Tofauti Ya 5; MWANAUME anapenda NGONO, Mwanamke anapenda MAPENZI.
Mwanaume na Mwanamke wamesukwa tofauti Sana katika Eneo la tendo la ndoa.
( man and Woman is different Wired)....!
Tendo la ndoa katika ndoa ndio Mhimili wa ndoa, Chakula Cha ndoa, Unyumba n.k
Lina Majina Mengi, Tendo la ndoa likikosekana NDOA inageuka inakuwa NDOANO.
Moja Ya sababu Ya Mwanaume inamfanya AOE ni kutaka kutimiziwa haja zake za kimwili ( Sexual desire).
ndio Maana Mwanaume akinyimwa anakuwa Kama MGONJWA, anaweza hata Kubaka, anakuwa chizi si chizi ( au nadanganya ndugu zangu?😅)
unaambiwa kisaikolojia " Sehemu Kubwa Ya ubongo wa Mwanaume unawaza Sana tendo hili"
Tendo hili ni NEEMA Sana likifanyika kwenye ndoa,nje Ya ndoa ni NOMA tupu.
“A man want sex to Feel Loved, a woman need Affection to Feel Loved”
Yaani "Mwanaume anataka ngono ili ajisikie KUPENDWA, mwanamke anahitaji MAPENZI ili ajisikie KUPENDWA"
hii ni sawa na Kusema "Mwanaume akikosa ngono kwa Mkewe anajisikia HAPENDWI, vile vile Mwanamke akikosa MAPENZI Anajisikia HAPENDWI"
Mwanaume na ngono kwa Mkewe ni Kama SAMAKI na MAJI, labda awe na MATATIZO Ya Kiafya au amerithi tabia za KIKE 🤭
LAKINI Mwanaume kuwa Makini SAMAKI na MAJI huwa marafiki Sana,lakini samaki siku amekamatwa na mvuvi, maji hutumika KUMPIKA rafiki Yake ( sijui Kama unaelewa?)
Tendo la Ndoa huondoa kisirani kwa wanandoa, Penzi linarudi UPYA, kajaribu na MKEO au MUMEO uone.
Ila Mkiendelea Kuwekeana Ratiba na Kunyimana mtakinahiana ( 1wakorintho 7:5)
Mwanamke kinachotangulia kwake ni MAPENZI( affection) so Kuna tofauti Kati Ya ngono na MAPENZI.
wanaume wengi wanajua MAPENZI Ila wengi zaidi hawajui MAPENZI.
Mwanamke ni kiumbe wa Hisia Sana( an emotional feeler) hawezi kutoa mapenzi ikiwa hisia zake hazijafikiwa.
___________