SoC01 Unahitaji kuanzisha biashara? Chukua fursa hii

SoC01 Unahitaji kuanzisha biashara? Chukua fursa hii

Stories of Change - 2021 Competition

Nawatania

Senior Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
148
Reaction score
549
Fursa maana yake ulione tatizo na utafute njia za kulitatua huku ukitengeneza pesa.

Ndio maana watu wengi ushindwa kuziona fursa maana hawapendi kutatua matatizo.

Daktari anatibu mgonjwa na anapata pesa
Mwalimu anapelekewa mwanafunzi hasiyejua kusoma wala kuandika anamtengeneza yeye kuwa Dactari, Mwalimu wake na mwalimu au injinia.

Niende kwenye mada; Tanzania ni kama nchi zingine ambazo zinaendea hivyo Tanzania ina fursa nyingi sana kama ambavyo nchi zote zinazoendelea zilivyojaa fursa.

Kwa kutumia technojia ya habari na mawasiliano kuna fursa kubwa naenda kukupa hapa chini.

Unaanzaje? Zunguka mitaa yote ya Tanzania hasa mijini utakutana na matangazo ya karatasi mtaani huyu anatangaza Shule, huyu anatangaza Chuo, huyu anatangaza ajira, huyu anatangaza tenda, wengine wanajitangaza nyakati za uchaguzi lakini zile Karatasi uwa zinaacha uchafuzi mkubwa wa mazingira hasa kuta mbalimbali za majengo maeneo mbali mbali mijini.

Hii ni fursa kwa sababu zifuatazo

1: Hakuna serikali yeyote duniani inayopenda mazingira yake yachafuliwe

2: Serikali itailinda biashara yako kwa sababu itapanua wigo wa ukusanyaji kodi

3: Makampuni wanatumia gharama kubwa sana kutangaza maana wanachapisha wenyewe matangazo, Wanayasambaza wenyewe na wanayalinda wenyewe yasibanduliwe yalipowekwa utawashawishi kwa kuwafanyia kila kitu.

4: Watu wengi utapeliwa pesa na baadhi ya makampuni hewa ambayo utangaza fursa hewa kwa sababu hakuna monitoring kwa makampuni husika.

Hizi hoja tatu zitakufanya upate pesa wewe kwa kutumia fursa hii ipasavyo.

Jinsi ya kuanza: Kasajili kampuni BRELA ambayo inajihusisha na mambo ya tekinolojia ya mawasiano, Pata Till namba na Reseni ya biashara anza kazi hivi.

Zitumie halimashauri za miji na majiji na uhakikishe unapata eneo la kujenga note board ambayo nitaonyesha picha yake hapo chini, Notes board zako ziwekewe taa ( electrical instillation) yaani wakati wa usiku iwake na waambie halimashauri ya kampuni yako itakapoanzia kwamba unahitaji tenda za matangazo yao uwe unawatangazia bure kwenye notes board zako watakupa

Fanya lobbying katika halimashauri hiyo wapige marufuku matangazo kubandikwa ovyo ovyo kwa kuwaelezea hasara zake kama nilivyozitaja hapo juu likiwepo swala la kodi waambie wewe utalipa kodi na VAT.

Hakuna halimashauri itagoma kukupa hii fursa hapo utatengeneza team kwenda maofisi yote na kuomba matangazo na kuacha mawasiliano ya kampuni yako.

Utatoa ajira kwa vijana maana kila kitu kitafanywa na kampuni yako kama Kudezaini, Kusimamia matangazo yenye kutaka kutapeli watu hii itakufanya kuwa karibu sana na Makampuni mengi na Serikali.

Pia hakikisha unakuwa na notes board za kutosha mjini pia uwe mbunifu mfano notes board chini yake unaweza kuweka kituo cha kuuzia magazeti kwenye kila notes board yako na kuwapa bule vijana watumie kuuzia huku wakilinda notes board ya kampuni yako na hii itakusaidia kwenye masoko maana watu wengi usimama kwenye vituo vya magazeti hivyo itakufanya upate wateja wengi wanafika kwenye notes board za kampuni yako na wakati huo kuwashawishi wateja watangaze na wewe.

Utaweka bei ya kawaida ya kuanzia kwa kigezo cha mtu au kampuni inataka kutangaziwa wapi? Kama ni note board moja labda ya posta utajua bei yako iweje kuna mwingine atakwambia anataka kutangaza notes board zote za Dar yaani (promotion announcement) utaweka utaratibu.

