Unajisifu una hela lakini umetelekeza mtoto

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
đź“–Mhadhara wa 25:

Mwanaume unaanzaje kukimbia majukumu ya kulea mtoto au watoto wako. Mwanaume rijali aliyekamilika hakimbii majukumu ya kulea damu yake, anaweza kumkimbia mwanamke aliyezaa nae lakini kamwe hakimbii jukumu la kumlea mtoto.

Iwapo mwanaume rijali atamkimbia mwanamke aliyezaa nae, atahakikisha anafanya jambo kati ya mambo haya mawili; ama kumchukua mtoto wake au kutengeneza mazingira ambayo yatamsaidia mtoto kupata huduma ya baba. Kamwe mwanaume rijali hata kama ni masikini hawezi kukaa miaka pasipo kujua mtoto wake ana hali gani huko aliko hata kama mama wa mtoto ana ajira inayomwingizia kipato.

Kuwa rijali sio tu kumpandisha jongoo mtungini, bali pia kusimama vyema katika majukumu yako. Kama umekataa jukumu lako la msingi wewe sio mwanaume uliyekamilika na ulipaswa kwenda kumsalimia P-Diddy kabla hajakamatwa.

Huku mjini kuna wanaume ambao wanajisifu wana pesa lakini nyuma ya pazia wametelekeza watoto wao wa kuwazaa. Miaka nenda rudi hawajui watoto wao wanakula nini, wanalishwa na nani, afya zao zikoje, wala hawajui watoto wanalala wapi. Wametelekeza watoto lakini jumapili wanajaza makanisa na kuahidi kutoa michango mikubwa makanisani, huku wengine ni watu wa swala tano.

Haiwezekani mwanao wa damu anatembea peku mtaani ilhali kule Kariakoo kuna Yebo hadi za shilingi elfu mbili, lakini wewe umevaa raba za gharama halafu hutaki kwenda kumsalimia P-Diddy. Are you serious?

MWANAUME KAMILI:

Mwanaume kamili hawezi kukaa zaidi ya wiki moja bila kujua hali ya mtoto au watoto wake. Kama itatokea hivyo basi atakuwa amesafiri amekwenda sehemu ambayo hakuna mawasiliano ya simu ya moja kwa moja, lakini kabla ya kusafiri naamini alihakikisha mtoto au watoto wake wanahemea wapi.

Kama wewe ni mwanaume unaona maisha ni magumu, je vipi kwa mtoto wako uliyemtelekeza atayaonaje maisha? - Ukiwa unatafuta hela halafu mwanao anakula jasho lako ni jambo linaloleta furaha sana.

Right Marker
Sept 30, 2024
Dar es salaam.
 
[emoji433]Mhadhara wa 25:

Tatizo ni hao wanawake wanao fanya watoto kua kitega uchumi kwao, mpaka baba unakereka na kuachana na ujinga wao.
 
Back
Top Bottom