Unaikumbuka timu hii ya Taifa ya Uholanzi

Unaikumbuka timu hii ya Taifa ya Uholanzi

Namuona mikono ya nyani edwin, seedorf, kluivert, edgar, kisiki stam, winga teleza overmars, team captain mwenyewe naona crystal palace wamemkimbiza de boer, zenden, philip cocu, van bronckhorst,reiziger.. mwisho kabisa nmeamua nmtenge peke yake ni fundi wa mafundi dennis bergkamp.. jamaa ni mwisho, skills za hali ya juu, mpira mwing mguuni, soka lake maridadi sio nguvu kulukundu.. mzee wa mabao matamu.. assist za lovely pass.
Huyo Dennis alikuwa fundi kweli ukiachilia mbali uoga wake wa kupanda ndege anabaki kuwa ni mmoja kati ya washambuliaji khatari sana wa orange
 
kwa kipaji cha Marco Reus na majeraha yanayomsibu kila kukicha kuna muda mwingine unaweza ukatokwa na machozi! Hana bahati. Ni kama ilivyotokea kwa akina Owen Hargreaves, Martin Laursen, Dean Ashton na wengineo!
Mzee mwenzangu huyo Owen Hargreaves alikuwa moto nakumbuka game moja kaumia mkongwe Stefan effenberg akaingia waqt mdogo nadhani ilikuwa game na ac Milan duh dogo alipiga mpira mwingi sana.
 
kwa kipaji cha Marco Reus na majeraha yanayomsibu kila kukicha kuna muda mwingine unaweza ukatokwa na machozi! Hana bahati. Ni kama ilivyotokea kwa akina Owen Hargreaves, Martin Laursen, Dean Ashton na wengineo!
Majeraha kwenye soka ni kitu kibaya kinafanya tusione vipaji vilivyotukuka vya baadhi ya watu.. hebu fikiria cr7 au messi wangekuwa pancha km reus, tusingeona ubora wao, ni km vile kifo, fikiria wacko jacko angekufa na miaka mitano, tusingefaidi vibao vikali, bob je!!?

Majeruh aisee yanatunyima raha kiukweli..
 
Huyo Dennis alikuwa fundi kweli ukiachilia mbali uoga wake wa kupanda ndege anabaki kuwa ni mmoja kati ya washambuliaji khatari sana wa orange
Naomba uongeze kweli nyingine, isomeke alikuwa fundi kweli kweli, kuweka msisitizo juu ya kipaji chake kilichotukuka.

Kiukweli soka lake lilikuwa linanikosha kweli kweli, namba 10 ya uhakika, soka la sasa tunakosa namba 10 dizain yake..
 
Namuona mikono ya nyani edwin, seedorf, kluivert, edgar, kisiki stam, winga teleza overmars, team captain mwenyewe naona crystal palace wamemkimbiza de boer, zenden, philip cocu, van bronckhorst,reiziger.. mwisho kabisa nmeamua nmtenge peke yake ni fundi wa mafundi dennis bergkamp.. jamaa ni mwisho, skills za hali ya juu, mpira mwing mguuni, soka lake maridadi sio nguvu kulukundu.. mzee wa mabao matamu.. assist za lovely pass.
Alikua anajenga sana vibanda hata alipokua Arsenal
 
Walikutana na mjomba italy nahisi walikosa bahati tu ila waliupiga mpira mwingi.. uholanzi mara nyingi wanakosa zali.. salipiga mpira mwingi mnoo. Km sikosei walikosa penat mbili ndan ya dakik 90.. golikipa ni toldo yule pale kwa waitaliano..

Kama sikosei Frank alikosa penati ndani ya dakika 90 akakosa penati pia baada ya dakika za nyongeza Toldo aliibuka shujaa Waholanzi hawakuamini maana walikuwa na kikosi kizuri sana.........Ila Waitaliano nao walienda kulizwa fainali na Mfaransa waliuliwa na goli la dhahabu.
 
Kluivert alikosa ndani ya dakika 90 akapata katika penat penat, nahis ni yeye tu ndio alimtungua toldo.
 
Sio uholanzi pekee, ni katika ulimwengu wa soka mkuu. kilikua kikosi bora kabisa. ila walikosa bahati tu.
Dah,mkuu usinikumbushe suala la jamaa kukosa bahati,ilikuwa nusu fainali Uholanzi na Brazil,1998 France,Uholanzi anakufa kwa penalti,niliumia kwa kweli..sidhani kama hawa Holland wangeingia fainali na wenyeji, wenyeji wasingebeba ndoo kirahisi vile..Jamaa walikuwa wametimia kwa kweli..
 
Back
Top Bottom