Nakaribisha maswali kwa fursa hii labda kama kuna jambo nimesahau kuliandika niulize nitakujibu

Kesho nitakuja na fursa nyingine
images (21).jpg
images (22).jpg
 
Upvote 31
Nimekuuliza swali kwanini kama ni risk why !!

1: makampuni bado wanatangaza matangazo mtaani ?nijibu

2: kwanini posta mpaka Leo ipo haijafa? Nijibu

3: Kwanini magazeti yapo hayajafa ambayo ni serious? nijibu

4: kwanini ukiweka tangazo mtandaoni ukiwa na follows mfano 100,000 watacoment 10 na like 200? Lakini mtu huyo huyo akiweka picha yake ya utupu atapata comment 10000 na like 80,000 why?

Fanya reseach Nijibu.
Do your home work properly acha ubishi dogo
 
1,hakuna kampuni ya maana inayotangaza mtaani
2.posta ya enzi za ujima ilikuwa active kukiko sasa kama hujui
3.mauzo ya magazeti yamepungua sana tena sana kulinganisha na miaka kumi nyuma
Ujaelewa kumbe lengo la biashara yenyewe

Iko hivi ngoja nikueleweshe kidogo
Lengo ni kukuza biashara ndogo ndogo na watu wawe well informed na kinachoendelea katika maeneo yao

Ndio maana nimekwambia hivi hakuna shule itakayokataa kutangaza na wewe je tuna shule ngapi dar?

Hakuna chuo kitakataa kutangaza na wewe je tuna vyuo vingapi Dar?

Hakuna tamasha lolote litakalokuwa linataka kufanyika mjini ukafuata biashara likakunyima

Vile vile kama unaanzisha kampuni ujashindwa hiyo kampuni kuifungulia website( blog) ili matangazo yote yaliyopo kwenye notes board yawepo tena kwenye blog ya kampuni yako.

Ndio maana nikamwambia shida sio kampuni shida ni ushawishi wa hiyo kampuni kufanya masoko hapo ndio wengi tunafeli.

Je una watu watakao kuwa tayari kufanya kazi?

Hakuna biashara ambayo haipo na hailipi Mimi nakataa.

Ulaya uko ambako technology ilianzia hizi notes board bado zinafanya kazi tena sana tu!

Nafikiri nimekujibu
 
Ujaelewa kumbe lengo la biashara yenyewe

Iko hivi ngoja nikueleweshe kidogo
Lengo ni kukuza biashara ndogo ndogo na watu wawe well informed na kinachoendelea katika maeneo yao

Ndio maana nimekwambia hivi hakuna shule itakayokataa kutangaza na wewe je tuna shule ngapi dar?

Hakuna chuo kitakataa kutangaza na wewe je tuna vyuo vingapi Dar?

Hakuna tamasha lolote litakalokuwa linataka kufanyika mjini ukafuata biashara likakunyima

Vile vile kama unaanzisha kampuni ujashindwa hiyo kampuni kuifungulia website( blog) ili matangazo yote yaliyopo kwenye notes board yawepo tena kwenye blog ya kampuni yako.

Ndio maana nikamwambia shida sio kampuni shida ni udhawishi wa huyo kampuni kufanya masoko hapo ndio wengi tunafeli.

Hakuna biashara ambayo haipo Mimi nakataa ulaya uko ambako technology ilianzia hizi notes board bado zinafanya kazi tena sana tu!

Nafikiri nimekujibu
Culture ya wazungu na waafrika tofauti sana,wazungu mpaka leo wanasoma sana magazeti,watanzania wana allergy na maandish ya kwenye makaratasi,simu na Tv ndio tumebase huko,hata housegirl hataki simu ya kitochi ika graduate anamaliza mwaka hajanunua gazeti
 
Watu wanadanya Digital Marketing and Advertisement wewe unataka kuturudisha nyuma miaka 70 dunia ilikotoka.

Mkuu tuko kwenye technology era achana na hayo Mambo unapoteza muda.

Halafu inaonekana hujui tenda za serikali kwasasa zinatolewaje.

Tenda zinatangazwa na PPRA chini ya mfumo wa TanePs huko halmshaur unaenda kupoteza muda tu.
 
Kama matangazo yangekuwa hakuna basi tusineona matangazo yanayozakaa mtaani ya kila aina

Madalali, mashule, vyuo, kazi kibao wakina Azzam wanatangaza hayo yote ni matangazo je chukulia mfano halimashauri ikioiga marufuku yatatangazwa wapi? Hii ni fursa ndugu.

