Unajua kuwa Tanzania Haina Admiral wa Navy?

Navy army ....kwa Tanzania ndio tunakua taratibu maana uwanha mpana sana wenye tech kubwa sana....muda utaongea nasi tunaenda taratibu....asante china kutufumbua uelewa kwenye navy kwa ujumla...na jeshi anga oia....plus urusi....
To correct you ni navy command, hatuna navy army
 
Sahihi. Hata Israel the highest military rank I mean Mkuu wa Majeshi ni Lieutenant General. Najaribu kuwaza CDF akikutana na yule wa Israel equivalent inakuwaje? Ufafanuzi tafadhali.
NATO sababu majeshi yao yana doctrines tofauti basi wao wana grades za STANAG na wanazitumia jeshi lolote duniani.
Kila cheo cha jeshi kinawekwa kwenye level, mfano North Korea wana doctrine tofauti sana na duniani kote, Urusi ina utofauti hasa kwenye Navy, Finland wana emphasis kwenye artillery hivyo si ajabu kukuta mkuu wao wa artillery and rocket forces ana cheo kikubwa kuliko wa nchi nyinginezo.

NATO mkanganyiko huu wanajua kuuweka sawa.
 
Wakipunguza vyeo watatawala kwa shida sana. Wanahitaji hivyo vyeo ili kuwapooza washiriki wao.
Tunahitaji overall review ya vyeo na output yake vs mishahara na marupulupu yake.

Tukiendelea hivi hatuta kwenda kwa ka nchi kadogo hivi.

Watawala weengi mishahara na huduma za bure kwao nyiingi, tutafika wapi, mwisho tutaanza kukopa kuwalipa mishahara na huduma za bure wapatazo kwa jasho letu.
 
Mkuu mi ningependa kujua kwanini CoS wengi hawaji kuwa majenerali mfano Mzuri ni Yule aliyeongoza mapambano ya M23 nilimtegemea Sana lakini hakuwa then huyo aliyetoka Yaani Lt Gen Mkingule Naye hajawa pia kwanini inakuwa hivyo
 
Unalalamika Rais kuvisha nishani Halafu unaongelea hela sasa nishani na hela Vina mahusiano Gani?
 
Jinsi tech. Inavyosonga,mambo ya drones na mengine mengi,naiona infantry ikiishilia mbali
Infantry haiwezi kufa hata siku moja sema tu utendaji kimbinu zile formation za kimapigano hazitakuwa Kama zamani ila infantry ndio huwa tegemeo kuliko hata anga na majini ambako sahizi ni rahisi kudetect kuwa adui anakuingilia
 
Sawa ndiyo mipango yetu; Lakini ulikuwa unajua kuwa Navy ya Tanzania haina Admiral?
Kama mtaalam uliyepitia huko, unaweza pia kutuambia upungufu na hasara ya kutokuwa na huyo admiral. Pia utoe majibu kama inawezekana kwamba tuna vifaa vya kutosha japo ninadhani hizi zaweza kuwa Siri za kijeshi.
 
Nafikiri ukubwa wa jeshi la majini na wingi wa meli za kivita ndio zinafanya apatikane Admiral
Sasa sijui tuna meli ngapi za jeshi na tunaenda mpaka mipaka ya wapi na meli zetu
 
Siasa kuziingiza kwenye majeshi hii πŸ‘† ndio hasara yake ss. Yan army uilinganishe na Navy,

Tufanye kazi kwa ukweli na uwazi . angalia Israel Hawana 4 🌟 general army, unafikiri ni kwani, jeshi na usalama wa inchi Yao, hauendeshwi kwa utashi wa akili za menyekiti.

Jeshi la Israel Lina jukumu 1 TU nalo ni kulinda maslahi ya Israel basi na sio kulinda wanasiasa.

Ss huku tuna ngangana kuteua macdf huku wakiwa tayari wana magonjwa kisukari , presha
 
Usilichukulie poa jeshi la wananchi, just because hawajionyeshi uko nje, haimaanishi wamestop ku develop. You have no idea nini kinaendelea ndani ya tpdf kwa sasa. Sisemi wako so advanced sana but wanaenda kwa pace yao, no advirtisement and just because ya technological advancement basi askari ana abandon basic principle za kuwa askari?

Look at ukraine? Bila kuwa na strong infantry guys ambao wata cover trenches meter by meter hata upewe robot 1M, huto succeseed.

Infantry ndio jeshi mama, uti wa mgongo wa jeshi lolote duniani. Sector zingine kama airforce na navy ni support brigades

Lakini kingine kuna budgetary issue, unakuwaje na advanced army wakati tu budgetary wise mnajibana?
Una expand military kapability on what budget?
 
Mkuu mi ningependa kujua kwanini CoS wengi hawaji kuwa majenerali mfano Mzuri ni Yule aliyeongoza mapambano ya M23 nilimtegemea Sana lakini hakuwa then huyo aliyetoka Yaani Lt Gen Mkingule Naye hajawa pia kwanini inakuwa hivyo
Inaonekana serikali haipendi kutabirika succession plan ya JWTZ na TISS. Hii ni kuondoa michezo ya kuwania vyeo na kutengeneza team. CoS anajua anamhitaji CDF, bila CDF CoS hamna na maofisa kadhaa wanabadilika. They are more likely kupendelea status quo iliyopo iendelee kuliko ibadilike wakati hawana uhakika na yajayo kama yatafurahisha.

Mara nyingi CoS anayeisha muda wake anakuwa amefika au anakaribia umri wa kustaafu jeshini, ukimfanya awe CDF anazidi sana umri wa utumishi.

Huyo aliyeongoza mapambano na M23 nadhani alistaafu kwa kuchelewa, hata kwenye mahojiano yake alikuwa anaoneakana.
 
Mbona inasemekana yeye mwenyewe ndio aliomba kustaafu
 
Kama mtaalam uliyepitia huko, unaweza pia kutuambia upungufu na hasara ya kutokuwa na huyo admiral. Pia utoe majibu kama inawezekana kwamba tuna vifaa vya kutosha japo ninadhani hizi zaweza kuwa Siri za kijeshi.
Umefurika bure. Post haisemi kuwa kuna faida au hasara bali ni kuonyesha kuwa Tanzania hatuna Admiral. Mbona Israel yenye jeshi active sana nayo haina hata rear admiral? Kwani hiyo ni shida?
 
Mkuu mi ningependa kujua kwanini CoS wengi hawaji kuwa majenerali mfano Mzuri ni Yule aliyeongoza mapambano ya M23 nilimtegemea Sana lakini hakuwa then huyo aliyetoka Yaani Lt Gen Mkingule Naye hajawa pia kwanini inakuwa hivyo
Davies Mwamnyange alikuwa CoS ndipo akawa General na CDF, hata Venance Mabeyo naye alianza kama CoS ndipo akawa General na CDF. General Mwakiborwa alifikia kuwa CoS wakati umri umeshaenda sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…