Unakubaliana na Boateng kuhusu Ronaldinho?

Mimi mwenyewe mpaka sasa sijawahi kumwona fundi wa mpira wa kariba ya Ronaldinho mpaka leo hii!!
 

Hivi wewe mbona unajitia Aibu??? Ungelikaa Kimya Basi Ungelificha Udhaifu Wako Wa Kutokuwa na Kumbukumbu Za Wachezaji Katika Huu Ulimwengu Wa Soka!

List Hiyo uliyoiweka Labda uwe unatafuna Bange Mbichi ndiyo utaweza Kuiandika..

Wacha Kumfananisha Fundi Gaucho na Vitu Vya Kijinga..
 
Wanaobishana na Boateng, je, wana maoni gani kuhusu takwimu hizi (siyo za Twaweza):

"Brazil forward Ronaldinho was named as World Player of the Decade by prestigious British magazine World Soccer ... Ronaldinho won the accolade based on the votes cast by readers in the 10 annual votes between 2000 and 2009 being converted into points" - Ronaldinho named player of the decade
 
Hapana mkuu umemdisgred sana Dihno kwa kumlinganisha na hao uliowataja. Kwa skills hakuna aliyewahi kumfikia dinho. Kina Juan Requelme, pablo Aimar, Ariel Otega, Redondo, na wengine wa aina hiyo ni wa kulinganishwa na zizzou. Dinho ni habari nyingine.
 
Ashley Cole 1994 WC?
 
Yuko sahihi kwani Pele na Maradona hajacheza nao. Enzi ya Pele, Boateng alikuwa bado hajazaliwa na enzi za Maradona, Boateng alikuwa mtoto. Sawa na baadhi ya wachangiaji wengi tu humu hawakumuona Pele akiwanyanyasa mabeki tena wakati huo sheria za makosa hazikuwa ngumu kama sasa. Wakati ule timu ya taifa ya Uruguay weeee acha tu.
 
Gaucho yuko vizuri sana

Lakini tunamsahau kaka yao JJ okocha
Huyu MTU nihatari sana

DUNIA haimzungumzii kwakua tu ametoka bara LA africa

Ila miongoni mwa wafalme wampira huyu jamaa anajua
 
Kwa mara ya kwanza ninamwona Ronaldinho ilikuwa ni 1999, Fifa World Cup U-20 akiitwa Ronaldo, mashindano yalifanyikia Nigeria, na Brazil ndo walikuwa mabingwa.

Kuna rafiki yangu mmoja akaniambia, huyu atakuwa mchezaji bora duniani (wakati huo akiitwa Ronaldo Mdogo), baada ya hapo tukamwona tena kwenye Olympics za mwaka 2000 ambapo walitolewa na Cameroon robo fainali huku tayari anaitwa Ronaldinho badala ya Ronaldo (jezi namba 7) akiwasawazishia Brazil goli dakika ya 94 (majeruhi) kwa faulo.

Baada ya hapo kila tukikumbushana na rafiki yangu yule anasema yeye ndiye aliyegundua kile kipaji eti.

Ronaldinho ni habari nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…