Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeibuka na ushindi katika mechi zake mbili za kirafiki, kwenye michuano ya CECAFA 3 Nations Tournament ikiwa ni maandalizi ya kuelekea fainali za Michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani ya Nchi (CHAN) 2024 zinazotarajiwa kuanza Agosti 2.
Tanzania ilianza vyema kwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda, Jumanne, Julai 22, 2025 kupitia bao la Iddi Suleimani (Nado) dakika ya 14, kabla ya kushinda 2-1 dhidi ya Senegal kwa mabao ya Abdul Suleiman (Sopu) na Ibrahim Hamad (Bacca).
Soma, Pia: Tanzania kufungua Michuano ya CAF CHAN 2024, Fainali kupigwa Kenya
Katika michezo mingine, Uganda iliifunga Senegal 2-1, Julai 24,2025 mabao yakifungwa na Arnold Odong na Patrick Kakande, huku Senegal ikipata bao la kufutia machozi kupitia Serigne Moctar Koita.
Bingwa mtetezi wa michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)
Senegal amepoteza mechi zote mbili. Senegal walitwaa ubingwa wa CHAN 2023 baada ya kuifunga Algeria kwenye fainali iliyofanyika nchini Algeria. Katika michuano ya CHAN 2024, Senegal iko Kundi D pamoja na timu za Nigeria, Sudan, na Congo
Taifa Stars itacheza na Burkina Faso katika mechi ya ufunguzi ya mashindano ya CHAN 2024, itakayofanyika Agosti 2, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam saa 2:00 usiku.