Unaikumbuka kesi ya Zombe; watoto wa 2000 kaeni mbali kidogo

Kuna kipindi kesi za watumishi zinaamuliwa kimchongo.. Sanaa ila wanasahau kuwa haki ya kweli ipo mbinguni..

Hapo ndiyo unakuta dereva anapigwa bastola anakufa mtuhumiwa anaachiwa kuwa aliua bila kukusudia matokeo yake hukumu ya Mungu anakufa kihoroo mwenyewe...Tena guest..

Hata hao ambao waliachiwa kwa hiyo kesi ya wafanya biashara ya madini ukiwaona leoo wapo kama akili imeruka.. Itoshe kusema.. Hakimu wa kweli ni Mungu..
 
Ipoje share kidogo

Sarah unaijua lakini ?
Abdallah Mwamwindi alimuua kwa kumpiga Risasi Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kupeleka maiti kituo cha polisi

Umetisha mshua 👊.... Ngoja ntaipitia
 
Alipokuwa obay pale alikuwa mjivuni sana huyo

Ova
mbona alikua mtu poa sana, tulikua tunahang out sana mkesha wa mwaka mpa kifamilia sjajua maybe i was young kiasi sikuwez kumjua mtu huyu yuko vipi hii ni kabla hajahamia dar na kukumbwa na maseke
 
Kesi ya Zombe ni moja ya kesi maarufu za mauaji nchini Tanzania. Inamhusisha aliyekuwa Afisa wa Polisi, Abdallah Zombe, na maafisa wengine wa polisi waliotuhumiwa kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, mkoani Morogoro, mwaka 2006.

Maelezo ya Kesi

Mnamo Januari 2006, wafanyabiashara hao—Julius Alphonce Msuya, Sadick Kalokola, na Juma Mohamed Malano—walikamatwa na polisi jijini Dar es Salaam wakishukiwa kuwa ni majambazi. Hata hivyo, baadaye walipatikana wameuawa katika eneo la Pande, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Polisi walidai kuwa waliwaua kwa risasi katika "majibizano ya moto" baina yao na majambazi.

Mchakato wa Kesi

  • Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kupangwa, na wahusika walijaribu kuyaficha kama mauaji ya kawaida ya majambazi.
  • Hatimaye, Zombe na maafisa wenzake walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji.
  • Mnamo 2009, Mahakama Kuu ya Tanzania iliwahukumu maafisa wengine wa polisi waliohusika, lakini abdallah Zombe aliachiliwa huru kutokana na ushahidi kutokuwa wa moja kwa moja dhidi yake.
  • Baadaye, upande wa mashtaka ulikata rufaa, lakini Zombe aliendelea kuwa huru.

Umuhimu wa Kesi

Kesi ya Zombe ilizua mijadala mikali kuhusu matumizi ya nguvu kupita kiasi na ukiukwaji wa haki za binadamu ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania. Ilibainisha changamoto katika mfumo wa haki za jinai na umuhimu wa uwajibikaji kwa maafisa wa polisi.
Hadi leo, kesi hii bado inabakia kuwa kumbukumbu muhimu ya changamoto za utawala wa sheria nchini Tanzania
NB:hii nchi imepitia uhuni sana
Kama utakumbuka maneno haya mahakama zetu zina kwenda kwa simu za wakubwa.
 
Hata kama hatukuwepo hampaswi kutufukuza mwacheni tujifunze na sisi kwan enzi za ukoloni ulikuwepo?
 
Kesi ya Zombe ni moja ya kesi maarufu za mauaji nchini Tanzania. Inamhusisha aliyekuwa Afisa wa Polisi, Abdallah Zombe, na maafisa wengine wa polisi waliotuhumiwa kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, mkoani Morogoro, mwaka 2006.

Maelezo ya Kesi

Mnamo Januari 2006, wafanyabiashara hao—Julius Alphonce Msuya, Sadick Kalokola, na Juma Mohamed Malano—walikamatwa na polisi jijini Dar es Salaam wakishukiwa kuwa ni majambazi. Hata hivyo, baadaye walipatikana wameuawa katika eneo la Pande, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Polisi walidai kuwa waliwaua kwa risasi katika "majibizano ya moto" baina yao na majambazi.

Mchakato wa Kesi

  • Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kupangwa, na wahusika walijaribu kuyaficha kama mauaji ya kawaida ya majambazi.
  • Hatimaye, Zombe na maafisa wenzake walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji.
  • Mnamo 2009, Mahakama Kuu ya Tanzania iliwahukumu maafisa wengine wa polisi waliohusika, lakini abdallah Zombe aliachiliwa huru kutokana na ushahidi kutokuwa wa moja kwa moja dhidi yake.
  • Baadaye, upande wa mashtaka ulikata rufaa, lakini Zombe aliendelea kuwa huru.

Umuhimu wa Kesi

Kesi ya Zombe ilizua mijadala mikali kuhusu matumizi ya nguvu kupita kiasi na ukiukwaji wa haki za binadamu ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania. Ilibainisha changamoto katika mfumo wa haki za jinai na umuhimu wa uwajibikaji kwa maafisa wa polisi.
Hadi leo, kesi hii bado inabakia kuwa kumbukumbu muhimu ya changamoto za utawala wa sheria nchini Tanzania
NB:hii nchi imepitia uhuni sana

Hukumu ya mwisho kabisa ya mojawapo ya Wahalifu wa tukio hilo imetolewa leo na Mahakama. Mahakama ya Rufani kwa mara nyingine tena imethibitisha kwamba Askari Polisi Christopher Bageni anapaswa kunyongwa hadi kufa. Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hii ya Tanzania, kwa sasa Mtu huyo hana tena nafasi au Haki nyingine ya Kukata Rufaa Mahakamani ili kupinga Hukumu hiyo. Hukumu hiyo ni ya mwisho kabisa.
Hii ni Habari njema Sana kwa Wapenda HAKI hapa Tanzania.

Ili kulinda maslahi mapana zaidi ya umma katika nchi hii, Rais wa nchi anapaswa ASAINI HATI YA KIFO ya huyu Mtu ili angalau kuanza kurejesha imani iliyopotea miongoni mwa Wananchi dhidi ya vyombo vya Dola, hususani kwa Jeshi la Polisi na Tiss.

Siyo Siri hata kidogo, Wananchi wengi zaidi tayari wamepoteza kabisa Imani dhidi ya Jeshi la Polisi kutokana na vitendo viovu vya uhalifu kama aliofanya huyu Askari Polisi Christopher Bageni.
 
shukrani mwamba
 
Back
Top Bottom