Unamchukuliaje mama yako ambaye hataki kukupa ukweli kuhusu baba yako mzazi na kuacha utumie ubini wa mtu mwingine?

Lanlady
 
Ni kweli madingi huwa wanafanya blunders nyingi sana lakini mwisho wake huwa wanakuwa Wana majuto sana huyu Lanlady asipaniki wala asijisikie vibaya aendelee na mishe zake tu. Ipo siku huyo Baba anayezingua Atakuja kumuomba msamaha. Cha msingi aeleleze akili yake kwenye maisha yake tu
 

Ipo mifano mingi sana. Kumpa pressure Mama ni kumuonea maana kuna wakati alifanya maamuzi ili mambo yasonge mbele.
Amuelewe especially kama na yeye anayelalamika ni mwanamke. Hujafa hujaumbika
 
Ipo mifano mingi sana. Kumpa pressure Mama ni kumuonea maana kuna wakati alifanya maamuzi ili mambo yasonge mbele.
Amuelewe especially kama na yeye anayelalamika ni mwanamke. Hujafa hujaumbika
Ni kweli na ndio maana Niliandika hapo post #3
 
Hakikisha unamjua Baba yako mzazi kuna FAIDA kubwa kuliko hasara .

Baba ndo anabariki watoto
Baba anatoa muongozo
Baba ndo Mungu wako.

Hata ukitaka kufanya ibada za mizimu kutambika kuondoa mambo mabaya you need to use the name of ur Fathers.

So keep this in mind .
 


In spiritual Baba ni muhimu Sana akufahamu Kama yupo na akupe mkono wake .

Fatilia umjue Baba yako halisi you will never remain the same .
 
Fanya mishe zako achana na mtu asitaka umjue, kama baba ana uhitaji na wewe angeshakupata maana ni rahisi kwa yeye kukutafuta wewe kuliko wewe kumtafuta yeye.

Na vipi ukampata na still akakukataa vilevile, achana na wanaosema sijui baba ndio mungu wako, sijui kabeba baraka ni imani zao ambazo sio lazima ziapply kwako.

Mama anawezakua alipitia jambo gumu ukapatikana wewe, na vipi kama nae hamjui baba yako halisi ni yupi. Mshukuru Mungu alikuzaa, hakutoa mimba, alikulea hakukutupa kama wanawake wengi wafanyavyo.

Mfurahie mama yako, mama yako ndio baba yako. Muelewe.
 
Kwanza fatilia struggle za Mama yako pindi akiwa na mimba yako. Ukute alikataliwa,alisimangwa,alinyanyanswa etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…