SoC01 Unahitaji kuanzisha biashara? Chukua fursa hii

Stories of Change - 2021 Competition

Nawatania

Senior Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
148
Reaction score
549
Fursa maana yake ulione tatizo na utafute njia za kulitatua huku ukitengeneza pesa.

Ndio maana watu wengi ushindwa kuziona fursa maana hawapendi kutatua matatizo.

Daktari anatibu mgonjwa na anapata pesa
Mwalimu anapelekewa mwanafunzi hasiyejua kusoma wala kuandika anamtengeneza yeye kuwa Dactari, Mwalimu wake na mwalimu au injinia.

Niende kwenye mada; Tanzania ni kama nchi zingine ambazo zinaendea hivyo Tanzania ina fursa nyingi sana kama ambavyo nchi zote zinazoendelea zilivyojaa fursa.

Kwa kutumia technojia ya habari na mawasiliano kuna fursa kubwa naenda kukupa hapa chini.

Unaanzaje? Zunguka mitaa yote ya Tanzania hasa mijini utakutana na matangazo ya karatasi mtaani huyu anatangaza Shule, huyu anatangaza Chuo, huyu anatangaza ajira, huyu anatangaza tenda, wengine wanajitangaza nyakati za uchaguzi lakini zile Karatasi uwa zinaacha uchafuzi mkubwa wa mazingira hasa kuta mbalimbali za majengo maeneo mbali mbali mijini.

Hii ni fursa kwa sababu zifuatazo

1: Hakuna serikali yeyote duniani inayopenda mazingira yake yachafuliwe

2: Serikali itailinda biashara yako kwa sababu itapanua wigo wa ukusanyaji kodi

3: Makampuni wanatumia gharama kubwa sana kutangaza maana wanachapisha wenyewe matangazo, Wanayasambaza wenyewe na wanayalinda wenyewe yasibanduliwe yalipowekwa utawashawishi kwa kuwafanyia kila kitu.

4: Watu wengi utapeliwa pesa na baadhi ya makampuni hewa ambayo utangaza fursa hewa kwa sababu hakuna monitoring kwa makampuni husika.

Hizi hoja tatu zitakufanya upate pesa wewe kwa kutumia fursa hii ipasavyo.

Jinsi ya kuanza: Kasajili kampuni BRELA ambayo inajihusisha na mambo ya tekinolojia ya mawasiano, Pata Till namba na Reseni ya biashara anza kazi hivi.

Zitumie halimashauri za miji na majiji na uhakikishe unapata eneo la kujenga note board ambayo nitaonyesha picha yake hapo chini, Notes board zako ziwekewe taa ( electrical instillation) yaani wakati wa usiku iwake na waambie halimashauri ya kampuni yako itakapoanzia kwamba unahitaji tenda za matangazo yao uwe unawatangazia bure kwenye notes board zako watakupa

Fanya lobbying katika halimashauri hiyo wapige marufuku matangazo kubandikwa ovyo ovyo kwa kuwaelezea hasara zake kama nilivyozitaja hapo juu likiwepo swala la kodi waambie wewe utalipa kodi na VAT.

Hakuna halimashauri itagoma kukupa hii fursa hapo utatengeneza team kwenda maofisi yote na kuomba matangazo na kuacha mawasiliano ya kampuni yako.

Utatoa ajira kwa vijana maana kila kitu kitafanywa na kampuni yako kama Kudezaini, Kusimamia matangazo yenye kutaka kutapeli watu hii itakufanya kuwa karibu sana na Makampuni mengi na Serikali.

Pia hakikisha unakuwa na notes board za kutosha mjini pia uwe mbunifu mfano notes board chini yake unaweza kuweka kituo cha kuuzia magazeti kwenye kila notes board yako na kuwapa bule vijana watumie kuuzia huku wakilinda notes board ya kampuni yako na hii itakusaidia kwenye masoko maana watu wengi usimama kwenye vituo vya magazeti hivyo itakufanya upate wateja wengi wanafika kwenye notes board za kampuni yako na wakati huo kuwashawishi wateja watangaze na wewe.

