Sina hakika sana mantiki ya hoja zako zimelalia wapi, ila nionavyo mimi hakuna haja ya kuunda kamati ya kujadili rangi za bendera ya taifa. Ni kweli viyu vingi vinabadilika kuendana na wakati na mabadiliko ktk maisha yetu ya kila siku, ila hili la kubadilisha rangi za bendera sioni kama linawezekana vipi.
Katiba inaweza kuandikwa upya ili kukidhi mahitaji ya wakati fulani. Hii inaewezekana kwa kuwa ndiyo dira na mwongonzo wa maisha yetu ya kila siku. Kuna mapugufu yanaonekana, yanarekebishwa then tunasonga mbele.
Nahisi huja ya kutaka kuwa na vazi la taifa ni moja ya mbinu za kuturudisha kule tulipopotea na kuacha maadili yetu kama taifa hasa katika nyanja ya mavazi. Ni ukweli usiopingika kuwa siku hizi mtu aweza kuvaa nguo yoyote tu aipendayo bila kujali jamii inayomzunguka ina mtazamo gani juu ya vazi hilo.
Kibinafsi mimi naunga mkono kuwepo na vazi rasmi kitaifa. Lakini pamoja na hilo, bado napinga matumizi makubwa ya rasilimali ktk mchakato wa kubuni na kufikia kupatikana kwa vazi hili. Ni ukweli usiopingika kwamba pamoja na kuwepo kwa vazi hilo la kitaifa, bado tutaendelea kuona vivazi vyetu hivi vya machukizo mitaani wamevaa kaka na dada zetu.
Nikirudi kwenye mada yetu, kiukweli sioni tatizo la rangi za bendera yetu. Tukitaka kufuatilia dhima ya rangi zile, mimi naona ni ileile.
Weusi ni rangi yetu Waafrika na itabaki kuwa hivyo milele. Kama tuna shaka na hili ni vema mtu mmoja mmoja akiamua aende dukani anunue rangi ajibadilishe ila rangi ya bendera yetu ibaki vile vile.
Na ikiwa tatizo ni kwamba tume haikuundwa wakati wa kubuni rangi zile, inawezekana ni mapungufu kweli. Lakini, je hayo mapungufu yana madhara gani kwetu? Je, zile rangi zina mapungufu gani ya kimantiki hadi tuhitaji kufanya marekebisho?
Zile rangi 3 zilizobakia mimi sioni shida. Ikiwa haziwakilishi hizo rasilimali hilo ni tatizo. Ila ikiwa haturidhiki na mgawanyo wa rasilimali hizo, hiki ni kitu tofauti. Rangi kama rangi hazina la kufanya ktk hili, kwa maana nyingine, hatupaswi kulaumu rangi ya bendera yetu. Ni lazima tutafute kitu kingine cha kutupia lawama lakini sio rangi za bendera. Mimi naamini maliasili zote zilizowakilishwa kwenye rangi za bendera zote zipo. Ingawa hakukuwa na tume maalum ya kubuni rangi za bendera yetu, lakini hata hivyo tunapaswa kumsifu huyo mwenzetu aliyeweza kubuni hiki kitu, alikuwa ni mtu makini.
Nionanyo mimi, kama kuna mtu anayetakiwa kulaumiwa kutokana na kushindwa kunufaika ipasavyo na hizi rasilimali zetu, ni wewe na mimi. Tumeweka wasimamizi wa hizi rasilimali zetu then wameshindwa kuzisimamia vizuri na sisi tumekaa kimya. Tunapaswa kulaumiwa sisi wenyewe. Tumeshindwa kuweka watu makini wa kutuongoza vizuri, badala yake tunaanza kuhoji uhalali wa rangi za bendera ya taifa. Haya ni mapungufu.
Kwa hilo la jina la taifa kwa sasa sina comment. Ngoja nikalitafakari kwanza huenda nikarudi baadaye.