Unahisi nani alinywea hapa?

Unahisi nani alinywea hapa?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Hapa ni wanaume wa shoka wakipigana mkwara, enzi soka lilikuwa na wababe. Unahisi hapa nani alinywea na nani alishinda?
ad34411826b5240c0789e44434bb32da.jpeg
 
Hapana chezea gattuso tetesi zinasema Ronaldo anajiandaa kuandika kitabu kuhusu huyu gattuso[emoji3][emoji3]
Usiku mmoja wa Ulaya ndani ya uwanja wa San siro jijini Milan nchini Italy, mashabiki wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange wa marudiano kati ya Ac Milan Vs Man Utd katika Uefa Champions League.

Man Utd ikiwategemea hasa Ronaldo Na Rooney ili kuiangamiza Milan, ghafla anaibuka muitaliano mmoja na kuiteka show nzima kibabe. Si mwingine ni Genaro Rino Gattuso. Anamuweka Ronaldo mfukoni muda mwingi wa mchezo katika ile style ya Man Marking (Man to Man).

Mechi inaisha Ac Milan wanasonga mbele lakini gumzo kubwa ni wapi alipokuwa Ronaldo kwa dakika 90 za mchezo ule. Ronaldo alipotea na hakika alipaswa kufunguliwa kesi ya UZURURAJI.

Gattuso anamaliza mechi ile huku akivua bukta yake na kuanza kushangilia kwa mbwembwe zote.
 
Gennarro Gattuso, Patrick vieira, Claude Makelele, Roy keane, Michael Ballack, Michael Essien..Watu wa aina hii kwenye Soka wanapotea kwa kasi sana. Soka limekuwa rahisi mno.
Pia usiwasahau akina Nemanja Vidic, Lee Bowyer, Effenberg, Kohler, Chrstian Ziege, Denis Wise na wengineo wengi wa kariba hyo
 
Usiku mmoja wa Ulaya ndani ya uwanja wa San siro jijini Milan nchini Italy, mashabiki wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange wa marudiano kati ya Ac Milan Vs Man Utd katika Uefa Champions League.

Man Utd ikiwategemea hasa Ronaldo Na Rooney ili kuiangamiza Milan, ghafla anaibuka muitaliano mmoja na kuiteka show nzima kibabe. Si mwingine ni Genaro Rino Gattuso. Anamuweka Ronaldo mfukoni muda mwingi wa mchezo katika ile style ya Man Marking (Man to Man).

Mechi inaisha Ac Milan wanasonga mbele lakini gumzo kubwa ni wapi alipokuwa Ronaldo kwa dakika 90 za mchezo ule. Ronaldo alipotea na hakika alipaswa kufunguliwa kesi ya UZURURAJI.

Gattuso anamaliza mechi ile huku akivua bukta yake na kuanza kushangilia kwa mbwembwe zote.

Umenikumbusha WC ya 2006 walipotwaa Ubingwa kule Ujerumani, alivua bukta pia....

Gattuso alikuwa ni beki mtata sana.
 
Back
Top Bottom