Umenikumbusha mbali sana, miaka ya 80 kuelekea 90 ndipo nilianza kulifuatilia sana hili jarida lililokuwa linatoka kila mwezi na hadithi za kusisimua sana akina Chepe, Kipepe, Sokomoko, Ndumilkuwili, Lodilofa, Madenge, Kifimbo Cheza, Dokta Pimbi, nakumbuka pia kulikuwa na kurasa kadhaa za vichekesho ilikuwa inaitwa cheka unenepe.
Ikifuatiwa na hadithi za wimbi la Kitintale unakutana na akina Obi, Linda, Zumo, Bosi Mayuyu liyekuwa anaishi kisiwani aliyekuwa anafanya biashara za madawa ya kulevya na magenge yake ya unyang'anyi, Ole aliyekuwa mtesaji wa huyo mdosi na mabaunsa wenzake. Riwaya za akina Eddy Genzel Mauaji ya Hayawani, Kizaizai na nyinginezo zilizokuwemo kwenye hilo jarida.