Unalipwa 500,000 TZS? Jaribu kuishi hivi!

Hapo kwenye zaka nimfaidishe mwamposa no way!

hydroxo

adriz de mbusii
 
Uko sahihi, Ikiwa kuna gharama nafuu basi vyema kununua huko. Hii sio mentality ya uongo, ni uhalisia bidhaa nyingi za supermarkets huwa na bei juu kidogo ukilinganisha na wauzaji wa mtaani.
However, kinachoangaliwa ni cost, sio wapi. Nilitaja supermarkets kujenga picha tu.
Ahsante.
 
Karibu, ehe nifanyeje? Maana niliwaza the only solution ni ku grow my sales na kujiongezea mshahara
Wait, Jane!
Nimepitia namba zako...
Na kama umetoa data za ukweli basi you really need help!

Kwa mujibu wa data ulizotoa hapo juu.
Income: 500,000 TZS
Fixed expenses:
Nyumba: 300,000
Dada: 70,000
School bus: 110,000
Umeme: 50,000
Dawasa: 15,000
Total tayari = 545,000 TZS
Hapo bado chakula, usafiri, dharura, au savings. Hii ina maana tayari deficit tayari ni 45k kabla hata ya kula. Kwa lugha rahisi, mfumo wako wa maisha uko juu ya kipato.
Kwa hiyo siwezi kukwambia “panga bajeti vizuri.” Bajeti haitatatua hili. Kuna options tatu tu ambazo financial analysis inatoa, hata ulete personal accountant PhD ya Harvard atakupitisha humu.
Option ya kwanza: punguza gharama kubwa.
Gharama inayoua bajeti hapa ni nyumba. 300k ni 60% ya income. Kitaalamu housing inapaswa kuwa si zaidi 25–30% ya kipato, TENA HAPA NI KWA MAISHA GHALI. Kwa income ya 500k nyumba inapaswa kuwa karibu 120k–150k, HAPANA IKIBIDI HATA 100K. Kama hawezi kupunguza hilo, pressure ya pesa itaendelea.
Option ya pili: ongeza income haraka.
Kwa structure yako ya sasa, realistically unahitaji angalau 800k–1M monthly income ili mfumo huo uwe stable. Hivyo ulichosema kuhusu kuongeza kipato uko sahihi.
Option ya tatu: restructure baadhi ya gharama.
Maswali ya kujiuliza:
Je school bus ya 110k ni lazima au kuna alternative ya bei nafuu?
Je dada wa kazi ni lazima full time au inaweza kuwa part-time?
Je matumizi ya umeme 50k yanaweza kushuka?
Lakini ukweli ni huu: hata ukipunguza kidogo, nyumba 300k bado ni mzigo mkubwa kwa income ya 500k.

Hivyo option ya kwanza na ya pili ni best.
Kwa Ushauri zaidi unaweza kuacha namba yako PM.
Thank you.
 
Vipi hela ya manzi au ndo usajili wa kudumu CHAPUTA a.k.a Bakari Mwamnyeto.
 
Wabongo bhana 😂
Nazungumzia experience yangu mkuu maana hata mwanafunzi wa UDSM anavuta zaidi ya hiyo kwenye Boom + Stationaries + Field allowanaces.

Hiyo hela nilikuwa nalipwa miaka 23 iliopita ndiyo maana nashangaa kama kuna mwajiri anamlipa graduate hiyo pesa kwa mwezi.
 
Nakubali mkuu 😂
 
Hela ya pedi hapo iko wapi?
Na kusuka/kunyoa?
Mafuta ya kupaka je?
Pesa ya taka?
Sabuni ya kuogea na kufulia?

Kwa hizo pirika za kugombea usafiri maji ya kunywa labda achote ya bomba lita 5 aende nayo ofisini. Bajeti ya chakula na maji ndogo. Labda Kama atashindia kacholi..!!
 
Umeniokoa mkuu, nilikuwa naumiza kichwa namna ya kuishi kwa bajeti kama hiyo. Kudos!
 
Naweza kubaliana na wew
 
Hi ni kwa wanaume haswa
Tena single
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…