Ntozi
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 226
- 300
Nchi ilitengeneza taswira mbaya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni,sasa ni lazima jambo lifanyike la kujisafisha na kwamba hatuko tena kule.Mungu ana makusudi kwa kila jambo, na mojawapo ya kusudi la Mungu katika hii kesi ya Mbowe, ni watawala kubanwa kimataifa ikiwamo kupunguziwa au kunyimwa kabisa mikopo na misaada iwapo Mbowe atafungwa.
Hawataishia hapo, wataongeza mbinyo kutaka aachiliwe na zaidi watataka mabadiliko ya katika mifumo yetu ya.kutoa haki sambamba na kutaka demokrasia iheshimiwe na hata kushinikiza Tume huru moja kwa moja, au kupitia shinikizo la demokrasia na utawala bora..
Kwa kifupi, wanaoitwa Mabeberu watakuwa wamepata mwanya au upenyo wa kuingiza agenda zao na ambazo obviously zitawagharimu watawala na chama chao kwa ujumla.
Hivyo, kuna gharama ya kulipa kitaifa na kimataifa, wapo Mbowe atafungwa, gharama ambayo itakuwa ni gharama ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na chama tawala ndio kita-suffer zaidi.
Madaraka bila maarifa ni maafa.
Mtakuja kuniambia.
Katika kutimiza azma hiyo,ni lazima wachache wenye political power kutoka vyama vya upinzani,wapitie maumivu ya hapa na pale.Mwenendo tu wa kesi unatoa picha halisi hata kwa mtu ambae hajasomea sheria.
Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app