Unahisi biashara yako inasuasua? Huenda hii ndio sababu kuu kwa 99.9%

Unahisi biashara yako inasuasua? Huenda hii ndio sababu kuu kwa 99.9%

FestoKaguo

Senior Member
Joined
Apr 1, 2022
Posts
128
Reaction score
202
Ijumaa kareem wana JF
Leo nimekuandalia hii thread ambayo inaweza ikakusaidia wewe mtu unayetaka kuingia kwenye biashara ya aina yoyote ile iwe ni kilimo, ufugaji au hizi biashara za kwenye frame hapa panakufaa.

Kabla ya yote inatakiwa utambue ya kwamba kuna kitu kimoja ambacho biashara zote ambazo unaziona ni kubwa huwa zinakifanya kabla ya kuingiza bidhaa yao sokoni… Lakini ukija kwa wajasiriamali wengi wadogo wao huwa wanakosea kwa kukiruka hicho kitu au kukifanya kwa uvivu!

👉 WANAFANYA MARKET RESEARCH! 👈

Biashara nyingi unazoziona ni kubwa huwa zinatabia ya kukusanya data kutoka kwa watu na kuzichakata kisha baadae wanakuja na product yao iliyotokana na taarifa walizozikusanya kwenye jamii.

Sasa nije kwako wewe mjasiriamali mdogo nikuulize swali, Unajua kwanini bidhaa zako/yako inaweza kuwa nzuri lakini bado haifanyi vizuri sokoni? 🤔

Huenda labda sisi wateja hatuihitaji!

Au labda kuna washindani wanaotoa kitu bora zaidi!

Labda bei yako ni ya juu sana au ya chini sana hadi haileti faida!

Hapa ndipo suala la kufanya MARKET RESEARCH Iinapokuja kuokoa biashara yako!

20250404_223333.jpg

Pichani huyo ni mteja kutoka United Arab Emirates alinicheki akitaka kujua opportunity ya kuleta service yake ya training nchini Tanzania lengo kuu alitaka kujua utayari wa hayo makampuni upoje haswa.
Sasa kufanya market research juu ya kitu unachotaka kukifanya huwa ina umuhimu na faida kubwa sana hebu tuangalie kidogo faida ya market research;

FAIDA ZA MARKET RESEARCH
✅ Kwanza inakusaidia kujua wateja wako wanataka nini HASWA (sio unachodhani wanataka!)
✅ Pia unagundua nafasi mpya sokoni kabla ya washindani wako kukuwahi
✅ Kingine unajifunza udhaifu wa washindani wako na kuutumia kujikuza zaidi kwenye biashara yako.
✅ Na ya mwisho kabisa unapunguza uwezekano wa kupata hasara kubwa

UNAWEZAJE KUFANYA MARKET RESEARCH HATA KAMA HUNA BAJETI?
Kitu cha kwanza kabisa ni unapaswa kuongea na wateja wako wa sasa kwa kuwauliza maswali au kuwapa dodoso wakusaidie kujaza maoni yao ujue wana kipi cha kuongeza au kukushauri.
Screenshot_20250404_230755_X.jpg

Kwa mfano hao ni huru pay ni taasisi inayojihusisha na kusaidia watu kupokea pesa kutoka nje ya nchi kwa njia yoyote kama cryptocurrency au kukusaidia kumiliki akaunti ya nchini marekani hapo wakawa wanahitaji maoni ya watumiaji wao juu ya huduma wanayoitoa nini waboreshe n.k

Pili unaweza kuangalia washindani wako wanafanya nini kwenye mitandao ya kijamii i.e je wamelist huduma zao kwenye social media au google map
Screenshot_20250404_231045_Maps.jpg

pichani ni google map nimesearch hotel zilizopo karibu na mimi zikaja kwahiyo kama unatoa huduma na haupo mtandaoni inamaana hii inakuwa ni moja ya challenge kwako kama ukihitaji hii huduma unaweza kunitafuta nikusaidie kuweka biashara yako google

Pia unaweza ukafanya polls au dodoso rahisi kwenye WhatsApp au Telegram groups and channels. Au unaweza ukatembelea magroup ya biashara uone watu wengi wanazungumzia nini kuhusu biashara za wengine au ya kwako ambayo inafanywa na mtu mwingine

STOP kufanya biashara kwa kubahatisha!
Chukua hatua sasa! Kabla hujawekeza mtaji wako wote kwenye biashara, hakikisha unafanya utafiti wa soko kwanza.

➡Mwisho wa siku nikuombe umtag rafiki yako ambaye ana biashara au anapanga kuanza biashara!

➡ SHARE hii post kwa wajasiriamali wengine ili waepuke makosa haya!
➡ Nitumie neno "Market Research" kwa namba 0765772976 nitakutumia mbinu za ziada za bure! kwenye whatsapp yako

Ahsante kwa kusoma natumai haujaondoka bure!!!
 
Back
Top Bottom