Unaifahamu vipi CocaCola?

Unaifahamu vipi CocaCola?

Jamii forum ni sehemu yenye watu wa kila aina ,(wadukuzi wa mambo) vipo vitu vingi ambavyo vimepata majibu na pia wengi wamefahamu mengi sana kupitia jamii forum (hongereni wote wanaoshiriki kikamilifu kutoa taarifa mbalimbali hapa JF)

Ila leo ninahitaji tusaidiane katika hili,kuhusu kampuni ya coca cola ambayo ina miaka 130 tangu kuanzishwa kwake (may 08,1886)

Kampuni hii licha ya kuuza kuliko kampuni yeyote ile ya vinywaji hapa duniani ina mambo mengine ambayo ni siri sana naomba kwa mwenye ufahamu wake anaweza kutushirikisha.

Inasemekana kampuni hii licha ya kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi na kueneka karibia dunia nzima ni watu wawili tu wanafahamu kuhusu utengenezaji wa vinywaji vya kampuni hii.

Nilipata mshituko kuhusu siri hii kipi kipo nyuma ya pazia ,imebidi nije JF kushirikishana juu ya kampuni hii,(japo sina nia ya kuwatangaza vibaya ila ninahitaji kufahamu).

Ntashukuru kwa wote watakaofanikisha hili na kuweka nondo zenye kuhusu kampuni hii.
Kwahiyo mkuu unataka mwenye kujua hiyo siri inayojulikana na watu 2 tu na ambayo imefichwa kwa takribani miaka 130,au unataka kujua kwa undani kuhusu kampuni ya Cocacola na kinywaji chao?
 
Huu ni uzushi tu.

Sasa kama ni wawili tu wanaojua, hawa wa hapa nyerere road wanatumia compounds zip kuipata coca??? Na wakati hawajui??? Au inashushwa na ndege na kujazwa ktk vyupa???
Inakuja kama concentrate kisha inachanganywa na maji hapa dar.
 
Bado hii kitu inapipa wakati mgumu kuielewa - yaani chemical analyser zenye latest technology zishindwe kujua ingredients zilizo changanywa kwenye soda ya CocaCola? Kisayansi ukichukua mls fulani utajua kiwanga cha single ingredient per ml wala hilo si kazi kubwa - unless wakisema labda concentrates hizo uhifadhiwa darini zikiwa kwenye barrels maalum zilizo tengenezwa kwa mbao, stainless steel au Aluminium zinabaki huko kwa miaka minne at a controlled temperature kama Whiskey na Wine hapo naweza kuwaelewa - hiyo ndiyo siri ambayo si raisi kuijua, lakini linapo kuja saula la ingredients hilo ni raisi kuli crack na concentration ya every single ingredient per mole itajulikana tu - kazi hiyo mpe Dk.Magufuli kama hatakupa majibu in no time.
Hata mm najiuliza hapo Mkuu, hii dunia ya sasa iliyojawa na Wanasayansi nguli washindwe kujua hiyo formula? Sio rahisi kwa kweli. Labda kama kuna kingine.
 
Mi naona licha ya kufanya ziara ya kushtukiza huko viwandani, hata tuseme wakiingia kitaa kujinunulia tu kama wateja wa kawaida, watazibaini hizo tofauti kiurahisi sana.

Na naamini wanalijua hilo maana ukienda pale World of Coca-Cola utakuta maelezo yanayoelezea utofauti wa bidhaa zao kulingana na maeneo husika kwa sababu masoko ndo hu determine bidhaa iweje kwenye soko flani.

Kuhusu hilo la secret recipe...huenda ikawa ni marketing ploy ya kujenga mystique flani juu ya bidhaa yao.

Kwa hiyo huenda wala hamna secret recipe yoyote ile ila tunaambiwa tu kuna 'closely guarded secret' ili kujenga hiyo mystique na hiyo mystique ndo inajenga mvuto na huo mvuto ndo unajenga raghba [interest].

Na hiyo raghba ndo inaongeza biashara. Na biashara inapoongezeka faida nayo inakua.

Hao jamaa usikute wanacheza tu na akili za watu maana kama ulivyosema, yaani kweli kabisa pamoja na maendeleo yote haya ya kisayansi wakemia wasijue vilivyomo kwenye hicho kinywaji?

Ngumu sana kuamini hiyo. Ndo maana nahisi huenda suala zima likawa ni marketing ploy tu.
Upo sahihi kabisa, mfano hapa kuna watu wataenda kutest coca cola ili kuona utofauti. Watajiona wao ni wa kipekee wakinywa Coca.
 
