Unamfanyaje Ndugu yako aliyekutapeli MILIONI 5 na sasa anakutukana, anakublock na kukutambia ?.

Hivi jamani mbona hatuna marafiki wema wa aina hii..anaeweza kukupata milioni 5 na ukawa mwaminifu na kumrudishia ukishamaliza shida zako? Wengine tunataman hata laki Tano tu...sembuse milioni 5? Dah haya.
 
Next time toa ambacho upo tayari kupoteza,
By the way njoo sumbawanga tumalize tatizo, wiki tu anazikwa huyo. Kama mbwai mbwai tu.
 
Achana nae.

Hana hela huyo
 
Kama ni ndugu yako mmezaliwa baba mmoja na mama mmoja achana naye, endelea na maisha yako. Ndugu yako ni ndugu yako tu, atarudi mwenyewe....ni suala la muda tu
hata hivyo tumesikiliza upande mmoja wa shilingi hivyo haitoshi kuhukumu...
 
pole sana ndugu hakopeshwi kama anashida ya 5ml ni bora umwambie nina 1m,2m au 3m au sina kabisa na ukimpatia mpatie kwa mashariti akiichezea asiludi tena kukuomba msaada..Mimi ndugu huwa simkopesh
 
Wewe huna hela ya kumkopesha mtu, wacha kujinyanyua mabega.
 
Huyo kama ni ndugu wa tumbo moja inaonekana alikuwa na husda na wewe sasa akatafuta namna ya kukutia hasara kwa lazima ndio maana akakukopa, sasa hilo la kukutukana na kutokukulipa ndio anatimiza ile kiu yake ya kukukomesha.

Ushauri:Achana nae wala usimdai maana hapo hutapata kitu kama hana nia maana hamkuandikishana,fanya kama huna ndugu hapo,kuna siku atarudi tu kukutafuta tena akiwa na hali mbaya.
 
Huyu tumezaliwa tumbo moja Mkuu.

Naongea haya nikiwa kwenye Kipimo Changu cha juu cha maumivu yaliyojawa na Hasira ndani yake , nikama vile kua kwetu mbalimbali ndiko kunachelewesha nisifanye Tukio .

Yaan kwann anitukane ? Aniblok? Anitambie ?.
Muachie Mungu. Kama uliweza kupata 5m ukampa basi unaweza kupata nyingine. Dunia itamfunza.
 
Milioni 5 isikupeleke jela Mkuu,

Kuna mzee niliongea juzi tu hapa anasema kama anaweza kukwepa Jela kwa namna yeyote atafanya. anasema alishamkamata mke wake na Kijana dereva fuso Gesti alichofanya aliwaangalia tu, mke akamwambia Chukua chako ondoka, jamaa hakumfanya kitu.

Anasema alishawahi kukorofishana na mzee wake, Mzee akamtupa jela mwaka 1 anasema hatamani tena kurudi huko na ndio maana hakumfanya lolote mgoni wake.
 
Huyo kama unaona anazo wala sio wa kusamehe kwani panga zimeisha acha uzembe mzukie asubuhi na mapema mwamshie kijiji kizima kwa zogo la maana mbona atazitoa tu
 
Huyo ni kama naniliu aliyeiba kura halafu anataka maridhiano
 
Usiuwe mpige kimbola Cha afutatu akahangaike Nako ubaya ubwela 😂 😂 malipo apa apa duniani juu mahesabu.
 
Ni nani aliyesema kila jambo ili litambuliwe rasmi lazima liwe katika maandishi?
Hapo amua moja kati ya haya
1. Mpeleke polisi kwa kosa la utapeli au mahakamani kwa kosa la madai.
2. Msamehe kwa kutumia ujumbe mfupi yaani sms tu then usiwe na ushirika naye kwenye jambo lolote.
Kinyume cha hapo utapoteza vitu vingi zaidi
 
Usitoe ahadi ukiwa na furaha wala usichukue maamuzi ukiwa na hasira,

Huyo mpotezee,achana nae kabisa,yani piga kimya,mfute kabisa,nina uhakika siku inakuja huko mbeleni,yeye ndiye atakayekutafuta,

Muache ateseke kwa ukimya wako,hilo litamtesa sana coz hatajua unawaza nini au utamchukulia hatua gani,kitendo cha kujibizana nae kinampa faida ya kusoma udhaifu wako,na amesha ona kua huna la kumfanya,

Piga kimya,endelea na maisha yako ila utakua umepata fuzo,

All the Best.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…