SoC01 Unahitaji kuanzisha biashara? Chukua fursa hii

Stories of Change - 2021 Competition

Nawatania

Senior Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
148
Reaction score
549
Fursa maana yake ulione tatizo na utafute njia za kulitatua huku ukitengeneza pesa.

Ndio maana watu wengi ushindwa kuziona fursa maana hawapendi kutatua matatizo.

Daktari anatibu mgonjwa na anapata pesa
Mwalimu anapelekewa mwanafunzi hasiyejua kusoma wala kuandika anamtengeneza yeye kuwa Dactari, Mwalimu wake na mwalimu au injinia.

Niende kwenye mada; Tanzania ni kama nchi zingine ambazo zinaendea hivyo Tanzania ina fursa nyingi sana kama ambavyo nchi zote zinazoendelea zilivyojaa fursa.

Kwa kutumia technojia ya habari na mawasiliano kuna fursa kubwa naenda kukupa hapa chini.

Unaanzaje? Zunguka mitaa yote ya Tanzania hasa mijini utakutana na matangazo ya karatasi mtaani huyu anatangaza Shule, huyu anatangaza Chuo, huyu anatangaza ajira, huyu anatangaza tenda, wengine wanajitangaza nyakati za uchaguzi lakini zile Karatasi uwa zinaacha uchafuzi mkubwa wa mazingira hasa kuta mbalimbali za majengo maeneo mbali mbali mijini.

Hii ni fursa kwa sababu zifuatazo

1: Hakuna serikali yeyote duniani inayopenda mazingira yake yachafuliwe

2: Serikali itailinda biashara yako kwa sababu itapanua wigo wa ukusanyaji kodi

3: Makampuni wanatumia gharama kubwa sana kutangaza maana wanachapisha wenyewe matangazo, Wanayasambaza wenyewe na wanayalinda wenyewe yasibanduliwe yalipowekwa utawashawishi kwa kuwafanyia kila kitu.

4: Watu wengi utapeliwa pesa na baadhi ya makampuni hewa ambayo utangaza fursa hewa kwa sababu hakuna monitoring kwa makampuni husika.

Hizi hoja tatu zitakufanya upate pesa wewe kwa kutumia fursa hii ipasavyo.

Jinsi ya kuanza: Kasajili kampuni BRELA ambayo inajihusisha na mambo ya tekinolojia ya mawasiano, Pata Till namba na Reseni ya biashara anza kazi hivi.

Zitumie halimashauri za miji na majiji na uhakikishe unapata eneo la kujenga note board ambayo nitaonyesha picha yake hapo chini, Notes board zako ziwekewe taa ( electrical instillation) yaani wakati wa usiku iwake na waambie halimashauri ya kampuni yako itakapoanzia kwamba unahitaji tenda za matangazo yao uwe unawatangazia bure kwenye notes board zako watakupa

Fanya lobbying katika halimashauri hiyo wapige marufuku matangazo kubandikwa ovyo ovyo kwa kuwaelezea hasara zake kama nilivyozitaja hapo juu likiwepo swala la kodi waambie wewe utalipa kodi na VAT.

Hakuna halimashauri itagoma kukupa hii fursa hapo utatengeneza team kwenda maofisi yote na kuomba matangazo na kuacha mawasiliano ya kampuni yako.

Utatoa ajira kwa vijana maana kila kitu kitafanywa na kampuni yako kama Kudezaini, Kusimamia matangazo yenye kutaka kutapeli watu hii itakufanya kuwa karibu sana na Makampuni mengi na Serikali.

Pia hakikisha unakuwa na notes board za kutosha mjini pia uwe mbunifu mfano notes board chini yake unaweza kuweka kituo cha kuuzia magazeti kwenye kila notes board yako na kuwapa bule vijana watumie kuuzia huku wakilinda notes board ya kampuni yako na hii itakusaidia kwenye masoko maana watu wengi usimama kwenye vituo vya magazeti hivyo itakufanya upate wateja wengi wanafika kwenye notes board za kampuni yako na wakati huo kuwashawishi wateja watangaze na wewe.

Utaweka bei ya kawaida ya kuanzia kwa kigezo cha mtu au kampuni inataka kutangaziwa wapi? Kama ni note board moja labda ya posta utajua bei yako iweje kuna mwingine atakwambia anataka kutangaza notes board zote za Dar yaani (promotion announcement) utaweka utaratibu.

