Asante kwa kuleta uzi huu hapa mkuu! Nina mengi ya kuandika kuelezea stori ya crush wangu lakini acha tu nifupishe maana huwa nikisimulia huwa kama ni love story inafaa hata kuchezewa movie! #Huyu dada kwa mara ya kwanza nilikutana naye kanisani, nilikuwa darasa la tatu, na umri wangu wa miaka kumi! Kwa mara ya kwanza moyo ulipasuka kwa mapenzi, yule dada aliingia moja kwa moja kwenye chumba cha moyo akakaa humo nakuishi. #Dada huyu alikaa moyoni kwa miaka 14 bila kutoka na kwa muda wote huo sikuwahi kumwambia ingawa wakati ule wa utoto aliweza kunigundua kama nipo nyang'anyang'a kwake coz body language zetu ziliongea hususani macho kila tulipokuwa tukikutana hasa kanisani, hakuna mahubiri yalikuwa yakiingia, yeye ndo alikuwa hubiri langu! Shida katika utoto ule wa kishule ya msingi ilikuwa ni uoga( udomo zege). # Uncondition love yangu kwa huyo dada ilikuja kushuka asilimia zake nikiwa na miaka 24. Kwa sasa yupo kwenye ndoa yake! Na mchango nilitoa, na tu marafiki.