Kama wewe ni mwanajeshi ama ni mtu tu unayeelewa mambo ya kijeshi, basi kuna kitu haukielewi sawa sawa.
Kabla ya mabadiliko ya mfumo wa vyeo vya jeshi la Navy miaka ya karibuni, kamandi za majeshi yote zilitumia vyeo vyenye kufanana, yaani vya Army.
Lakini vyeo vya Navy vilipobadilishwa, kuna barua nadhifu ilitolewa kufafanua kila cheo kulinganishwa na vyeo vya Army/Air force.
Kwa hiyo kila cheo cha afisa ama askari wa Navy kina ulinganifu wa cheo cha afisa ama askari wa Army/Air force na equivalent rank huwa haizidi cheo inacholingana nacho.
Chukulia mnapokutanishwa majeshi ya mataifa mbali mbali cha kwanza huwa ni kutafsiri equivalent ranks, yaani cheo hiki ni sawa na cheo kipi kwa jeshi jingine.
Tukija kwenye upandishwaji wa vyeo kutofikia cheo flani, hilo lipo wazi, vyeo vya jeshi hufuata muundo.
Hata mkuu wa majeshi aliyepo sasa, cheo alichonacho hakimstahili, alistahili cheo cha chini yake, kwa wajuzi wa mambo tunaona kama anavaa cheo cha kisiasa.
Jeshi kimuundo, ukishatoka Brigade, kuna Division, baada ya divisheni kuna corps na baada ya hapo kuna Army.
Uhalali wa vyeo kimuundo upo hivii: Brigade inaongozwa na Brigadier general, Division inaongozwa na major general, corp inaongozwa na Lutenant general na Army inaongozwa na General.
Hizi command za majeshi zilizopo Tz zina hadhi ya Divisions na viongozi wake ni major generals ambapo ni sawa.
Baada ya hapo kimuundo inafuata Corp ambapo jeshi letu ndiyo limekomea, na cheo kinachostahili ni Lutenant general na siyo General kama tukifuata muundo.
Kwa hiyo Cdf wa Jwtz alitakiwa awe Lt general.