Utaweka bei ya kawaida ya kuanzia kwa kigezo cha mtu au kampuni inataka kutangaziwa wapi? Kama ni note board moja labda ya posta utajua bei yako iweje kuna mwingine atakwambia anataka kutangaza notes board zote za Dar yaani (promotion announcement) utaweka utaratibu.

Nakaribisha maswali kwa fursa hii labda kama kuna jambo nimesahau kuliandika niulize nitakujibu

Kesho nitakuja na fursa nyingine
 
Upvote 31
Yuko old stone age eti notice board,hata shule siku hizi matokeo no online
Mkuu acha kupotoka na kupotosha..., kuna kitu kinaitwa niche market, pia kuna market segmentation na target marketing...

Hivi unadhani kwa mama anayepika maandazi kitaa au anayepangisha kachumba au tuseme mtu ambaye wateja wake wanatokea mtaani pekee ukimpa choice aweke tangazo lake kwenye mti wa kijiwe cha gahawa mataani / au dukani kwa mangi na kutangaza facebook au kwenye CNN America wapi patakuwa na impact kwa biashara yake?

Unadhani traffic ya watu wa mtaani dukani kwa mangi itazidiwa na watu wanaoingia instagram kuangalia issue nyingine ambapo kwao matangazo ni kero (tena wanatafuta adblocker kabisa)....

Au jamii ya kitaa ambao smartphone kwao hata kutumia hawawezi unadhani itakuwa bora uwatangazie kigodoro kitakuwepo saa ngapi kwenye facebook au sehemu wanapojumuika mtaani ?
 
Mama lishe aweke tangazo kwenye notice board?anamlenga nani?
 
Mama lishe aweke tangazo kwenye notice board?anamlenga nani?
Walaji wake mtaani; au wajenzi wanaokuja kujenga nyumba pale mtaani ambao ni wageni wakifuata sigara dukani kuna namba zake pale "Kwa Chai Makande, Vitumbua na Miguu ya Kuku nipigie Au Order za Kesho muachie Mangi" Au Nimehama kijiwe nimetoka mtaa wa tatu kwa Zuberi sasa Nipo Barabara ya Saba mkabala na Shimo la Taka"

Au Mtori umerudi Wateja wangu Karibuni tena Nimeshatoka Rombo....
 
Tangazo la hivyo halihitaji notice board unabandika tu ukutani au kwenye nguzo ya umeme kama yale ya waganga wa kienyeji au vyuo vya mitaani,naomba ustick kwenye notice board
 
Tangazo la hivyo halihitaji notice board unabandika tu ukutani au kwenye nguzo ya umeme kama yale ya waganga wa kienyeji au vyuo vya mitaani,naomba ustick kwenye notice board
Moja Mdau kasema badala ya watu kuchafua mistimu pawe na specified location....

Pili nadhani hakuna sehemu yenye traffic mtaani kama dukani au kijiweni (hivyo jamaa akiongea na mangi akaweka bango lake pale watu watasoma na huenda wakakubali kutoa chochote)

Sisemi kwamba atapata pesa (biashara ya matangazo sasa hivi ni ngumu hata online inabidi uwe na akili usiuze matangazo bali utoe content zenye matangazo kwa siri); Point yangu ni kwamba kuna watu ambao ukitaka kuwatarget notice board ina impact kuliko other medium of communication (though not sure they will be willing to pay a lot) ingawa unaweza kuingia nao mkataba kama ni chumba au gari badala ya kulipia tangazo ukapata commission...
 
Kama umekiri kuwa biashara ya matangazo nowadays ni ngumu nashukuru atleast unaonekana unajua unachoongea,na ni ngumu kweli
 
Well asante kwa kunijibia
 
Idea nzuri, ungeifanya a separate thread ili watu wengi waione; imeruhusiwa pia kuwa na threads nyingi ila itakayoshinda ni moja!
 
Uzi mzuri huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…