Nakaribisha maswali kwa fursa hii labda kama kuna jambo nimesahau kuliandika niulize nitakujibu

Kesho nitakuja na fursa nyingine
images (21).jpg
images (22).jpg
 
Upvote 31
Yuko old stone age eti notice board,hata shule siku hizi matokeo no online
Mkuu acha kupotoka na kupotosha..., kuna kitu kinaitwa niche market, pia kuna market segmentation na target marketing...

Hivi unadhani kwa mama anayepika maandazi kitaa au anayepangisha kachumba au tuseme mtu ambaye wateja wake wanatokea mtaani pekee ukimpa choice aweke tangazo lake kwenye mti wa kijiwe cha gahawa mataani / au dukani kwa mangi na kutangaza facebook au kwenye CNN America wapi patakuwa na impact kwa biashara yake?

Unadhani traffic ya watu wa mtaani dukani kwa mangi itazidiwa na watu wanaoingia instagram kuangalia issue nyingine ambapo kwao matangazo ni kero (tena wanatafuta adblocker kabisa)....

Au jamii ya kitaa ambao smartphone kwao hata kutumia hawawezi unadhani itakuwa bora uwatangazie kigodoro kitakuwepo saa ngapi kwenye facebook au sehemu wanapojumuika mtaani ?
 
Mama lishe aweke tangazo kwenye notice board?anamlenga nani?
 
Walaji wake mtaani; au wajenzi wanaokuja kujenga nyumba pale mtaani ambao ni wageni wakifuata sigara dukani kuna namba zake pale "Kwa Chai Makande, Vitumbua na Miguu ya Kuku nipigie Au Order za Kesho muachie Mangi" Au Nimehama kijiwe nimetoka mtaa wa tatu kwa Zuberi sasa Nipo Barabara ya Saba mkabala na Shimo la Taka"

Au Mtori umerudi Wateja wangu Karibuni tena Nimeshatoka Rombo....
 
Tangazo la hivyo halihitaji notice board unabandika tu ukutani au kwenye nguzo ya umeme kama yale ya waganga wa kienyeji au vyuo vya mitaani,naomba ustick kwenye notice board
 
Moja Mdau kasema badala ya watu kuchafua mistimu pawe na specified location....

Pili nadhani hakuna sehemu yenye traffic mtaani kama dukani au kijiweni (hivyo jamaa akiongea na mangi akaweka bango lake pale watu watasoma na huenda wakakubali kutoa chochote)

Sisemi kwamba atapata pesa (biashara ya matangazo sasa hivi ni ngumu hata online inabidi uwe na akili usiuze matangazo bali utoe content zenye matangazo kwa siri); Point yangu ni kwamba kuna watu ambao ukitaka kuwatarget notice board ina impact kuliko other medium of communication (though not sure they will be willing to pay a lot) ingawa unaweza kuingia nao mkataba kama ni chumba au gari badala ya kulipia tangazo ukapata commission...
 
Kama umekiri kuwa biashara ya matangazo nowadays ni ngumu nashukuru atleast unaonekana unajua unachoongea,na ni ngumu kweli
 
Moja Mdau kasema badala ya watu kuchafua mistimu pawe na specified location....

Pili nadhani hakuna sehemu yenye traffic mtaani kama dukani au kijiweni (hivyo jamaa akiongea na mangi akaweka bango lake pale watu watasoma na huenda wakakubali kutoa chochote)

Sisemi kwamba atapata pesa (biashara ya matangazo sasa hivi ni ngumu hata online inabidi uwe na akili usiuze matangazo bali utoe content zenye matangazo kwa siri); Point yangu ni kwamba kuna watu ambao ukitaka kuwatarget notice board ina impact kuliko other medium of communication (though not sure they will be willing to pay a lot) ingawa unaweza kuingia nao mkataba kama ni chumba au gari badala ya kulipia tangazo ukapata commission...
Well asante kwa kunijibia
 
Idea nzuri, ungeifanya a separate thread ili watu wengi waione; imeruhusiwa pia kuwa na threads nyingi ila itakayoshinda ni moja!
Niende moja kwa moja kwenye mada nimesema kila siku nitatoa wazo angalau moja la biashara

Wazo jepesi kabisa ambalo halina mambo mengi ni katika pia tasinia ya Utanashati hasa kwa vijana wa kiume. Ingawa hata vijana wa like viatu vya vinahitaji kufanyiwa polishing.

