Unaishi vipi na watu wa mtaani kwenu ulikozaliwa na kuishi huko

Unaishi vipi na watu wa mtaani kwenu ulikozaliwa na kuishi huko

Nimezaliwa katika mtaa ambao kwa sasa naweza ita ni uswahilini, pamoja na wengi kuondoka na kujichanganya kwingine, mimi narudi home karibu kila wiki kwa sababu home zipo biashara zinazonipeleka , pamoja na wengine kuhama bado wapo wenyeji wengi sana wanaoshi hapo mtaani kwetu,.........


.
.........


. Moja ya changamoto ni ile imani ya uliowacha home wanamini umetoboa na maisha umeyapatia ( ukweli sijatoboa maisha ni magumu sana, ) wao homies wakikuona tu ni vizinga na kuomba hela hali hii inaboa sana( kifupi bado sijapata hela isiyokuwa na budget so nikitoa buku nimeharibu hesabu ,nimejaribu mbinu nyingi imeshindikana sasa naishi kwa kujificha ficha tu , ukitokea msiba au tukio la kijamii huwa ni siku ya kuombwa pesa tu, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,, , , , ,,bar huko ni shida utaombwa bia ukome, mara upigiwe simu nimekamatwa kituo cha polisi, mara wakuarike kwenye sherehe flan hivi michango kibao nk , na kumbuka hawa ni homies ndio nikifa watanizika, hawa ndio yakitokea matazizo nyumban wanashiriki,, ndio wananipa deal nyingi , je wewe unaishije nao
Naishi nao vyema tu, na uzuri tangu bado mdogo nilikuwa peace na wengi

Kwa sasa amani inatawala kasoro kwa baadhi ya kaka zetu ambao walituonea bila sababu kisa tu wao wakubwa, hao ndio mpaka kesho wanajishtukia kutokana na unoko waliotufanyia
 
Mi nimezaliwa nakukulia keko machungwa masela nilokuwa nao 70% wamepukutika wameamia walipojenga wazazi wao kama nilivyomimi mzee alivyotuchukuliza nakuami kwenye mjengo wetu nakumbuka nilishawai ludi mtaa wangu wa milembe kuwapa hai nikakabwa wakasepa na A10s toka apo skuludi
Pole mkuu yani wauni wa milembe wamekugeuka au ni namba D umenikumbusha mbali sana milembe,wasumbufu,ubesa wakina banza na kj pale wavurana bango[wavuta bangi] mimi nipo tolori sema machungwa nina wanangu kibao niliskuli nao Mgulani.
 
Mm huwa sirudi kabisaaaa, naogopa kurogwa maana uchawi kwetu umetamalaki.
 
Pole mkuu yani wauni wa milembe wamekugeuka au ni namba D umenikumbusha mbali sana milembe,wasumbufu,ubesa wakina banza na kj pale wavurana bango[wavuta bangi] mimi nipo tolori sema machungwa nina wanangu kibao niliskuli nao Mgulani.
Mgulani nimesoma pale mpaka darasa la4 R.I.P mwal mkuu MJ ila keko kilichokuwa kinaniflaisha chini ya 2005 hakuna nyumba isiokuwa nampiganaji tumejifunza sana kung-fu karate na boxer sijui waliniviziaje wakanikaba watoto wa 2000
 
Mgulani nimesoma pale mpaka darasa la4 R.I.P mwal mkuu MJ ila keko kilichokuwa kinaniflaisha chini ya 2005 hakuna nyumba isiokuwa nampiganaji tumejifunza sana kung-fu karate na boxer sijui waliniviziaje wakanikaba watoto wa 2000
😂😂nimecheka sana hizi habari za keko.

kuna uzi humu wa kitambo sana ulielezea maisha ya keko ya kitambo icho kwa kirefu sana inasemekana uko maisha ni fulu ubabe.

mitaa imejaa magym na madojo yasiyo rasmi😆ukizubaa lazima uchezee makonzi ya pua🤣
 
nilihama kitaa miaka mingi. uwa narudi mara chache sana. kitaa watu wengi ni wapya kwangu. apo kuna mix ya wahamiaji kutoka mikoa na maeneo mengine na wale madogo niliowaacha wanabebwa migongoni na mamazao wananyonya. saivi ni wakubwa ndo wababe apo kitaa. hawa wengi hatufahamiani.

wale wa zamani wa rika langu wengi washasambaa ulimwenguni kufanya maisha yao, waliobaki unakuta ni mmojammoja wale unakuta mtu mzima lakini kwa changamoto za kimaisha bado anaishi kwa mzazi wa kumzaa. hawa wengi mkikutana utajuta.
 
