Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Hapa nilipo Pepsi inakimbiza vibaya mnosokoni kukoje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa nilipo Pepsi inakimbiza vibaya mnosokoni kukoje?
namaanisha dunianiHapa nilipo Pepsi inakimbiza vibaya mno
OK.namaanisha duniani
Kwahiyo mkuu unataka mwenye kujua hiyo siri inayojulikana na watu 2 tu na ambayo imefichwa kwa takribani miaka 130,au unataka kujua kwa undani kuhusu kampuni ya Cocacola na kinywaji chao?Jamii forum ni sehemu yenye watu wa kila aina ,(wadukuzi wa mambo) vipo vitu vingi ambavyo vimepata majibu na pia wengi wamefahamu mengi sana kupitia jamii forum (hongereni wote wanaoshiriki kikamilifu kutoa taarifa mbalimbali hapa JF)
Ila leo ninahitaji tusaidiane katika hili,kuhusu kampuni ya coca cola ambayo ina miaka 130 tangu kuanzishwa kwake (may 08,1886)
Kampuni hii licha ya kuuza kuliko kampuni yeyote ile ya vinywaji hapa duniani ina mambo mengine ambayo ni siri sana naomba kwa mwenye ufahamu wake anaweza kutushirikisha.
Inasemekana kampuni hii licha ya kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi na kueneka karibia dunia nzima ni watu wawili tu wanafahamu kuhusu utengenezaji wa vinywaji vya kampuni hii.
Nilipata mshituko kuhusu siri hii kipi kipo nyuma ya pazia ,imebidi nije JF kushirikishana juu ya kampuni hii,(japo sina nia ya kuwatangaza vibaya ila ninahitaji kufahamu).
Ntashukuru kwa wote watakaofanikisha hili na kuweka nondo zenye kuhusu kampuni hii.
Inakuja kama concentrate kisha inachanganywa na maji hapa dar.Huu ni uzushi tu.
Sasa kama ni wawili tu wanaojua, hawa wa hapa nyerere road wanatumia compounds zip kuipata coca??? Na wakati hawajui??? Au inashushwa na ndege na kujazwa ktk vyupa???
Hata mm najiuliza hapo Mkuu, hii dunia ya sasa iliyojawa na Wanasayansi nguli washindwe kujua hiyo formula? Sio rahisi kwa kweli. Labda kama kuna kingine.Bado hii kitu inapipa wakati mgumu kuielewa - yaani chemical analyser zenye latest technology zishindwe kujua ingredients zilizo changanywa kwenye soda ya CocaCola? Kisayansi ukichukua mls fulani utajua kiwanga cha single ingredient per ml wala hilo si kazi kubwa - unless wakisema labda concentrates hizo uhifadhiwa darini zikiwa kwenye barrels maalum zilizo tengenezwa kwa mbao, stainless steel au Aluminium zinabaki huko kwa miaka minne at a controlled temperature kama Whiskey na Wine hapo naweza kuwaelewa - hiyo ndiyo siri ambayo si raisi kuijua, lakini linapo kuja saula la ingredients hilo ni raisi kuli crack na concentration ya every single ingredient per mole itajulikana tu - kazi hiyo mpe Dk.Magufuli kama hatakupa majibu in no time.
Upo sahihi kabisa, mfano hapa kuna watu wataenda kutest coca cola ili kuona utofauti. Watajiona wao ni wa kipekee wakinywa Coca.Mi naona licha ya kufanya ziara ya kushtukiza huko viwandani, hata tuseme wakiingia kitaa kujinunulia tu kama wateja wa kawaida, watazibaini hizo tofauti kiurahisi sana.
Na naamini wanalijua hilo maana ukienda pale World of Coca-Cola utakuta maelezo yanayoelezea utofauti wa bidhaa zao kulingana na maeneo husika kwa sababu masoko ndo hu determine bidhaa iweje kwenye soko flani.
Kuhusu hilo la secret recipe...huenda ikawa ni marketing ploy ya kujenga mystique flani juu ya bidhaa yao.
Kwa hiyo huenda wala hamna secret recipe yoyote ile ila tunaambiwa tu kuna 'closely guarded secret' ili kujenga hiyo mystique na hiyo mystique ndo inajenga mvuto na huo mvuto ndo unajenga raghba [interest].
Na hiyo raghba ndo inaongeza biashara. Na biashara inapoongezeka faida nayo inakua.
Hao jamaa usikute wanacheza tu na akili za watu maana kama ulivyosema, yaani kweli kabisa pamoja na maendeleo yote haya ya kisayansi wakemia wasijue vilivyomo kwenye hicho kinywaji?