Ukitembea kwenye miji yetu mingi Tanzania utaona watu bado wanafanya kazi vile vile miaka naenda miaka rudi wenye ubunifu ni wachache wengi wamemezwa na utamaduni hawaendelezi biashara zao kama inavyotakiwa hivyo Mimi nimeiona tena fursa katika biashara ya kung'alisha viatu.

Kungalisha viatu ni nini? Ni kule kuondoka vumbi na uchafu mwingine katika ngozi ya kiatu kiwe cha kiume au cha kike.

Ukipita miji yetu utawakuta vijana wanafanya kazi hii wapo katika mazingira ambayo sio rafiki kwa wateja.

Lakini ukiangalia kwa upana na umakini hii biashara ni moja ya biashara inayolipa kupita maelezo mfano kubrashi kiatu kimoja uchukua kama dakika 5 tu na ni shilling 1000 kwa mijini lakini kazi hii imeonekana sio kazi ya wasomi ni kazi ya watu ambayo hawajaenda shule kabisa kitu ambacho sio kweli kila mtanzania anawezafanya hii kazi uwe na master's, degree, diploma, certificate au hauna cheti chochote unaweza kufanya hii biashara.

Mapungufu ya wale wanaoifanya yachukue kama fursa

Hatua ya kwanza nenda katengeneze viti vya wateja vya kukaa wakati wanasafishiwa viatu nitakuonyesha kwenye picha hapo chini.

Tafuta maeneo ya miji yenye mabosi wengi na wafanyakazi wengi mfano kwa Dar es salaam kuna maeneo mengi ila nakutajia baadhi
Mlima city
Posta ya zamani
Posta mpya
Makumbusho
Muhimbili
Kumara
Stationi
Na maeneo mengine mengi baada ya kutengeneza hicho kiti peleka hayo maeneo tafuta wafanyakazi very smart kila kiti kiwe na wafanyakazi wawili mmoja wa wakike na mwingine wa kiume, wape simina ya angalau wiki moja jinsi ya kufanya kazi na kuwa wakalimu kwa wateja.

Hakikisha kila kiti cha polishing kinakuwa na gazeti moja utakuwa unabadilisha mfano Tanzania watu wengi wanapenda kusoma gazeti gani la siasa na la michezo? Fanya utafiti na hakikisha kila unapofungua asubuhi liwepo.

Pia tafuta mtu mpe tenda ya Ku supply karanga kwenye vituo vyako afunge karanga ndogo ndogo ambazo mteja akija anakula wakati anabrashiwa viatu vyake hii ni kwa sababu ya kupata watu wengi.

Tagert ni watu 30-50 kwa kila kiti chako na ili kukwepa kuibiwa unaweza waambia wale wafanyakazi wako kwamba wakulipe wenyewe kwa siku unawaambia mfano kwa siku moja unahitaji shilingi 12000.
Hapo utaweka shilingi 10000 benki na elf moja utawanunulia gazeti na elf moja utaweka kwenye budget ya karanga kila siku

Chukulia umeanza na vituo 5 maana yake ni 5×10000= 50000×30 ni 1.5 million kwa mwezi

Weka malengo ya kuwa na vituo 200 Tanzania nzima utakuwa ukitengeneza pesa kiasi gani?

Unaanza kupanua biashara zako sasa unaongeza viti na kupanuka ikiwezekana Tanzania nzima utapata wateja wa kutosha na unaliteka soko.

Baada ya hapo unaweza kubadilisha strategies za kufanya biashara yako sasa kulingana na watu wengine utakuwa hauwafikii mfano unaweza kuwa na magari ambayo ndani yake utadesign sehemu ya kubrashi viatu vya wateja kulingana na foleni ya Dar unakuwa na magari yanayoanzia Mbagala kuja mjini mbezi stand ya magufuli kuja mjini na Bunju kuja mjini yakipita maeneo mbali mbali unapandisha watu bure na unaweka sehemu ya kusafishwa viatu kwa wakina mama na baba na kucha kwa wakina Dada ndani ya gari.

Utakusanya pesa za kutosha na kampuni ya namna hii sio lazima uwe na pesa nyingi hapana unaweza kuanza hata na kiti kimoja ila kazi inayotakiwa kufanyika ni kwenye marketing.

Hii ni biashara kubwa na hapa nimeongea 30% ya hiyo idea.

Naomba nikomee hapa kwa Leo nitaongeza pia kesho

View attachment 1855872

View attachment 1855873

View attachment 1855874
 
Fursa maana yake ulione tatizo na utafute njia za kulitatua huku ukitengeneza pesa.

