Wakuu habari
Kwa wale mnaofanya biashara zenu wenyewe ambao hamtegemei mshahara kutoka kwenye ajira za Serikali au private company..
Haya naomba mtuambie hapa, wewe na hiyo biashara yako unajilipa mshahara bei gani Kwa mwezi? Na unafanya biashara gani?
Tuambie Gross salary na net net salary unayo earn each monthly
Mimi na biashara ya boda na Uwinga kkoo, najilipa laki sita, hii net salary.
(KWA MAONI YANGU)
Jinsi ya kujua jinsi ya kujilipa kwenye biashara ni jambo mtambuka, kwa sababu kwenye biashara kuna watu wa aina mbili.
1. Aliyejiajiri: Huyu ni lazima awepo ofisini. Asipokuwepo, hakuna kitu kinafanyika. Mfano: Fundi cherehani.
2. Mjasiriamali: Huyu uwepo wake sio lazima sana. Ana mfumo ambao unamsaidia jinsi ya kufanya kazi. Mfano: Fredy Vunjabei.
Sasa linapokuja swala la kujilipa, inategemea sana upo kundi gani.
1. Kwa aliyejiajiri hana utofauti mkubwa sana na mwajiriwa, hii ni kwa sababu wote wanauza muda wao. Hivyo kipimo cha jinsi ya kujilipa kwa aliyejiajiri kinatakiwa kishabiane na cha mwajiriwa (Hapa unalinganisha biashara unayofanya na scale za mishahara ya wafanyakazi wanaofanya kazi kama uliyojiajiri).
2. Kwa mjasiriamali huyu uwepo wake ofisini sio wa lazima sana katika biashara yake, hivyo hana kipimo maalumu. Kipimo cha kujilipa kinabadilika badilika kutegemeana na mazingira ya biashara. Mfano:- kuna mwezi anaweza asijilipe kabisa kwa sababu fedha iliyopatikana haitoshelezi kujilipa yeye, kuwalipa wafanyakazi na kurudisha mikopo . Ila kuna miezi ambayo kwa mwezi atapata 4x baada ya kutoa matumizi yote. Kumbuka huyu mtu anatumia team kufanya kazi na sio yeye kuhusika moja kwa moja. Kwa kipindi ambacho yuko kwenye loss, atatafuta namna nyingine ya kusurvive.
Hivyo ni ngumu sana kupata jibu la moja kwa moja la kujua ni kiasi gani mfanyabiashara anajilipa kila mwezi, hii ni kutokana na utofauti wa wafanyabiashara kama nilivyoeleza hapo juu.
N.B
Kama kuna sehemu nimekosea naomba nirekebishwe