Nimezaliwa katika mtaa ambao kwa sasa naweza ita ni uswahilini, pamoja na wengi kuondoka na kujichanganya kwingine, mimi narudi home karibu kila wiki kwa sababu home zipo biashara zinazonipeleka, pamoja na wengine kuhama bado wapo wenyeji wengi sana wanaoshi hapo mtaani kwetu,.........
.........

Moja ya changamoto ni ile imani ya uliowacha home wanamini umetoboa na maisha umeyapatia (ukweli sijatoboa maisha ni magumu sana) wao homies wakikuona tu ni vizinga na kuomba hela hali hii inaboa sana(kifupi bado sijapata hela isiyokuwa na budget so nikitoa buku nimeharibu hesabu, nimejaribu mbinu nyingi imeshindikana sasa naishi kwa kujificha ficha tu.

Ukitokea msiba au tukio la kijamii huwa ni siku ya kuombwa pesa tu, bar huko ni shida utaombwa bia ukome, mara upigiwe simu nimekamatwa kituo cha polisi, mara wakualike kwenye sherehe flan hivi michango kibao nk. Na kumbuka hawa ni homies ndio nikifa watanizika, hawa ndio yakitokea matazizo nyumbani wanashiriki, ndio wananipa deal nyingi, je wewe unaishije nao?
Daaa sie mtaa tuliokulia NHC waliuza ule mtaa kwa fisadi papa na alibomoa zile nyumba zote tumebaki na mtaa wetu kwenye whatsapp tu.
 
hali hiyo ipo sana tu yaani ukipotea mwaka mmoja wanajua unakula maisha safi, wakikuona wanatamani uwabebe mgongoni 😅
 
Miye sina noma kule kijijini kwetu kuna sehemu wanauza tekawima naenda pale naagiza banga mbili. Wanakunywa miye nakunyw maji mpaka saa nane hivi huuyoo natimua zangu. Na jioni wanakuja pale kwa babu tunapigq stori za zamani na kuulizana nani yuko wapi na anafanya nini yaani shwari kabisa.
 
Miaka hiyo ya 2015 kishuka chini kabla elimu haijavurugwa unaambiwa mtoto wa uswahilini nilifaulu form 4 peke yangu mtaa mzima tena kutoka kwenye hizi shule za kata nilimake headline mtaa mzima kwa kushangaza watu hakuna aliyetegemea maana kamali za kucheza karata na za ma-pooltable,kushinda vijiwe vya bodaboda,mabifu ya makempu,ulikuwa hunikosi.

Na hao wenzangu wengine waliacha shule darasa la nne,tano na sita,wakatupa taulo.Wengine walikaza wakamaliza la saba na mwanangu mmoja RIP rama akaishia form 2.

Nashukuru Mungu nilikuwa na kampani ya hovyo lakini alinipenda kwa kunipa ufahamu mkubwa mkubwa na nilikuwa najielewa flan maana kwakuwa shule nilikuwa kipanga nikawa na best kampani ila home ndio nipo na wahuni lakini nilikuwa natumia muda mwingi shule kuliko nyumbani so uhuni ukapungua na mpka sahv nimeacha ila usela mavi naujua sana.

Basi shule ikanitenga na wana baada ya hapo yakawa yaliyotakiwa yawe.sasahvi wadau wa mtaani wananitafuta sana niwasevu wakijua nina mipango kumbe na mimi hali yangu tete kuliko wao.

Location Gongo la mboto
 
Back
Top Bottom