacheza na hao nyoka akiwa na antivenon sahihi kila muda
Nadhani kwa upande wa malipo hiyo ni moja ya contents kwenye programu za dstv atakuwa analipwa huko
 
Kuna wakati nilikuwa nafuatilia hiko kipindi huwa wanatoa kabisa tahadhari kwamba usije ukaiga wanachokifanya maana hiyo kazi inahitaji uzoefu kuliko inavyodhaniwa.

Kingine nyoka wengi hata wale tunaoona sisi hatari sana (black mamba cobra puff adder etc) hawamngʼati kwa sababu ya uzoefu wake akikutana nao mwili wake hauzalishi ile kemikali inayoashiria uadui kati binadamu na nyoka husika so mpaka nyoka aje kugundua jamaa hana nia mbaya (kumkamata) anakuwa tayari ameshamthibiti na vifaa vyake.
 
Asante sana kwa ufafanuzi mzuri. Nimeelewa kitu
 
Haha imebidi kwanza nicheke, kabla ya kuanza kumsaka nyoka huwa wanahitaji maelezo kwa wakaazi wa alipoonekana nyoka ili kujua kwanza ni nyoka wa aina gani na wachukue hatua zipi za kukabiliana nae. Kama hawajapata maelezo ya kueleweka huwa wanachukua tahadhari zote kama za kuvaa miwani na groves mikononi na kuanza kumtafuta. Wakishamtambua ni aina gani ya nyoka huwa wanamuelezea kuanzia aina za sumu alizonazo na incase akakuwahi kukung'ata unapaswa kuchukua hatua gani.
Kiufupi hiyo huduma huwa hawaotoi bure bali hulipwa baada ya kufanikisha ukamataji. Hawajizungukii tu mitaani bali hupigiwa simu na hutoa price yao.
Kumbe
 
Huyo jamaa ni wa muda sana, katafute historia yake alianza na mke wake wa kwanza wakaachana mpka akawa na uyo mzungu hapo..

Ko ni mzoefu anajua basics zote za kukamata nyoka, naamini alisomea hayo mambo.

Wanalipwa kwa episode inayorushwa kwenye kipindi.. na njia nyengine, kwa kifupi jamaa mzigo anao usimchukulie poa kabisa.
Kumbe pesa ipo siyo kujitolea
 
Hatari kubwa ya nyoka wa black mamba ni kama hutakuwa na antivenon yake karibu.
Hiyo jamaa anacheza na hao nyoka akiwa na antivenon sahihi kila muda
Nadhani kwa upande wa malipo hiyo ni moja ya contents kwenye programu za dstv atakuwa analipwa huko
Basi kumbe matendo yake ilibidi waandike kama mieleka kwamba "DON'T TRY THIS AT HOME"😀😀
 
Kuna wakati nilikuwa nafuatilia hiko kipindi huwa wanatoa kabisa tahadhari kwamba usije ukaiga wanachokifanya maana hiyo kazi inahitaji uzoefu kuliko inavyodhaniwa.

Kingine nyoka wengi hata wale tunaoona sisi hatari sana (black mamba cobra puff adder etc) hawamngʼati kwa sababu ya uzoefu wake akikutana nao mwili wake hauzalishi ile kemikali inayoashiria uadui kati binadamu na nyoka husika so mpaka nyoka aje kugundua jamaa hana nia mbaya (kumkamata) anakuwa tayari ameshamthibiti na vifaa vyake.
Dah, kumbe wako smart sana
 
Kuna kasumba za uongo mwingi sana kuhusu watu tunavyo amini kuhusu nyoka kutokana na vitabu vya kiimani na simulizi za kale

Kwa kawaida Nyoka ANAMUOGOPA zaidi binadamu kuliko sisi tunavyo muogopa.

Nyoka ni moja ya viumbe smart sana, akikutana na binadamu kabla huja muona atakacho kifanya kwanza ni kukukwepa na kujificha, atakugonga iwapo atahisi unataka kumshambulia…….na mara nyingi hutoa kwanza warning kulingana na aina ya nyoka
 
Bwana mdogo huko sikushauri ukafanye content wewe content za kupata pesa kirahisi fanya kama Harmonize mmakonde.

Huko Mzee wa manyoka amekuwepo kitambo sana na nimzoefu alafu anapassion na hiyo kazi hafanyii hela.

Hakuna cha bure huko mambo yamenyooka ukiwa na nyoka unapiga simu, mnakubaliana wankuja kukupa huduma ya kumuondoa nyoka katika mazingira yako.

Bongo hakuna nyoka wengi wala wenye sumu kali kama MSUMBIJI NA BONDENI KWA MADIBA.
 
😀😀😀 Kwamba ww ni mzee siyo
 
Back
Top Bottom