Yupo MTU aliyegundua hicho kinywaji,by then alitaka kitumike kutibu ugonjwa wa kifua(kikohozi). Haikutibu but watu waliokunywa walikipenda kinywaji na kukiona ni refreshing. So jamaa akamix tena watu kunywa wakanogewa. Hapo ndio kikaanza kutengenezwa na kunyweka km kiburudisho. Watu wakanunua formula kutoka kwa mgunduzi na kuanza kutengeneza. Ikaja wazo la chupa za kuhifadhia na lebo as in jina LA kinywaji maana kina asili ya colanuts.
Siwezi kuandika yote hapa ila badae dunia nzima ikajua na watu kutaka kuzalisha kinywaji husika. Mpango ukawa ni kununua kibali cha kuzalisha then unazalisha chini ya masharti yao. Hapo ndio linakuja suala la concentrates and chemicals husika za kuzalishia coca.
Africa kipo kiwanda cha kuzalisha hizo concentrates na sio lazma utoe U.S.A. Pia sio kila coca ya Tanzania iko chini ya Mengi. Kuna kiwanda Dar,Mbeya,Moshi na Mwanza. Mengi yupo Moshi tu,Mwanza wamiliki wengine na Dar na mbeya zipo chini ya MTU mmoja mwingine. Yaani hao wahusika wote wanakibali cha kuzalisha,kusambaza na kuuza na wana mipaka ya kimasoko. Yaani Mengi anauza soda zake maeneo/mikoa maalum bila kuingiliana na wengine. Hii ni moja ya masharti na vigezo ambavyo vinafuatwa na kusimamaiwa from coca mwenyewe kuepusha Shari kwenye biashara.
 
Kwenye uzalishaji pia kuna variations zimeruhusiwa,kwa maana ya kiwango cha gesi au sukari. Ilimradi soda iko ndani ya viwango vilivyoruhusiwa,hata hao wahusika wa nje hawana tatizo. So usishangae soda ya moshinkuwa tofauti na ya Mbeya,Mwanza au Dar. Hata ya Mwanza ya Leo na keshokutwa zaweza kuwa na utofauti japo huwa ni mdogo kiladha mdomoni.
 
It's supposed to be one of the most closely guarded trade secrets on Earth – so secret that only two employees know it at any one time. The recipe of Coca Cola contains a list of 'secret' ingredients known as '7X' – herbal extracts which give the drink it's unique flavour, which the company has guarded for a century.
 
Upo sahihi kabisa, mfano hapa kuna watu wataenda kutest coca cola ili kuona utofauti. Watajiona wao ni wa kipekee wakinywa Coca.

Unaposikia kwamba eti kuna watu wawili tu waijuayo hiyo recipe unajiwa na maswali kichwani...kwamba yawezekana ni bonge la siri.

Lakini kwa mtaji huo huo kama una akili utajiuliza..ina maana kwa miaka yote hiyo ni watu hao hao wawili ndo wenye kuijua hiyo siri?

Yaani tokea miaka ya 1800 huko ni hao watu wawili tu ndo wenye kuijua? Hao watu hawafi? Wanaishi milele?

Hiyo inayoitwa siri ina nini spesho? Mbona kinywaji chenyewe ni cha kawaida tu...

Uspesho wa Coca-Cola ni nini hasa hadi kuwepo na bonge la siri ya formula yake kwa miaka yote hiyo?

Binafsi bado nina mashaka kwa uwepo wa hiyo siri. Huenda wala haipo na kilichopo ni hekaya tu.

Siri gani hiyo inayojulikana kuwa ni siri? Mimi nijuavyo siri huwa hata hazijulikani kuwa ni siri.
 
Duh! Huu mjadala naona bado haujafungwa.. Aisee

Naona comment nyingi zinaeleza kwamba inawezekanaje na maendeleo makubwa hivi lakini washindwe kung'amua hizo recipe.. Nimeeleza kwenye bandiko langu la kwanza kuwa kuna wanasayansi wameweza 'kucrack' hiyo sercret recipe lakini tatizo limebaki kwenye viwango vya uchanganyaji na namna ya kuchanganya..
Labda nieleze kwa mapana.!! Kuna nadharia au tuseme attempt kadhaa zilizofanyika kung'amua hiyo secret recipe..

Nadharia # 1: Reed Recipe

Ung'amuzi huu uliletwa na mfamasia John reed, na akadai kuwa coca cola wanatumia vifuatavyo kutengeneza hiyo secret recipe;
Citrate of caffeine, citric acid, lime juice, maji, sukari, umaji maji wa zao la kola, umaji maji wa zao la coca, vanilla extract.

Anadai kuwa vitu hivi vikichanganywa katika viwango sahihi unapata ladha ya coca cola! Coca cola wenyewe wamepinga hili kuwa waliacha kutumia kola katika vinywaji vyao miaka ya 1980 na pia hawatumii lime juice.

