Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

Umenirudish mbali sana kimawazo,nimemkumbuka hadi marehemu mshua,alikuwa analipenda sana gazeti la sani,pia vita vya zena na betina,duh hahahaha
 
Kuna siku profesa ndumilakuwili hana kitu akawa ameenda kwenye phone booth a mpigie mshkaji wake bahati simu zikaingiliana akawa jamaa anatoa maelezo kuwa sheikh swalehe atakuja kuchukua fedha baada ya swala ya I jumaa jamaa akazidi kumuelekeza atakavyokuwa amevaa yaani hagal(kiremba)na kanzu pia huwa haachani na tasbihi.Alichofanya ndumila ni kwenda kuazima hivyo vivazi na akaenda kabla swala haijaisha waqt anatoka kuchukua fedha akakutana na mtu kavaa kama yeye akasema nadhani huyo ndio sheikh swalehe mwenyewe.
 
Wadau naona wengi mnasema lilikua la 86 mim nimezaliwa 90 lakini nakumbuka 99 hadi 2001 kulisoma hili gazeti maana wahusika wengi nawajua au kulikua na gazeti lingine likitumia hao wahusika kwa miaka ya karibuni ??????
 
Gazeti ili kama jamaa bado wapo wanaweza kurudi kitaa kwa kutengeneza cartoon za kucheza kwenye runinga na soko lipo.
 
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa hata neno NOMA lilitokea kwenye jarida la sani
 
Maneno kama vinibu,ulabu sisterduu nonino,mtu akiwa dhulumat aliitwa bob mazishi.
 
Dah me katuni tu ndo nilikuwa nasoma hamna habar niliyo kuwa naisoma...
 
mimi nayatafuta majina ya wachezaji wa bush star dah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…