Unakumbuka nini enzi za kuandikiana barua za mapenzi?

Ata Mimi napenda Sana penpalling ni pm nikupe my address tuwe tunaandikiana barua pia facebook kuna magroup mengi ya penpals unaweza kupata marafiki wa kuandikiana barua kutoka duniani kote
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Noma sana, nishawahi kupigwa nusu nife na mwalimu kwa sababu ya hii mambo
 
"nikinywa maji nakuona kwenye glass"

huu ulikua zaidi ya uongo bt kwa kua mapenzi ni upofu kamwe uongo huu hawakuwahi ubaini.
 
Wakati nipo darasa la 6, kuna mwalim mpya wa kike alihamia pale shuleni kwetu kwa ajili ya kutufundisha somo la sayansi. Alikuwa mweupe, bado binti tu. Wanafunzi tulikuwa tunampenda sana maana hakuwa mkali sana.

Sasa siku moja tupo class nikawaambia jamaa zangu wawili niliokuwa nakaa nao kwenye dawati moja, kuwa nitamuandikia barua yule ticha. Alaf kama masihara niliiandika kweli ile barua japo sikuwa na dhamira ya kumpelekea.

Nikaiweka kwenye mfuko wa nyuma wa kaptura alaf nikakausha. Nikaisahau.

Sasa kesho yake yule ticha baada ya kumaliza kipindi chake, akawa karudi ofisini, akasahau chaki zake darasani. Nakumbuka kuna ticha mwingine aliniita ofisini, wakat natoka yule madam akaniagiza nimchukulie chaki zake nilete ofisini.

Nilimbebea chaki zake then nikapitia toilet kwanza. Zile chaki nikaziweka kwenye mfuko wa kaptura pia. Sasa wakati nazitoa nimpe, kumbe na ile barua ikaanguka, ila sikujua. Inavyoonekana ticha aliiokota na kuisoma. [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Nikawa nashangaa tokea siku hiyo ticha kila akiniona anacheka tu, au akija class lazima niulizwe maswali muda wa kipindi chake, mara utaskia akisema "we mtu mzima njoo ufute ubao" [emoji28][emoji28][emoji28].

Akaanza kufatilia maendeleo yangu as if tunafahamiana.

Kuna siku baada ya kipindi chake akaniambia nimbebee madaftari tuliyokusanya darasani. Nilivyofika ofisini akaniambia "Dogo soma kwanza, mapenzi hayatokufikisha popote"

Nikajiuliza why aniambie vile? Hapo nikaikumbuka barua yangu. Nikaitafuta ila sikuiona.

Last year katika purukushani za mjini, nikakutana tena na yule madam. Uzuri mimi ndio nilikuwa wa kwanza kumuona na kumtambua. Nikabadili njia fasta.

Kumbe aliniona, na alinijua (maana tokea std 6 hadi namaliza std 7 tulijenga ukaribu sana kama mwalim na mwanafunzi). Nipo kituoni nasubiria usafiri, nashangaa mtu ananiuliza "Dogo upo kwenye kusaka hela au bado unaendekeza mapenzi?. Alafu mbona unanikwepa, au hutaki jibu la barua yako?" [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂😂😂
 
😂😂
Aisee...imenifanya nimkumbuke J 🤣🤣 yeye wakati wa mtongozo hakuandika barua ila alimtuma Dada wa kazi..ingawa nilianza ona makeke yake nikimuazima daftari lazima nione nyuma ya jaradio kaandika "my love na vikopakopa kibaooo"🤣🤣🤣🤣 j bwana..na alivyotoa nyongo si bidada Nitake msemea kwa Mama 😂😂😂 hatareeee ..kaka wa watu uoga ukamjaa akaanza niomba msamaha..wakati kamoyo kalikuwa kanamkubali🤸🤸

Vibarua Sasa vikaanza kupamba moto alipokuwa boarding ..vimaneno vya mapenzi Mara sijui no one like you Kama psquare..nataka niwe na wewe milele Kama Ray c🤣🤣🤣🤣🤣 wapiiiiiii....!!!!...J alikuwa na mbwembwe Aisee.
 
Hahahahhaa, I love this. Hii sio tungo ni halisi. Ila ni mwalimu mzuri hakukuaibisha, mwingine asiyeelewa utoto ungetakani kuhama Shule.

Maana zile akili za utoto kuidondosha sishangai. Lakini kwann umkimbie mpaka sasa, yaani bado waona aibu tu?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] bas ulkua unajiona km RIHANNA vile lol
 
Haha ! Barua zilikuwa na taste yake bhn.
 
Mie nakumbuka mwaka flani kulikuwa na kamanzi mtaa wa pili nakahusudu kinyama ila mchizi domo zege.

Muda ukawa unaenda bila kukatokea ila siku moja napita chocho nikakuta kamebananishwa na Mwana boya tu anakapa Mistari, dah kidume ikani Pain Ikabidi nirudi Home kutafakari naiwahi Vipi meli Kabla haijazama, Mzee ndio nikatoka na wazo la BARUA..Nikaichora pale barua vizuriii full makopa na makiss humo tena nikamwambia nina bonge la muwa utakula mpaka usaze[emoji38]..

Afu nikatia mia mbili ndani yake kwenye bahasha nikamuita dogo lasi afanye service ya kunipelekea kwa Manzi ujumbe wangu matata..

Nikamwambia usipo fikisha mie naweza KUFA[emoji38]

Bwana wee dogo kumbe battery low asee si akazunguka kwa nyuma akaingia mlango wa uwani akampelekea bi mkubwa ile barua kwa madai ANAHOFIA BRAZA ANAWEZA AKAWA ANATAKA KUUZA NYUMBA KIMYA KIMYA WAO WATAISHI WAPI?..

Bi mkubwa akaifungua na kuanza kuisoma, nikasikiaaa weee mbwaaaaa njooo!!
Kwenda kule daaaah sikuamin macho yangu kuona bi mkubwa kashikilia kizibiti[emoji41]
 
Dogo alikuwa battery low kweli. Usnitch huwa unaanzia mapema kweli.
 
Aisee nilikuwa Advance.
Nyumbani alikuwa anakaa mtoto wa mamamkubwa. Nilimuelewa sana. Nilimwandikia barua ikanaswa dah. Ilikuwa fedheha
 
Ata Mimi napenda Sana penpalling ni pm nikupe my address tuwe tunaandikiana barua pia facebook kuna magroup mengi ya penpals unaweza kupata marafiki wa kuandikiana barua kutoka duniani kote
unaweza kunitajia hizo jina za group za fb
 
Ilikuwa ni lazima kumiliki kalamu yenye wino mwekundu mahsusi kwa ajili ya kuchorea vikopa kopa, vidamu damu na mshale ulotoboa kopa
Mtu mbadi utakuwa ndio wale wenye mwandiko mzuri ambaye anawaandikia wenzake barua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…