Nadharia # 2: Merory Recipe

Hii imechapishwa kwenye kitabu cha Food Flavourings.. Uchambuzi wake uko complex kiasi kwamba unahitaji uelewa wa juu wa kemia kuelewa (binafsi nimetoka kapa nimeekewa kiduchu sana) Lakini moja ya vitu walivyovieleza kuwa recipe hiyo ina "extract ya cocaine" pamoja na Tuloul..

Coca cola wamepinga vikali hii nadharia..

Nadhari #3: Pemberton Recipe
(Hii ndio nadharia inayoaminika zaidi)

Nadharia hii imedukuliwa kutoka kwenye diary ya mgunduzi wa kinywaji cha coca cola Bw. John S. Pemberton.
Diary hiyo inaeleza vitu vifuatavyo ambavyo ndio vinaamini labda vinatumia kutengeneza hiyo recipe;
Alcohol, chungwa (oil orange), cinnamon (oil cinnamon), lemon (oil lemon), nutgem (oil nutgem), nerioli (oil norioli), coriender (oil coriender)

Kisha vinachanganywa na ingredients za caramel, coca leaf, vanilla extract, caffeine.

Kitendawili ni viwango gani vinapaswa kutumiwa kwa kila 'kiungo' na vipikwe kwa muda gani, na kwenye uchanganyaji kipi kinaanza na kipi kinafuata na vichanganywe kwa stahili gani.

Jambo la mwisho; sijaeleza kuwa ni watu wawili pekee kwenye historia wanaojua hii siri, bali nimesema ni wafanyakazi wachache (wengi husema wawili) wanaofahamu hiyo siri katika muda husika (at a given time).

The Bold.

Cc: Bukyanagandi, Nyani Ngabu, Raphael wa Ureno, Aleyn
 
Swali gumu, watu wawili ndo wanajuwa siri ya Coca-Cola je hawa watu 2 hawafi maana ina zaidi ya miaka 100 hii company. Kuna utaratibu gani unaotumia kurithishana ujuzi.
 
Inatengenezwa na mmea wa coca yaani coca plant,mmea huu ndio malighafi ya cocaine
Cocacola ina addiction kwa watumiaji
 
mkuu kwa sasa wanasayansi wanaweza vitu vingi ambavyo viko complicated ! sembuse hiyo ya coca ? hati miliki baba ndio issue……!!
 
Swali gumu, watu wawili ndo wanajuwa siri ya Coca-Cola je hawa watu 2 hawafi maana ina zaidi ya miaka 100 hii company. Kuna utaratibu gani unaotumia kurithishana ujuzi.

Mimi nahisi huenda hiyo ni stori tu ya kukuza na kuendeleza legend ya Coca-Cola.

Nahisi huenda hata hakuna siri ila tumeaminishwa tu kuwa ipo.

Na kweli tushaaminishwa kuwa kuna siri basi ukweli pengine hatutakuja kuujua.

We fikiria....ni siri gani hiyo ambayo watu huambiwa ipo?

Nijuavyo mimi kama kitu ni siri basi hata kujua uwepo wake huwezi kujua.

Lakini hii ya Coca-Cola eti tunajua ipo ila hatuijui ni siri gani.

Nasita kuamini.

Nadhani ni mbinu tu ya kibiashara inayofanya watu waendelee kuwa na raghba na hiyo bidhaa.

Imagine unakunywa kinywaji ambacho unaambiwa recipe yake ni bonge la siri....si utajisikia kuwa unakunywa bonge la kinywaji....

Bado sana kuamini hilo.
 
Huu ni uzushi tu.

Sasa kama ni wawili tu wanaojua, hawa wa hapa nyerere road wanatumia compounds zip kuipata coca??? Na wakati hawajui??? Au inashushwa na ndege na kujazwa ktk vyupa???

nyinyi mnaletewa vitu vilivyotengenezwa tayar! yaan kama ni cement nyny mnatia maj 2 mpate zege
 
Kwa taarifa yako tu ni kuwa katika Patent zenye thamani kuliko zote duniani ya coca cola ndio namba moja,

pia ndio inayolindwa kuliko zote, ndio maana hadi leo hiyo ni siri kubwa sana, hao wengine akina pepsi na wenzake wanajaribu kutengeneza lakini hawawezi kutoa kama koka.

hiyo ni siri ya familia, na sio wanafamilia wote wanajua.
akifa baba anamuachia mtoto
Wakifa wote kwa pamoja?
 
Miongoni mwa siri kubwa ni kuficha kiwango cha sukari kilichomo. Ni hatari sana. Angalia hapa rais wa cococola europe anavyobanwa kuhusu kiasi cha sukari!!

Back
Top Bottom