Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,558
- 64,966
Sasa hivi, migogoro ya kifamilia, kimahusiano, kufumaniana tunafanya kwa mitandao ya kijamii.
Msuluhishi wetu mkuu ni mitandao ya kijamii; iwe JF, YouTube, Tiktok na mingineyo.
Wakati zamani, migogoro tulikuwa tunaipeleka kwa wazee, wazazi, wazee wa mila au ukoo tukiamini wao ndio wasuluhishi bora.
Lakini nyakati hizi mambo yamebadilika, hatuoni umuhimu wa hawa wazee tena, na kukimbilia mitandaoni kwa ajili ya usuluhishi.
Unahisi ni nini kilichofanya haya mabadiliko?
Au ndio kama ule msemo usemao, ata wahuni nao huzeeka, ikitafsiri; wazee wa sasa ni vijana wa zamani waliokuwa na aina fulani ya maisha yasiyokuwa na afya kwa jamii.