Ebwana baada ya mabishano ya muda mrefu humu ndani ikabidi nimtafute muhusika mwenyewe kuweza kupata baadhi ya taarifa na kujua lipi ni kweli na lipi sio kweli mana wadau wameongea mengi sana wanayoyajua....
View attachment 758774View attachment 758775
Kwenye maongezi Pinna anasema Kikosi kilianza harakati zake miaka ya 97-98 huko block 41 Kinondoni, lengo la kundi ndio kama hivyo ilikua kufanya music wa hiphop tena ngumu tu na malengo yao yalitimia.....
Kuhusu mabeef na fujo za kipingi kile jamaa hakua tayari kuongelea sana kwani alikua anasisutizia tuyaache hayo ya kitambo na yalishapita sasa hivi ameshakua mtu mzima, lakini nilikomaa anielezee kidogo kuhusu nyimbo yake ya beef na kumpiga Dudu baya....
"Inshort nyimbo ya beef yaliyoongelewa mule ndani ni ukweli asilimia 97 na Dudu nilimdunda kweli akakimbia japo yeye alikua anakataa ila ni zamani kipindi damu inachemka, J na UKIMWI ilikua ni vibe tu ila ilisemekana kweli alipita na demu mwenye mdudu.....
Pia kuhusu kukimbiza maaskari ni kweli kuna wanga walijichanga wakakodi mapoti satudake lakini nilinguruma na hatimae walikimbia na pingu zao viunoni ni kitambi lakini".....
Pia nilimuuliza kuhusu beef lao kubwa na N2N ila alisema lile halikua beef lao kubwa kuwahi kutokea ila lilionekana kubwa kutokana na kwamba N2N nao walikua wanafanya muziki kwahiyo walikua wanafahamika lakini kuna makubwa walishafanya mitaani....
Kuhusu kumchangia Bou alikataa kua hawakumchangia Kikosi kizima ila muhusika alitoa sababu tu za kufanya asionekane mnyonge mbele ya jamii....
Pia kwakusisitiza hilo aliniambia kwa kipindi kile anaishi yale maisha hakuna mtu yeyote aliekua anamtisha wala kumuhofia katika mambo ya ubabe wa hapa na pale na kila mtu alikua analijua hilo na walikua wanamuheshimu na kumuogopa mno that why ata collabo hakua anafanya kutokana na kwamba walikua wanahofia ata kumface kuomba ushirikiano.....
Pia nilimuuliza jinsi ya kupita Wimbo wao ambao wadau tumeutafuta sana bila mafanikio 'Nyimbo tosha' ft belle 9 aliniahidi kunitumia lakini mpaka leo hajafanya hivyo...
Kwasasa anajihusisha na harakati kama vile kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, Siasa anafanya na kaahidi ataendelea kutafuta nafasi ya kuingia mjengoni, pia anakampuni yake ya ulinzi.....