Unajiandaaje na maisha ya uzeeni?

Unajiandaaje na maisha ya uzeeni?


Uzee ni umri wa kuwa tegemezi kama mtoto mdogo, kama katika ujana wako ulijipanga vizuri na kujiwekeza vya kutosha katika rasilimali fedha, miradi, na watu n.k uzee kwako hautakuwa kero kwa wengine.


Tofauti na hapo, utakuwa unawaachia laana kwa wale wote watakao kuwa tofauti na matakwa yako katika uzee wako, pale inapotokea kuwa na uhitaji fulani na haufanikiwi.

Kwangu binafsi, napambana na kuwa na watoto wengi, na kama itawezekana huko mbeleni itabidi nitafute eneo la kijiji, angalau ekari kumi, bahati nzuri ardhi kijijini inauzwa bei nafuu; humo ndani niishi na vijana wangu pamoja na mifugo.

Lengo likiwa nikigeuka huku na kule naona vijukuu na watoto ili kupunguza upweke na msongo wa mawazo katika uzee wangu.

Je ,wewe unajiandaaje na maisha ya uzeeni?​
Kula vyako. Warithi hawana shukrani.
 
Yaan leo tu nilikua nawaza jambo hili naingia jf nakutana mada kama hii.Nimewaza sana vibanda vyangu vya mjini nitavipangisha vyote baada ya kumaliza kuvifanyia finishing.
Nataka niende kati ya mbeya ama Songwe ninunue shamba lenye miti tayari nifuge nikisubiri kifo
 
Back
Top Bottom