Unaikumbuka Brazil hii ya mwisho kubeba Kombe la Dunia?

Unaikumbuka Brazil hii ya mwisho kubeba Kombe la Dunia?

Nakumbuka siku hii Brazil ikicheza fainali na Germany kule Korea/Japan wakati mechi inaendelea mchana hivi tulipigiwa simu kuwa babu amefariki huko kijijini kitu iliyopelekea bi Mkubwa na masista wakaanza kulia sana wengine kwa sauti, ila kwa umaridadi wa Ronaldo de Lima alivyokuwa akimnyanyasa oliver khan ilibidi tuendelee kucheki mechi hadi walipokabidhiwa kombe ñdio tukaanza kusikiliza mambo ya msiba, r.I.p babu kila nikiwaza world cup ya 2002 huwa nakukumbuka.
 
Hii bi Brazil ya mwaka 2002, unakumbuka wachezaji gani kikosini? Ulikuwa wapi wapi wakati Captain Cafu akiinua ndoo ya ubingwa?
2002-world-cup-brazil-all-7-dvd-matches-ronaldo-rivaldo-5681.jpg
Ronaldo De Lima mzee wa kazi, Ronaldinho Gaucho entertainer full raha.

Hawa jamaa ni wachezaji wangu bora wa maisha.
 
Hawa walikuwa moto sana sitasahau manake nilikuwa mshabiki mkubwa sana wa Brazil
 
Enzi hizo zikatoka na big g za stika za wachezaji
 
RONALDINHO, RIVALDO, RONALDO, ROBERTO. Hawa ni watu wabaya sana.
 
Back
Top Bottom