Unakumbuka mwaka 1994 Wazanzibar walivyokasirika Rais wa Zanzibar kuondolewa kuwa Makamu wa Rais wa Muungano?

Watu hawataacha kumchagua Rais wa jamhuri hata kama hawamjui mgombea mwenza wake. So mgombea mwenza anabebwa na mgombea... Huwezi kujustify uhalali wake...
 
Umakamu wa Mgombea mwenza ni halua, ambapo si rahisi tena kwa mgombea Urais wa JMT Kutokea Zanzibar.
 
Kwani ilikuwaje baada ya kukasirika? Wewe imekusaidia nini baada ya kutukumbusha yaliyotokea ?. Tushauri tufanyeje leo wewe uliekumbuka.
 
Rais wa Zanzibar alikua ni makamu wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa kwanza alikua ni yule mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano.
 
Huyo babu yenu hakuna alichokifanya cha maana na hatakumbukwa....ameondoka na kuiacha zanzibar ikiendelea na mfumo huo huo wa kuiba kura.
 
Sintuambie tu mbona mnazunguka zunguka tu ndio maana Wakenya tunaambiwa tunaropoka sana Aaa...!
 
Duuu bila kusoma comment nisingeelewa huu uzi. Japo hata sasa Makamu anatoka Zanzibar na ikitokea kwa namna yoyote Rais aliyepo akashindwa kutekeleza majukumu yake bas huyo Mzanzibar ndio atachukua usukani, labda kwenye hili ni kwamba huyo atakua amepigiwa kura na watanganganyika na pia atakua kutoka mbogamboga.
 
Wakati Karume anafariki cheo cha Makamu wa pili cha Kawawa kilishafutwa miezi miwili kabla na Kawawa alishakuwa Waziri Mkuu.

 
Wakati Karume anafariki choe cha makamu wa pili cha Kawawa kilishafutwa miezi miwili kabla na Kawawa alishakuwa Waziri Mkuu.
Ninajua kuwa baada ya mauaji ya Karume mwaka 1972, Nyerere aliunda baraza jipya la mawaziri na katika reshuffle ile ndipo nafasi ya makamu wa pili wa Rais ilipoondolewa na kuundwa kwa nafasi ya waziri mkuu. Nisahihishe kama una taarifa zaidi ya hapo.
 
Inawaka waka mama...inapendeza chattle ai mama, tano tena ! Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kichuguu,

Reshufle unayoisema ni kweli ilikuwepo lakini haihusiani na ninachokisema.

Kawawa ameapishwa kuwa Waziri Mkuu mnamo Februari 18, 1972 yaani takribani miezi miwili kabla ya kifo cha Karume, kwani Karume ameuawa Aprili 7, 1972.

Ninajua kuwa baada ya mauaji ya Karume mwaka 1972, Nyerere aliunda baraza jipya la mawaziri na katika reshuffle ile ndipo nafasi ya makamu wa pili wa rais ilipoondolewa na kuundwa kwa nafasi ya waziri mkuu. Nisahihishe kama una taarifa zaidi ya hapo.
 
Hili bandiko ni kama linatanua uwanja wa fikra wa rejea ya mambo kadha wa kadha yanayoendelea
 
Kama Rais wa Zanzibar akiwa moja kwa moja Makamu wa Rais wa Jamhuri, itakuwaje kama Rais wa Jamhuri anatoka Zanzibar kama ilivyokuwa kwa Ali Hassan Mwinyi? Kwa sasa hakuna tatizo kwa kuwa Mgombea Mwenza lazima atoke upande mwingine: Mgombea urais akitoka Bara, Makamu lazima atoke Zanzibar. Hivi sasa ni Rais Magufuli wa Bara na Makamu ni Samia Suluhu wa Zanzibar. Makamu wa Rais Mwinyi (kutoka Zanzibar) alikuwa Malecela wa kutoka Bara. Hakuna tatizo.
 
Nyerere alifahamu kua Rais ni binadamu ana nyama na damu.
 
Hivyo iko siku tutaona ukweli wa alichosema Nyerere. Iko siku Rais wa muungano ataweza kupata tatizo ikabidi makamu wa Rais achukue Urais ndipo wazanzibari wenye akili ngumu waelewe.
[emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…