Nyerere na Bomani waliku right kabisa. Katiba ya tanzania haijawahi kuwa wazi kuhusu kupokeana madaraka wakati Rais akifa; kwa mfano wakati Karume alipofariki, Makamu wa wa pili wa Rais wakati huo alikuwa Kawawa, lakini yeye hakuwa promoted kuwa makamu wa kwanza wa Rais, badala yake aliletwa Jumbe ambaye alikuwa waziri wa nchi kwenye ofisi ya Makamu wa kwanza Rais wakati huo.
Halafu Nyerere alipostaafu, Mwinyi hakuwa automatic choice bali kulikuwa kampeini kubwa sana ya "huyu ni mwenzetu" iliyofanywa na Nyerere ili kumkubali Mwinyi kama mrithi wa Nyerere, kulikuwa na uwezekano mkubwa sana wa watu wengine kuiwania nafasi hiyo.
Bado kulikuwa na woga wa "Treason Act 1351" kuhusu kuongelea uwezekano wa rais kufia madarakani.