Unamchango gani kwenye club ya mtaani kwako?

Unamchango gani kwenye club ya mtaani kwako?

Mohammed Khatibu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2018
Posts
1,170
Reaction score
1,617
Leo wakat naenda dukan kupata mahitaj nikakuta pembezon mwa duka kuna vijana wameva jez nikajua fika hawa ni wachezaji.

Wakat nikiendelea kufanya manunuz mmoja akanifuata akanambia; "...shekhe(nilikuwa nimevaa kanzu) sisi ni timu ya hapa mtaani kwetu, huwa tunafanya mazoezi hapo uwanja wa shule ya msingi, tunaomba mchango wako kwa kitu chochote..!

Mi kwakuwa sikuwa na hela ya kutosha nikawapa hela zilizobaki baada ya manunuz, ila bado moyon mwangu kuna roho inanambia nifanye zaidi ya hapa.
 
Umeshawahi kuwepo kwenye hizo timu/klabu ukajua huwa wanatumiaje hizo pesa wanazochangisha/omba?

Kuna ligi yoyote inayoendelea ambayo wao ni washiriki?
  • Wanakodi ndondo?
  • Wanakodi jezi?

Shiriki mara mbili tatu hivi kwenye mazoezi yao na angalau mechi moja ya mojawapo ya ligi walioyojiunga...baada ya hapo, utajua nini cha kufanya.
 
Sawa mkuu

Mkuu umefanya kitu cha maana sana,ukipata mda nenda hata mda wa mazoezi unaweza wachangia hata buku 2 tu,wakikuona tu basi hapo kwa namna moja au nyingine watakuheshimu wewe na familia yako hapo mtaani
 
Mi mchango wangu kwenye timu ya mtaa nimetoa buku mbili tu alafu pia nilikua nacheza no 11 nikipiga cut in kama za kina Robben lazima nifunge goli ila nikawa mjeuri maana ndo nilikua superstar wa timu baada ya kuona jamaa hawanipi heshima yangu nimesusa nimehamia timu ya mtaa wa jirani na mwezi uliopita timu niliyohamia ilicheza na timu ya mtaani kwangu nikacheza na niliifunga goli mbili ila walitaka kunivunja miguu sikumaliza dakika 90
 
Wengine ni wahuni tu wanavaa jezi, wanachangisha michango hali ya kuwa hawana mechi wala nini, hizo wanaenda gawana.
 
Michango ya kijingajinga Huwa sichangi Kwa sababu hayo ndio mambo yanafanya watu wasiwe bize na kazi Kwa sababu zipo njia nyepesi za kupata pesa. Hebu fikiria mtu upo bize unaenda kazini wenzetu wapo vijiweni na vitisheti na mipira kuomba michango ya mechi
 
Katika andiko langu mnamo mwaka 2014 nilielezea mambo ya kuweza kuifanya Ligi yetu kuwa bora; moja wapo lilikuwa kufanya kila mechi ionyeshwe kwenye luninga (hilo limefanywa)... Moja ya mambo ambayo nilishauri ni kufanya juhudi za nguvu kuwa na vilabu regional yaani watu wawe na mwamko wa kushabikia timu zao (hilo litaleta ushindani ) badala ya kuwa na mashabiki glory hunters...
 
Mi mchango wangu kwenye timu ya mtaa nimetoa buku mbili tu alafu pia nilikua nacheza no 11 nikipiga cut in kama za kina Robben lazima nifunge goli ila nikawa mjeuri maana ndo nilikua superstar wa timu baada ya kuona jamaa hawanipi heshima yangu nimesusa nimehamia timu ya mtaa wa jirani na mwezi uliopita timu niliyohamia ilicheza na timu ya mtaani kwangu nikacheza na niliifunga goli mbili ila walitaka kunivunja miguu sikumaliza dakika 90
Hii michezo ya timu za mitaani hukawii kuvunjwa mguu na kuingizia familia shida zisizokuwa za lazima! Niliwawahi kucheza mpira wa timu za mitaani miaka hiyo nimemaliza six! Kaja jamaa kunikaba kanipelekea moto wa mtama nikaangukia kichwa karibu nivunje kichwa! Tangia hapo sitaki kusikia! Wengi wao wanavuta bangi na hawajui sheria za mpira!
 
Back
Top Bottom