Ndio maana watu wengi ushindwa kuziona fursa maana hawapendi kutatua matatizo.

Dactari anatibu mgonjwa na anapata pesa
Mwalimu anapelekewa mwanafunzi hasiyejua kusoma wala kuandika anamtengeneza yeye kuwa Dactari, Mwalimu wake na mwalimu au injinia.

Niende kwenye mada; Tanzania ni kama nchi zingine ambazo zinaendea hivyo Tanzania ina fursa nyingi sana kama ambavyo nchi zote zinazoendelea zilivyojaa fursa.

Kwa kutumia technojia ya habari na mawasiliano kuna fursa kubwa naenda kukupa hapa chini.

Unaanzaje? Zunguka mitaa yote ya Tanzania hasa mijini utakutana na matangazo ya karatasi mtaani huyu anatangaza Shule, huyu anatangaza Chuo, huyu anatangaza ajira, huyu anatangaza tenda, wengine wanajitangaza nyakati za uchaguzi lakini zile Karatasi uwa zinaacha uchafuzi mkubwa wa mazingira hasa kuta mbalimbali za majengo maeneo mbali mbali mijini.

Hii ni fursa kwa sababu zifuatazo
1: Hakuna serikali yeyote duniani inayopenda mazingira yake yachafuliwe

2: Serikali itailinda biashara yako kwa sababu itapanua wigo wa ukusanyaji kodi

3: Makampuni wanatumia gharama kubwa sana kutangaza maana wanachapisha wenyewe matangazo, Wanayasambaza wenyewe na wanayalinda wenyewe yasibanduliwe yalipowekwa utawashawishi kwa kuwafanyia kila kitu.

4: Watu wengi utapeliwa pesa na baadhi ya makampuni hewa ambayo utangaza fursa hewa kwa sababu hakuna monitoring kwa makampuni husika.

Hizi hoja tatu zitakufanya upate pesa wewe kwa kutumia fursa hii ipasavyo.

Jinsi ya kuanza: Kasajili kampuni BRELA ambayo inajihusisha na mambo ya tekinolojia ya mawasiano, Pata Till namba na Reseni ya biashara anza kazi hivi.

Zitumie halimashauri za miji na majiji na uhakikishe unapata eneo la kujenga note board ambayo nitaonyesha picha yake hapo chini, Notes board zako ziwekewe taa ( electrical instillation) yaani wakati wa usiku iwake na waambie halimashauri ya kampuni yako itakapoanzia kwamba unahitaji tenda za matangazo yao uwe unawatangazia bure kwenye notes board zako watakupa

Fanya lobbying katika halimashauri hiyo wapige marufuku matangazo kubandikwa ovyo ovyo kwa kuwaelezea hasara zake kama nilivyozitaja hapo juu likiwepo swala la kodi waambie wewe utalipa kodi na VAT.

Hakuna halimashauri itagoma kukupa hii fursa hapo utatengeneza team kwenda maofisi yote na kuomba matangazo na kuacha mawasiliano ya kampuni yako.

Utatoa ajira kwa vijana maana kila kitu kitafanywa na kampuni yako kama Kudezaini, Kusimamia matangazo yenye kutaka kutapeli watu hii itakufanya kuwa karibu sana na Makampuni mengi na Serikali.

Pia hakikisha unakuwa na notes board za kutosha mjini pia uwe mbunifu mfano notes board chini yake unaweza kuweka kituo cha kuuzia magazeti kwenye kila notes board yako na kuwapa bule vijana watumie kuuzia huku wakilinda notes board ya kampuni yako na hii itakusaidia kwenye masoko maana watu wengi usimama kwenye vituo vya magazeti hivyo itakufanya upate wateja wengi wanafika kwenye notes board za kampuni yako na wakati huo kuwashawishi wateja watangaze na wewe.

Utaweka bei ya kawaida ya kuanzia kwa kigezo cha mtu au kampuni inataka kutangaziwa wapi? Kama ni note board moja labda ya posta utajua bei yako iweje kuna mwingine atakwambia anataka kutangaza notes board zote za Dar yaani (promotion announcement) utaweka utaratibu.

Nakaribisha maswali kwa fursa hii labda kama kuna jambo nimesahau kuliandika niulize nitakujibu

Kesho nitakuja na fursa nyingineView attachment 1854903View attachment 1854904
Uzi mzuri huu
 
Back
Top Bottom