...😀
umenichekesha sana VC,
huenda mimi nilikuwa na tabia mbaya ya kuchunguza sana, ngoja nikupe mifano nilipokuwa na tick sawa au hapana kwenye 'Questionnair' za warembo miaka hiyo ya 47! (siku hizi nimeokoka! 😱)...;
1. Nywele
-napendelea vimwana mwanywele, bahati mbaya wenye vipili pili walikuwapo pia. Iweje mabutu yanayosukiwa mawigi, au hizo extensions zisahauliwe mpaka ziote ukoko aka 'Dandruff'? mpaka leo hii si ajabu kukutana na mrembo wa nguvu lakini nywele 'phoooooaaah!'
2. Make up
- si utani, inabidi wengine wajivishe mask kuboresha reception zao, lakini hakuna sababu ya kulala bila kuondoa hizo eye lashes, sijui wanja au mascara... Ukiona mwanamke analala na hayo ujue anaficha mengi kuliko hayo uyaonayo...
3. Shingo,
-kama anasahau kusugua shingo yake mpaka ikaota ukoko, ujue kuna sehemu nyingine nyingi muhimu mwilini zimesahauliwa...
4. Kwapa
- yaani hakuna sababu inayotosheleza kwanini awe na nywele kwapani!
5. Kucha
- Angalau awe na kucha za kiasi basi, sio mikucha mireefu kiasi kwamba unajiuliza anawezaji kujisafisha kwenye tundu za 'kusikilizia'
6. Body smells
- kuna tofauti kati ya body smells na body Odour,...iwapo mwenyewe hajui tofauti kati ya kunuka na kunukia basi hata matumizi ya Perfume yatakuwa hayana maana...
baada ya hapo nilichunguza anapoishi;
- najua wengi wanakurupuka kusifia sebuleni na mapambo ya ukutani, binafsi sidanganyiki na hayo...
macho yangu yalifanya kazi ya ziada maeneo haya;
7. Toilet/bathroom
-ni mtumiaji wa maji au toilet paper pekee?
8. Jikoni kwake
- Kuna mmoja kopo hilo la bafuni/maliwatoni, ndilo alokuwa anachotea maji ya kupikia, kukogea na huenda hata kujisafishia!
9. Anavyoandaa vinywaji/chakula
- Ukiona Bi mrembo hajui hata maana ya glass towel, almuradi anakuletea bilauri ya maji ikitiririka maji nje na ndani, kama hilo halitoshi kwa mbali unasikia kashombo ka samaki ujue kuna kazi huko mbeleni!
kisha namalizia na;
9. Nguo zake hasa za ndani
- Kwenye malavi dovey, kuna wale ambao kufumba na kufungua unakuta weshavua kufuli zao, iwe baada ya kulazimishwa uizime taa, au baada ya kujifunika gubigubi...! waogopeni sana hao...
Enzi za u bachelor nilikuwa nafanya kazi ya ziada kuhakikisha naijua 'siri ya urembo' kwanini 'kufuli' ilikuwa inafichwa, na kweli... mara kadhaa nilikutana na binti wa nguvu lakini 'kufuli' dhooful hali!
Anyway, baraza la jumapili hili... kesho j'3 tukalijenge taifa 😀