tamimusalim
JF-Expert Member
- Jun 17, 2014
- 1,822
- 498
Ni kundi liliotikisa katika ulimwengu wa r&b uko marekani katikati mwa miaka ya tisini,kundi hili liliundwa na akina dada Lisa lopes,T boz na Chill na albam yao iliowapa umaarufu mkubwa ni ile waliozindua mwaka 1994 iliojulikana kama ;crazy sex cool" albam hii ilioandaliwa na producer nguli wakati ule dallas austin ilitokana na majina yao yaani lisa alijulikana kama cazy" yaani ni kichaa kweli awapo stage"Tbozz huyu alijulikana kama sex na kweli alikuwa sex yaani mrembo" na Chill huyu alijulikana kama cool nakweli alikuwa cool yaani mpole" miongoni mwa nyimbo ambazo zilizowaweka kwenye chart za billboard sana ni creep" na no srubs" kundi hili lilivunjika na kupotea kabisa hasa bahada ya kifo cha mwenzao LISA LOPEZ na mahasimu zao wakubwa walikuwa ni kundi la x-ecsape liliokuwa chini ya producer jumanne dupriJD pia change face,na swv.