Unajiandaaje na maisha ya uzeeni?

Unajiandaaje na maisha ya uzeeni?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Uzee ni umri wa kuwa tegemezi kama mtoto mdogo, kama katika ujana wako ulijipanga vizuri na kujiwekeza vya kutosha katika rasilimali fedha, miradi, na watu n.k uzee kwako hautakuwa kero kwa wengine.​

Tofauti na hapo, utakuwa unawaachia laana kwa wale wote watakao kuwa tofauti na matakwa yako katika uzee wako, pale inapotokea kuwa na uhitaji fulani na haufanikiwi.

Kwangu binafsi, napambana na kuwa na watoto wengi, na kama itawezekana huko mbeleni itabidi nitafute eneo la kijiji, angalau ekari kumi, bahati nzuri ardhi kijijini inauzwa bei nafuu; humo ndani niishi na vijana wangu pamoja na mifugo.

Lengo likiwa nikigeuka huku na kule naona vijukuu na watoto ili kupunguza upweke na msongo wa mawazo katika uzee wangu.

Je ,wewe unajiandaaje na maisha ya uzeeni?​
 
Yaani haya maisha usipokuwa makini utakufa ukiwa unajiandaa tu:
  • Ukiwa mtoto unajiandaa na shule
  • Ukiwa shule unajiandaa na kazi au ajira
  • Ukiwa na kazi unajiandaa na uzer
  • Ukiwa mzee unajiandaa na kifo

Umeishi lini sasa?
 
Yaani haya maisha usipokuwa makini utakufa ukiwa unajiandaa tu:
  • Ukiwa mtoto unajiandaa na shule
  • Ukiwa shule unajiandaa na kazi au ajira
  • Ukiwa na kazi unajiandaa na uzer
  • Ukiwa mzee unajiandaa na kifo

Umeishi lini sasa?
Alafu usipojiandaa, kuna uwezekano wa kuishi miaka mingi ya mateso; na ukijiandaa baada ya muda mfupi unakutana na kifo.
Sasa kipi bora?
 
Back
Top Bottom