Aloo umenikumbusha machungu mkuu, hii mechi ilinifanya niichukie sana michuano ya uefa champs league, yaani baada ya mechi kuisha sikuamini kabisa na ilichukua muda kuamini. Fara sana yule mu Hungary aliyochezesha hii mechi namuombeaga kifo mpaka leo!
Nikikumbuka milima tuliyopitaga mpaka tunafika fainali ule ubingwa ulistahili kuwa wetu, nakumbuka tulimtoa real Madrid tena ile galaticoz iliyokuwa na watu kama Ronoldo, Michael Owen,Robinho,Raul,Beckham na sio hii ya akina benzema. Tukamtoa na juventus liyekuwa mtawala wa ligi ya italy! Nusu fainali tukanusurika kwa Villarreal aliyokuwa tishio kule Spain... Yaani acha tu.
Mimi mpaka mpira unaanza nilikuwa sina wasi wasi kabisa nilijua Barcelona ni ronadinho pekee tu, na kweli Ebue na koro toure walimdhibiti sana ronadinho. Mambo yalikuja kuvurugika baada ya ile red card ya magumashi aloyopewa Lehmann. Ndio Barcelona wakaanza kucheza mpira wao, lakini pamoja na hivyo bado tuliwapiga goli na kuwakosa zingine nyingi tu.
Kuna huyu jamaa wa kuitwa Henrick Larsson huyu ndie aliyekuja kutuharibia sherehe kabisa sijui aliingia na dawa, yaani aliyoingia tu second touch akatoa assist kwa eto'o. Halafu Wenger nae alivyokuwa mwehu walivyochomoa akamtoa Fredrick Leunjberg akamwacha Alexender helb aliyokuwa anasumbuliwa tu na iniesta, tumepigwa goli la pili ana mtoa fabregas ana mleta flamin, nadhani alichanganyikiwa zaidi hata ya mashabaki.
Aisee ile mechi iliniuma sana lakini pia henry nae alitunyima ushindi sababu alipata clear chances kama tatu hivi yuko yeye na valdes halafu zote aliishia kumpa tu.
Anyway Niko Emirates hapa tunamkandamiza Spurs!