Wakati nipo darasa la 6, kuna mwalim mpya wa kike alihamia pale shuleni kwetu kwa ajili ya kutufundisha somo la sayansi. Alikuwa mweupe, bado binti tu. Wanafunzi tulikuwa tunampenda sana maana hakuwa mkali sana.
Sasa siku moja tupo class nikawaambia jamaa zangu wawili niliokuwa nakaa nao kwenye dawati moja, kuwa nitamuandikia barua yule ticha. Alaf kama masihara niliiandika kweli ile barua japo sikuwa na dhamira ya kumpelekea.
Nikaiweka kwenye mfuko wa nyuma wa kaptura alaf nikakausha. Nikaisahau.
Sasa kesho yake yule ticha baada ya kumaliza kipindi chake, akawa karudi ofisini, akasahau chaki zake darasani. Nakumbuka kuna ticha mwingine aliniita ofisini, wakat natoka yule madam akaniagiza nimchukulie chaki zake nilete ofisini.
Nilimbebea chaki zake then nikapitia toilet kwanza. Zile chaki nikaziweka kwenye mfuko wa kaptura pia. Sasa wakati nazitoa nimpe, kumbe na ile barua ikaanguka, ila sikujua. Inavyoonekana ticha aliiokota na kuisoma. [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Nikawa nashangaa tokea siku hiyo ticha kila akiniona anacheka tu, au akija class lazima niulizwe maswali muda wa kipindi chake, mara utaskia akisema "we mtu mzima njoo ufute ubao" [emoji28][emoji28][emoji28].
Akaanza kufatilia maendeleo yangu as if tunafahamiana.
Kuna siku baada ya kipindi chake akaniambia nimbebee madaftari tuliyokusanya darasani. Nilivyofika ofisini akaniambia "Dogo soma kwanza, mapenzi hayatokufikisha popote"
Nikajiuliza why aniambie vile? Hapo nikaikumbuka barua yangu. Nikaitafuta ila sikuiona.
Last year katika purukushani za mjini, nikakutana tena na yule madam. Uzuri mimi ndio nilikuwa wa kwanza kumuona na kumtambua. Nikabadili njia fasta.
Kumbe aliniona, na alinijua (maana tokea std 6 hadi namaliza std 7 tulijenga ukaribu sana kama mwalim na mwanafunzi). Nipo kituoni nasubiria usafiri, nashangaa mtu ananiuliza "Dogo upo kwenye kusaka hela au bado unaendekeza mapenzi?. Alafu mbona unanikwepa, au hutaki jibu la barua yako?" [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Sent using
Jamii Forums mobile app