DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Ndugu zangu, wakati mwingine tuache kulalamika kwa vitu ambavyo vipo wazi kabisa.
Mashabiki wa Yanga wanalalamikia TFF na Bodi ya Ligi kwa kuwapa Simba viporo vingi, wakilinganisha na viporo ambavyo Yanga ilikuwa navyo msimu wa 2022-23.
Kuna mambo kadhaa ambao wanajisahaulisha, mojawapo ni kuwa huo msimu wa 2022-23, Simba ilifika hatua ya robo fainali ya CAFCL wakati msimu huu wa 2024-25, Yanga imetolewa hatua ya makundi. Hii moja tu ni sababu tosha ambayo inaweza kutengeneza gape ya hata game 4 kutegemeana na mtiririko wa ratiba za mashindano mengine kama mashindano ya kufuzu AFCON na Kombe la Dunia.
Pia tukumbuke kwa msimu huu Simba iliahirishiwa mechi zake mbili kwa sababu ya ajali za barabarani iliyozipata timu pinzani, Dodoma Jiji na JKT. Hiyo tayari iliharibu ratiba na kutengeneza gape jingine.
Pia wakumbuke kwamba ratiba ya msimu huu iko tight ili ligi iishe mapema kupisha mashindano mengine kama ya CHAN. Msimu wa 2022-23 uliisha 08/06 wakati msimu wa 2024-25 ulipangwa uishe 24/05. Hapo kuna tofauti ya wiki zingine mbili. Kwa maana hiyo timu ambazo hazikuwa na mashindano ya kimataifa zilikuwa zinacheza mechi zaidi kwa muda mfupi kila nafasi ilipopatikana.
Kwa kumalizia, hatujasahau kuwa Yanga pia mechi zake zilikuwa zinaahirishwa sana tu msimu ule wa 2022-23 hata katika mazingira ambayo hayakuwa ya lazima mfano mechi ya kimataifa ipo Dar Jumamosi, halafu anaahirishiwa mechi zake za ligi wiki nzima wakati mechi yake iliyofuata ilikuwa iwe pia Dar na ingeweza kuchezwa hata Jumanne. Hatujasahau hilo. Hii iliisaidia sana Yanga kulinda afya ya wachezaji wake na pia kutowapa wapinzani nafasi ya kusoma current form ya wachezaji na timu.