Unamfunga Mbowe kisha unakatiwa misaada na mikopo na zaidi kutakiwa kuimarisha utawala bora na demokrasia

Nchi ilitengeneza taswira mbaya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni,sasa ni lazima jambo lifanyike la kujisafisha na kwamba hatuko tena kule.
Katika kutimiza azma hiyo,ni lazima wachache wenye political power kutoka vyama vya upinzani,wapitie maumivu ya hapa na pale.Mwenendo tu wa kesi unatoa picha halisi hata kwa mtu ambae hajasomea sheria.


Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Hii inayoitwa kesi ni uwendawazimu mtupu, kuanzia jaji, waendesha mashtaka, polisi mpaka mashaihidi wao. Ni ujinga mtupu. Ndiyo maana Afrika hatuendelei, na tutaendelea kudharaulika Duniani kote kama race duni kuliko zote.

Tuna matatizo mengi lukuki, lakini tunapoteza muda kuhangaika na ujinga.

Tunashindwa kupata muda na rasilimali za kutengenezea mabwawa ya hifadhi ya maji ya kutosha lakini tuna fedha na muda wa kuendesha kesi za kijinga kabisa kama hii ya Mbowe.

Samia kuna maeneo, kiasi ameonekana kujitahidi, lakini kwa kesi hizi za kijinga, hatakumbukwa kwa lolote la maana. Anazunguka huko na huko, kuwadanganya wazungu kuwa anasimamia haki, anafikiri wazungu ni wajinga wa kuamini manebo yake bila ya kuangalia yale anayoyatenda!!

Awaamrishe hao majaji vibaraka wake wamfunge Mbowe haraka, ndiyo atawajua wazungu.
 
bahati mbaya sana ni kwamba, mabeberu hao hao wamesema kesi ipo mahakamani, watu wasubiri mahakama itoe haki. pia, kila kukichwa wapo ikulu wanamtembelea samia na kuahidi kutoa misaada. hamuwezi kutuchongea tena kwa mabeberu tukanyimwa misaada na kupata shida kama kipindi cha jpm, sasaivi hata Tundu lisu kule ulaya hana faida kwasababu wazungu wameshapatana na samia. Mungu ibariki Tanzania.
 
Kwani Mbowe ndo mtoa mikopo na misaada?!??!!!
 
Unaotaa we mkaka unaotaa unaota wee mdada unaoota [emoji23][emoji23]
 
Serikali inamkono mrefu. Tunaangalia huo mkono ulivyowananasa makomando wastaafu
 
Hatutakiwi kutegemea wazungu watatulie mambo yetu. Tunatatakiwa tuseme hii siyo sawa na haikubaliki kwa vyovyote vile au ni sawa na iendelezwe.
Fikra za kuwategemea wazungu ndipo msingi wa umasikini ulipojengeka.
Ingekuwa vizuri sana ungemalizia ndiyo atawajua wananchi badala ya wazungu.
 
Anafungwa tu na mikopo haisimami.
 
Kama atapatikana na hatia atafungwa tu ,tusitishane ,hii ni nchi huru ,Ina Sheria zake ,lazima zifuatwe
 
Nakubaliana nawe.
 
Na Mungu ndiye atayafanya haya! Ni Mungu wa mabeberu au wa Mbowe! au Mungu mmoja tu tunaye mjua? Mbona huyu Mungu anapendelea upande mmoja?
 
Hiyo nayo ni kesi yenye sifa za kuitwa kesi?

Shahidi anaingia na madesa mahakamani na bado anendelea kuaminiwa na mahakama?

Mambo haya ni kwenye hii nchi ya giza tu.
Naamini unafuatilia kesi humu JF kwa jinsi inavyoletwa. Ukitaka kujua uhalisia wa mwenendo wa kesi ni jambo jema ukahudhuria hasa siku ambayo Jaji husoma hukumu ya kesi ndogo ndogo (za pingamizi).

Mfano wa madesa unauchukulia kishabiki zaidi kuliko ukweli wenyewe. Labda kama utatoa hoja za kisheria dhidi ya hukumu ya madesa kukubaliwa
 
Kesi iko mahakamani wewe unaleta habari ya vikwazo na kunyimwa misaada- unapoteza mda bure kwa kuelekeza nguvu nje ya mahakamani
 
Awamu ya Hayati Magufuli haiwezi kukwepa lawama za kuulea sana ugaidi wa mbowe. Bora sana rais wa sasa ameamua kuumaliza kabisa huu mchezo. Mbowe ni gaidi, awamu ya tano ilimlea sana.
 
hua nakuona bright kumbe ni hamnazo kiasi hiki? mzungu hawezi kuusaidia upinzani lolote kama serikali inadeliver wanachotaka, sana sana atatoa vijitamko vya kinafiki bila kuchukua hatua yoyote, tizama wanachofanyiwa wapinzani uganda & rwanda kisha jiulize hao mabeberu wamechukua hatua gan kisha linganisha na ulichoandika hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…