Hapa cha kufanya ni kuwa na marketing term iliyo serious na wanaoweza kuwa smart kushawishi makampuni kutangaza nao.

Tanzania tunakwama sehemu moja tu kwenye marketing tukiweza huko tutakuwa na biashara nyingi na maana fursa ni nyingi sana.
Umejaa theories kijana Mambo hayako hivyo.

Nenda kaulizie gharama za Matangazo kwenye hizo boards ndio utaelewa TANZANIA Ina laana.

Siku hizi huoni hata Lori za Azam wamebandua stickers nenda kaulize sababu ?

Zile Daladala ambazo zilikuwa zimebandikwa matangazo huoni zimepungua !!! Nenda kaulize sababu halafu uje kufuta Uzi wako
 
Nimekuuliza swali kwanini kama ni risk why !!

1: makampuni bado wanatangaza matangazo mtaani ?nijibu

2: kwanini posta mpaka Leo ipo haijafa? Nijibu

3: Kwanini magazeti yapo hayajafa ambayo ni serious? nijibu

4: kwanini ukiweka tangazo mtandaoni ukiwa na follows mfano 100,000 watacoment 10 na like 200? Lakini mtu huyo huyo akiweka picha yake ya utupu atapata comment 10000 na like 80,000 why?

Fanya reseach Nijibu.
We bado mdogo Sana mwenye hayo Mambo ,

Comments au likes chache sio sababu kuwa tangazo halijawafikia watu. Kuna Kitu kinaitwa Engagement kwenye Social media advertisement anaweza asicommemt hata mtu mmoja ila Engagement Ina watu 13,000

Nasikitika kusema huna unalojua
 
Watu wanadanya Digital Marketing and Advertisement wewe unataka kuturudisha nyuma miaka 70 dunia ilikotoka.

Mkuu tuko kwenye technology era achana na hayo Mambo unapoteza muda.

Halafu inaonekana hujui tenda za serikali kwasasa zinatolewaje.

Tenda zinatangazwa na PPRA chini ya mfumo wa TanePs huko halmshaur unaenda kupoteza muda tu.
Sijasema uombe tenda Mimi pls
 
We bado mdogo Sana mwenye hayo Mambo ,

Comments au likes chache sio sababu kuwa tangazo halijawafikia watu. Kuna Kitu kinaitwa Engagement kwenye Social media advertisement anaweza asicommemt hata mtu mmoja ila Engagement Ina watu 13,000

Nasikitika kusema huna unalojua
Ndio tunarudi pale pale sasa mtu kutonunua gazeti sio kwamba hataki gazeti ila ni vile inawezekana hana pesa mfukoni ya kulinunua

Jiulize kwanini mtu akiona mwenzie ana gazeti na yeye anaomba apitie? Nijibu
 
Jina lako linakusadifu
 
Umejaa theories kijana Mambo hayako hivyo.

Nenda kaulizie gharama za Matangazo kwenye hizo boards ndio utaelewa TANZANIA Ina laana.

Siku hizi huoni hata Lori za Azam wamebandua stickers nenda kaulize sababu ?

Zile Daladala ambazo zilikuwa zimebandikwa matangazo huoni zimepungua !!! Nenda kaulize sababu halafu uje kufuta Uzi wako
Mkuu biashara yeyote ni masoko kama hauna kitengo cha masoko hauwezi kufanya.

Ulishawai kujiuliza kwanini media kama TBC1 ambayo inaonekana bure kwenye kila king'amuzi inashindwa kupata matangazo na wasafi TV ambayo imekuja juzi na inalipiwa kwenye kinga'amuzi ina matangazo?

Jibu linakuja tatizo ni content na kitengo cha masoko
Hakuna biashara duniani ambayo aifanyiki nakwambia issue ni vipi unaifanya?

Hapa unafungua kampuni unaanza operation.

Unafungua website yake matangazo yote yaliyo kwenye notes board vile vile yana appear kwenye website.

Unafungua account kwenye social media zote zinasaport biashara

Utakosaje biashara? Tatizo sio kufanya tatizo unafanya kwa namna gani?
 
We bado mdogo Sana mwenye hayo Mambo ,

Comments au likes chache sio sababu kuwa tangazo halijawafikia watu. Kuna Kitu kinaitwa Engagement kwenye Social media advertisement anaweza asicommemt hata mtu mmoja ila Engagement Ina watu 13,000

Nasikitika kusema huna unalojua
Dogo hajielewi achana nae
 
Mkuu biashara yeyote ni masoko kama hauna kitengo cha masoko hauwezi kufanya.