Ngumu sana kuamini hiyo. Ndo maana nahisi huenda suala zima likawa ni marketing ploy tu.
Upo sahihi kabisa, mfano hapa kuna watu wataenda kutest coca cola ili kuona utofauti. Watajiona wao ni wa kipekee wakinywa Coca.
Wanaojua formula ni watu wawili tu hapa Tz,mengi na klyn!
mkuu kwa sasa wanasayansi wanaweza vitu vingi ambavyo viko complicated ! sembuse hiyo ya coca ? hati miliki baba ndio issue……!!Duh! Huu mjadala naona bado haujafungwa.. Aisee
Naona comment nyingi zinaeleza kwamba inawezekanaje na maendeleo makubwa hivi lakini washindwe kung'amua hizo recipe.. Nimeeleza kwenye bandiko langu la kwanza kuwa kuna wanasayansi wameweza 'kucrack' hiyo sercret recipe lakini tatizo limebaki kwenye viwango vya uchanganyaji na namna ya kuchanganya..
Labda nieleze kwa mapana.!! Kuna nadharia au tuseme attempt kadhaa zilizofanyika kung'amua hiyo secret recipe..
Nadharia # 1: Reed Recipe
Ung'amuzi huu uliletwa na mfamasia John reed, na akadai kuwa coca cola wanatumia vifuatavyo kutengeneza hiyo secret recipe;
Citrate of caffeine, citric acid, lime juice, maji, sukari, umaji maji wa zao la kola, umaji maji wa zao la coca, vanilla extract.
Anadai kuwa vitu hivi vikichanganywa katika viwango sahihi unapata ladha ya coca cola! Coca cola wenyewe wamepinga hili kuwa waliacha kutumia kola katika vinywaji vyao miaka ya 1980 na pia hawatumii lime juice.
Nadharia # 2: Merory Recipe
Hii imechapishwa kwenye kitabu cha Food Flavourings.. Uchambuzi wake uko complex kiasi kwamba unahitaji uelewa wa juu wa kemia kuelewa (binafsi nimetoka kapa nimeekewa kiduchu sana) Lakini moja ya vitu walivyovieleza kuwa recipe hiyo ina "extract ya cocaine" pamoja na Tuloul..
Coca cola wamepinga vikali hii nadharia..
Nadhari #3: Pemberton Recipe
(Hii ndio nadharia inayoaminika zaidi)
Nadharia hii imedukuliwa kutoka kwenye diary ya mgunduzi wa kinywaji cha coca cola Bw. John S. Pemberton.
Diary hiyo inaeleza vitu vifuatavyo ambavyo ndio vinaamini labda vinatumia kutengeneza hiyo recipe;
Alcohol, chungwa (oil orange), cinnamon (oil cinnamon), lemon (oil lemon), nutgem (oil nutgem), nerioli (oil norioli), coriender (oil coriender)
Kisha vinachanganywa na ingredients za caramel, coca leaf, vanilla extract, caffeine.
Kitendawili ni viwango gani vinapaswa kutumiwa kwa kila 'kiungo' na vipikwe kwa muda gani, na kwenye uchanganyaji kipi kinaanza na kipi kinafuata na vichanganywe kwa stahili gani.
Jambo la mwisho; sijaeleza kuwa ni watu wawili pekee kwenye historia wanaojua hii siri, bali nimesema ni wafanyakazi wachache (wengi husema wawili) wanaofahamu hiyo siri katika muda husika (at a given time).
The Bold.
Cc: Bukyanagandi, Nyani Ngabu, Raphael wa Ureno, Aleyn
Swali gumu, watu wawili ndo wanajuwa siri ya Coca-Cola je hawa watu 2 hawafi maana ina zaidi ya miaka 100 hii company. Kuna utaratibu gani unaotumia kurithishana ujuzi.
Huu ni uzushi tu.
Sasa kama ni wawili tu wanaojua, hawa wa hapa nyerere road wanatumia compounds zip kuipata coca??? Na wakati hawajui??? Au inashushwa na ndege na kujazwa ktk vyupa???
Wakifa wote kwa pamoja?Kwa taarifa yako tu ni kuwa katika Patent zenye thamani kuliko zote duniani ya coca cola ndio namba moja,
pia ndio inayolindwa kuliko zote, ndio maana hadi leo hiyo ni siri kubwa sana, hao wengine akina pepsi na wenzake wanajaribu kutengeneza lakini hawawezi kutoa kama koka.
hiyo ni siri ya familia, na sio wanafamilia wote wanajua.
akifa baba anamuachia mtoto