Unamchukuliaje mtu ambaye mnapokutana kwa muda mfupi tu, tayari ameshajinadi sifa zake zote?

Unamchukuliaje mtu ambaye mnapokutana kwa muda mfupi tu, tayari ameshajinadi sifa zake zote?

royal tourtz

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Posts
255
Reaction score
326
Za jumapili wadau. iko hivi,

Unaweza kutana na mtu yeyote inaweza kuwa kwenye gari au njiani au kaja hapa hapo dukani au ofisini kwako kwa namna yoyote ile..

Ile katika kuongea ndani ya nusu saa ameshakuambaia kazi anayofanya, mshahara, wanawake aliopitia kama ana nyumba au gari.. au gharama ya nyumba aliyopanga. Kama ameshafirisika atakuambia kazi zote za nyuma alizowahi kufanya na ndoto zake.

Sasa mimi huwa najiuliza yote hayo unaniambia yanasaidia nini na ili iweje hali hatuna chochote cha kutuunganisha ni leo tu imetokea tumeonana.

Labda kuna wadau humu huwa mnawaelewa hawa watu wanataka nini ili nisiwe nawahukumu bure kumbe wana nia njema.
 
Unamsamehe unaendelea na mambo yako.. Easy
 
Unatakiwa umtumie vizuri, ndani ya mwaka mmoja nawe unakuwa na nyumba yako na biashara.
Kuna wanawake wabobezi, wanapenda sana ufunguke 'code'; ndio maana wengine wanatamani ulewe kwanza uwe mwepesi wa kumwaga hela.
 
Hao ni wagonjwa wa akili. Wana Narcissistic Personality Disorder (NPD)

Screenshot_20220327-082722_Chrome.jpg

Screenshot_20220327-082613_Chrome.jpg
 
Mimi nadhani watanzania tunaishi kijamaa ndio maana haya mambo hutokea. Just imagine umepanda daladala halafu mtu anaanza kukupa mambo yake yote, ya mkewe, watoto, kazini, mtaani...maisha ya binafsi kabisa....can you imagine watanzania tulivyo.


Ukiwa kwenye daladala, kama unataka kuanzisha mada, just say, NCHI HII BWANA....[emoji23][emoji23]

Then sikiliza watu watakavyoanza kuongea. Ndivyo tulivyo, ndio mazingira yetu, kwa wenzetu mtu anapanda daladala na novel yake, ataisoma mwanzo wa safari hadi mwisho, akifika anashuka, vijana wao wameweka headphones masikioni, ni mziki kwa kwenda. Jamii tofauti tu..
 
Back
Top Bottom