Ulishawai kujiuliza kwanini media kama TBC1 ambayo inaonekana bure kwenye kila king'amuzi inashindwa kupata matangazo na wasafi TV ambayo imekuja juzi na inalipiwa kwenye kinga'amuzi ina matangazo?

Jibu linakuja tatizo ni content na kitengo cha masoko
Hakuna biashara duniani ambayo aifanyiki nakwambia issue ni vipi unaifanya?

Hapa unafungua kampuni unaanza operation.

Unafungua website yake matangazo yote yaliyo kwenye notes board vile vile yana appear kwenye website.

Unafungua account kwenye social media zote zinasaport biashara

Utakosaje biashara? Tatizo sio kufanya tatizo unafanya kwa namna gani?
Kwanini watu wapeleke matangazo Wasafi na wasipeleke matangazo kwenye mabango ya Barabarani?

Ndio maana tunakwambia matangazo Sasa hivi ni Kidigitali na sio hizo takataka zako za Kuchafua miji
 
Kwanini watu wapeleke matangazo Wasafi na wasipeleke matangazo kwenye mabango ya Barabarani?

Ndio maana tunakwambia matangazo Sasa hivi ni Kidigitali na sio hizo takataka zako za Kuchafua miji
Kila mtu atachagua pa kupeleka sio kila mtu ana uwezo wa kupeleka kwenye radio na tv

Wa radio atapeleka

Wa TV atapeleka

Wa barabarani apeleke

Wewe peleka uko kwenye Radio na watakaopeleka kwenye mbao za matangazo wapeleke kwanini unalazimisha kila mtu atangaze wewe unavyotaka?

Mazingira yalivyo sasahivi kwa hayo matangazo kuchafua je kuna tatizo gani yakitengenezewa utaratibu wa sehemu ya kuwekwa kama alivyosema mleta mada?

Hebu tuwe tunajitahidi kuangalia mambo in positive way kuliko kuangalia mambo in negative way kila siku.
 
Dogo hajielewi achana nae
Hoja yake ipo wazi kabisa kakwambia unataka digital makerting wewe Fanya kwanini unataka kuzuia wengine wasifanye kivingine?

Why una negative mentality hivyo? Kasema wazi hapo juu kuwa na notes board hakuzuii wewe kuwa na website, kuwa na accounts kwenye social media zote hata kuwa na channel YouTube kwa kutumia jina ilo ilo la kampuni .

Hapo shida ya mtoa hoja iko wapi? Mimi binafsi nimeelewa wewe ndiye ujielewi.
 
Hiyo mode yake ilishapitwa na wakati .atakula hasara aje kulia lia humu.simkatishi tamaa namwelekeza kujifunza hakuna mwisho.notice board karne hii😇
 
Kila mtu atachagua pa kupeleka sio kila mtu ana uwezo wa kupeleka kwenye radio na tv

Wa radio atapeleka

Wa TV atapeleka

Wa barabarani apeleke

Wewe peleka uko kwenye Radio na watakaopeleka kwenye mbao za matangazo wapeleke kwanini unalazimisha kila mtu atangaze wewe unavyotaka?

Mazingira yalivyo sasahivi kwa hayo matangazo kuchafua je kuna tatizo gani yakitengenezewa utaratibu wa sehemu ya kuwekwa kama alivyosema mleta mada?

Hebu tuwe tunajitahidi kuangalia mambo in positive way kuliko kuangalia mambo in negative way kila siku.
Kuna sehemu nimekataza mtu asipeleke matangazo kwenye mbao ?

Nilichofanya Ni kufanya analysis. Watu wanapeleka matangazo kwenye account za Watu huko Facebook au Instagram utapambana vipi kuleta upinzani uwashawi walete matangazo kwenye mbao zako.
 
Hiyo mode yake ilishapitwa na wakati .atakula hasara aje kulia lia humu.simkatishi tamaa namwelekeza kujifunza hakuna mwisho.notice board karne hii[emoji56]
Sasa wewe kuna biashara haifi? Au kuna biashara nyepesi? afanye kwanza ndio alete mrejesho kwamba kafirisika ndio ajifunze.

M- pese, Tigo pesa ndio biashara za kisasa lakini biashara kibao tu zinakufa na watu wanakimbia

Hakuna biashara nyepesi na hakuna biashara ngumu!

Business is all about taking risk!
 
Back
Top Bottom